mrangi
JF-Expert Member
- Feb 19, 2014
- 88,759
- 123,368
Nimeshanga sana kuona watu huku wanaona jambo geniNi kweli Watanzania walio wengi ni wazito sana kuelewa hata vitu vidogo tuu vya kawaida.
P
Kweli watz wako nyuma sana kujua mambo
Ova
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nimeshanga sana kuona watu huku wanaona jambo geniNi kweli Watanzania walio wengi ni wazito sana kuelewa hata vitu vidogo tuu vya kawaida.
P
Hili sikuwahi kulijua ndio nalisikia leo, ila hakuna tatizo, hao wafungwa ni Watanzania hivyo wanaweza kufanyishwa kazi popote. Hata wale masheikh wa uamsho, walishikiliwa kwenye magereza ya huku bara!.Umesahau miaka ya nyuma wafungwa walikuwa wanatoka zenji
Na kuja kufanya kazi kwenye ranchi hiyo
Kulikuwa na mpaka gereza lao
Ova
Huko nimezunguka kote miaka hiyoHili sikuwahi kulikua ndio nalisikia leo, ila hakuna tatizo, hao wafungwa ni Watanzania hivyo wanaweza kufanyishwa kazi popote. Hata wale masheikh wa uamsho, tumewashikilia kwenye magereza ya huku bara!.
P
Eneo lote la Zanzibar ni eneo la JMT, hata wewe ukitaka unapata eneo Zanzibar kama mwekezaji.Tanzania bara yenyewe inasemekana
Nao huko unguja wana sehemu yao pia
Ova
No sio wako nyuma, bali ni watu wa ajabu sana!. Utakuta hapa wanapiga kulele kusikia Zanzibar ina eneo bara, lakini kuna ma settles walikuwa na maeneo kama yule Mzungu Steyn mwenye ushamba ya ngano kule Malbadawi Hanang, Mashamba ya chai ya Mufindi yanamilikiwa na Brookebond, Pale Kisarawe Luna eneo la hectares 27,000 ni shamba la Sun Biofuels, walalima mibono kaburi kuzalisha Biofuels. Kule Machame Luna mzungu na mkewe, Silverdales, wamedhulumiwa shamba lao, no one complains lakini Mzanzibari kuwa na eneo bara... nongwa!.Nimeshanga sana kuona watu huku wanaona jambo geni
Kweli watz wako nyuma sana kujua mambo
Ova
Wewe Paskali serikali yako ina eka 6,000 katika nchi gani hapa duniani?Wanabodi,
Kama kawaida yangu kila nipatapo fursa huja na kwa maslahi ya taifa.
Maslahi ya leo ni hii issue ya SMZ kumiliki eneo la ekari 6000 Bagamoyo. Tangazo la SMZ Zanzibar: Hekta 6,000 zilizopo Bagamoyo ni mali yetu
limeleta taharuki na sintofahamu kubwa kwenye mitandao ya kijamii hadi baadhi ya watu kutoa povu!.
Kuna watu wanatafsiri potofu kuwa sehemu ya Ardhi ya Tanzania Bara ni sehemu ya Zanzibar!.
Ukweli ni huu
Anza na bandiko hili la mwaka 2014 iujue historia ya eneo hilo lilimilikiwa vipi na Zanzibar Zanzibar ndani ya Tanganyika ilianzia huku kisha soma majadiliano ya Bunge ya miaka ya nyuma kuhusu issue hii.
View attachment 2644793
Shamba la Mifugo Linalomilikiwa na SMZ huko Bagamoyo
MHE. MOSSY SULEIMANI MUSSA aliuliza:-
Kwa kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliwahi kuwa na shamba kubwa la mifugo (ng’ombe) ranchi huko Bagamoyo:-
(a) Je, Serikali ya SMZ bado inamiliki shamba hilo? (b) Je, hadi kufikia kuboreshwa kwa shamba hilo SMZ ilitumia shilingi ngapi?
NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na uvuvi naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mossy Suleimani Mussa Mbunge wa Mfenesini lenye vipengele (a) na (b) kwa pamoja kama ifuatavyo:-
(a) Mheshimiwa Spika kwa kuzingatia Ranchi ya Zanzibar Bagamoyo (RAZABA) iliyoko Makurunge katika Wilaya ya Bagamoyo inamilikiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Ranchi hiyo ilianzishwa mwaka 1976 baada ya kupata kibali kutoka kwa Kamishna wa Ardhi chenye kumbukumbu namba LD/70254/12/TBR cha tarehe 24/09/1971, hivyo kwa taarifa hizo Wizara yangu bado inaamini shamba la RAZABA bado ni mali ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, hata hivyo kwa vile swali linaloulizwa na Mheshimiwa Mbunge linahusu mali zilizo chini ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi sio Wizara ya Muungano napenda kumjulisha Mheshimiwa kuwa Wizara yangu haiwajibiki kujua kama Serikali ya Mapinduzi Zanzibar bado inamiliki au haimiliki shamba hilo.
