Wabara ondoeni shaka, ardhi ya SMZ Bagamoyo si sehemu ya Zanzibar. SMZ haina hati; limetelekezwa miaka 45 ila Zanzibar inamiliki kihalali

Umesahau miaka ya nyuma wafungwa walikuwa wanatoka zenji
Na kuja kufanya kazi kwenye ranchi hiyo
Kulikuwa na mpaka gereza lao

Ova
Hili sikuwahi kulijua ndio nalisikia leo, ila hakuna tatizo, hao wafungwa ni Watanzania hivyo wanaweza kufanyishwa kazi popote. Hata wale masheikh wa uamsho, walishikiliwa kwenye magereza ya huku bara!.
P
 
Nampongeza sana Pasacl Mayalla, ni mtu mwenye IQ kubwa sana na kuweza kuelewa anachosema inabidi uwe umepata A au B kwenye somo la Constitutionalism and Legal Systems of East Africa; Kwetu sisi akina Shivji wadogo tunamwona kama Mchochezi na atakiwa kupingwa kwa nguvu ya HOJA,
ameonyesha uchochezi wa aina 2, sio kweli kuwa Zanzibar inapewa 4.5% ya Mikopo yote, huo ni uongo mkubwa sana. Pili, kwenye doctrine ya adverse Possession doesn't apply kwenye ardhi inayomilikiwa na mtu mwingine, doctine of adverse possession ina apply kama wavamizi wanamevamia bila kupewa na mtu yeyote na bila kuwa na taarifa kuwa hili eneo ni la Mtu mwingine
 
Hili sikuwahi kulikua ndio nalisikia leo, ila hakuna tatizo, hao wafungwa ni Watanzania hivyo wanaweza kufanyishwa kazi popote. Hata wale masheikh wa uamsho, tumewashikilia kwenye magereza ya huku bara!.
P
Huko nimezunguka kote miaka hiyo
Hadi nkaonaga vibao vimeandikwa
smz ,ndomana sioni jambo geni

Ova
 
Nimeshanga sana kuona watu huku wanaona jambo geni
Kweli watz wako nyuma sana kujua mambo

Ova
No sio wako nyuma, bali ni watu wa ajabu sana!. Utakuta hapa wanapiga kulele kusikia Zanzibar ina eneo bara, lakini kuna ma settles walikuwa na maeneo kama yule Mzungu Steyn mwenye ushamba ya ngano kule Malbadawi Hanang, Mashamba ya chai ya Mufindi yanamilikiwa na Brookebond, Pale Kisarawe Luna eneo la hectares 27,000 ni shamba la Sun Biofuels, walalima mibono kaburi kuzalisha Biofuels. Kule Machame Luna mzungu na mkewe, Silverdales, wamedhulumiwa shamba lao, no one complains lakini Mzanzibari kuwa na eneo bara... nongwa!.
P
 
Wewe Paskali serikali yako ina eka 6,000 katika nchi gani hapa duniani?
 
Thanks my fellow leaned brother, eneo hilo ni kubwa na abandoned for 45 years mpaka juzi, kama mtu alivamia akiwa pale, ameoa, watoto wamezaliwa na sasa ni wajukuu!, mtu kama huyo unamuhamishaje?.
P
 
Usichanganye mambo katika uelewa wa umiliki mashamba.
Hao uliowataja ni aidha kampuni zilizoandikishwa kisheria na zikapewa umiliki wa ardhi kwa masharti yaliyopo Ardhi, au ni watu binafsi waliomilikishwa mashamba wa muda maalum na masharti maalum na watakuw na Certificates of Occuppacy yaani Title(Hati)
 
Hakuna tofauti umiliki huo wa Zanzibar na umiliki mwingine wowote, tofauti ni moja tuu, SMZ wana barua ya kibali, hawana hati!.
P
 
Hoja ya kwamba wa bara wakiruhusiwa kumiliki ardhi Zanzibar kisiwa kitazama yani ukimaanisha kitajaa sana haina mashiko

Lakini umesema Zanzibar ni sehemu ya bara iliyomumunyika na kuwa kisiwa mistari michache chini yake ukayataja maeneo ya bara ambayo yalikuwa ni sehemu ya Zanzibar ikaipatia bara

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Tatizo kubwa la Zanzibar Chao ni Chao wakati Cha kwetu ni Cha wote. Ardhi SI swala la Muungano, mtanzania bara kumiliki ardhi ni dhambi kubwa sana.
Hoja ya kwamba wao Wana eneo dogo Haina nguvu kwani hata population Yao ni ndogo na kwa Kasi tuliyonayo SI muda mrefu hii ardhi itakuwa haitoshi.
Kwa mujibu wa katiba ya Muungano Kuna mambo manane ya Muungano ikiwamo gesi na mafuta na utaratibu wa kuyaondoa ni kupata theruthi mbili za Baraza la wawakilishi na theruthi mbili za bunge la jamhuri ya Muungano ila walipohisi Wana mafuta waliliondoa kinyemela hili swala kuwa la Muungano kwa hofu rais akitoka bara hawatanufaika nitaomba siku Moja Pascal kwa sababu wewe sio tu mwandishi ila umesomea sheria uliandikie Makala. Ila rais alipokuwa Toka upande wao mkataba wa gesi ndio wa kwanza kukusanya na Kenya je sisi watanganyika kwanini tusiwe baa wasiwasi kuwa wanatapanya Mali zetu.
Kwa kifupi kama katiba ya Muungano ilivunjwa wakakaa kimya ni swala la muda huu Muungano wa kimchongo kuvunjika.
Warioba katika rasimu Yao alisema ni hero watanganyika wakapewa serikali Yao kabla hawajaidai ikifikoa hatua ya kudai uwekezaji na uporaji unaofanywa na Zanzibar kwa kisingizio Cha Muungano vyote vitataifishwa
 
Mimi mwenyewe Nina kiwanja pale KIBUYUMIMBA na ni eneo hilo hilo la RAZABA
 
Wakati Nyerere anawapa Zanzibar ardhi huko Bagamoyo miaka ya 1970s kulikuwa na sababu ya msingi. Biashara zote zilikuwa zikifanywa na serikali (mfano RTC, NMC. NAFCO, nk). Hakukuwa na wafanya biashara binafsi ambao wangepeleka ng'ombe Zanzibar. Hivyo, ilikuwa muhimu SMZ ifanye kazi ya kununua ng'ombe bara, kuwapa malisho kwenye Ranchi bara, na kisha kuwapeleka Zanzibar kwa ajili ya nyama, nk.

Mambo yalipobadilika kukawa na wafanya biashara binafsi (private enterprise), hilo jambo halikuwa muhimu tena, ndo maana Znz walitelekeza Ranchi Kwa miaka 45!

Hata kwa sasa, awamu ya sita, hakuna sababu za msingi za Smz kutaka tena hilo eneo.
 
Hao wamekuja kama wawekezaji wa kigeni. Na pengine wengine ni raia kamili. Sasa sisi na Zanzibar tulipoungana tulikubaliana kuwa kila mtu atabaki na ardhi yake. Kuwa ardhi siyo suala la Muungano. Ukitaka kwenda kwa mwingine utaenda kuwekeza kama raia wa kigeni. Hivyo ndivyo inavyotakiwa. SMZ inawakilisha raia wote wa Zanzibar. Wakitaka ardhi Tanganyika lazima waje kama wawekezaji wa kigeni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…