(b) Mheshimiwa Spika, Wizara yangu haijui kama shamba hilo ambalo liko chini ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar lilitumia shilingi ngapi katika kuliboresha, namshauri Mheshimiwa Mbunge akapate majibu ya takwimu hizo Wizara inayohusika katika Serilkai ya Mapinduzi Zanzibar.
WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI:
Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Naibu Waziri naomba kutoa maelezo ya nyongeza kama ifuatavyo.
Mheshimiwa Spika, shamba hilo ambalo ni kweli kama alivyosema Naibu Waziri lilimilikishwa kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar lakini kwa miaka mingi sana karibu 30 halitumiki, kwa hivi karibuni Serikali imemega sehemu na kuwapa wawekezaji, watawekeza katika mambo ya biofuel na Sehemu bado inaendelea kuwa mali ya SMZ.
View attachment 2644761
My Take
Hivyo Watanzania wenzangu isiwe na wasiwasi kabisa kuhusu hili, after all eneo lote la Zanzibar ni sehemu ya JMT hakuna sababu ya watu kutoa povu, Wanzanzibari kuniliki Ardhi Bara lakini Wabara hawewezi kumiliki ardhi Zanzibar, kwasababu Wazanzibari ni Watanzania wenzetu wana haki zote za Utanzania, ila Zanzibar ni the minority, visiwa vyao ni very tiny, tukiruhusu kila Mtanzania kumiliki ardhi Zanzibar, itaelemewa na kuvizamisha visiwa vile!.
- Wabara ondoeni shaka kuhusu umiliki wa SMZ eneo Bagamoyo, SMZ inalimiliki eneo hilo kihalali kabisa kwa vile walipewa na Mwalimu Nyerere.
- Kitendo cha SMZ kumiliki eneo huku Tanzania bara, hakulifanyi eneo hilo kuwa sehemu ya Zanzibar, ni eneo halali la SMZ ila ardhi ni ya Tanzania bara.
- Nchi yoyote inaweza kumiliki eneo nchi nyingine yoyote, umiliki huo haulifanyi hilo eneo kuwa sio sehemu ya nchi husika.
- Japo SMZ inalimiliki eneo hilo lililokuwa hekta 6,000, kwanza SMZ, haina hati ya umiliki bali ina kibali cha umiliki No. LD/70254/12/TBR cha tarehe 24/09/1971.
- SMZ ililitelekeza eneo hilo kwa miaka 45, hivyo serikali ikalimega kumpa mwekezaji, Halmashauri ya Bagamoyo imelipima viwanja inaviuza.
- Kwa vile ni eneo halali la SMZ, na sasa SMZ imeibuka kuonyesha ina interest na eneo lake, then itarudi serikalini kuelezea hiyo interest, serikali itakwenda kulipima limebakia kiasi gani, SMZ itapimiwa upya na kugawa.
- Iwapo SMZ bado italihitaji eneo lote la awali la ekari 6,000, then italazimika kuwalipa fidia watu wote waliomegewa kihalali.
- Kama pia limevamiwa na wananchi, then sheria yetu ya Ardhi ya Vijiji No. 5 ya mwaka 1999 will apply kwa mtu aliyetelekeza eneo lake kwa miaka 45, wale wavamizi wana haki fulani.
- Ikionekana madhara ya kuwaondoa wavamizi ni makubwa kuliko kuirejeshea SMZ eneo hilo, then kile kibali cha umiliki wa SMZ kinafutwa, wananchi wanapimiwa, na SMZ wanapewa eneo jingine, tuna mapori kibao ya kumwaga, hata wakitaka heka 10,000 wanapewa.
- Hii ya kuwagaiya wavamizi imefanyika sana kwenye maeneo ya jeshi na maeneo ya RTD, wavamizi wamepimiwa na kuhalalishiwa!.
Wakati wa kuumbika nchi, Zanzibar ilikuwa eneo la bara likamegeka kwa sea erosion, hivyo Visiwa vya Zanzibar ni sehemu halali ya Tanzania bara ndio maana dhima ya muungano wetu adhimu ni udugu, sisi ni ndugu moja, Waarabu walipokuja Zanzibar ile 1732 Sultan Seyyid Said alipohamoshia Sultanet take toka Oman kuja Zanzibar, aliwakuta wenyeji halisi ni Wahadimu, kutoka Bara, alivitwaa visiwa hivyo toka ukoo wa Mwinyimkuu, na waliompindua Sultan kwenye yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ni wajukuu wa Mwinyimkuu wenye Zanzibar yao, ndio maana slogan ya Mapinduzi Daima ipo, na baada ya muungano tumekuwa kitu kimoja, ndio maana slogan ya muungano ni tutaulinda kwa gharama yoyote.
Miongoni mwa gharama hizo ni kumsamehe madeni, kumpa 4.5% ya fedha za mikopo na misaada, ajira na hata kumpa eneo lolote Wazanzibari watakalotaka.
Watanzania bara tujifunze kuwa na shukrani, tushukuru sana Zanzibar, ukanda wa eneo la maili 10 ya Pwani ya ya bahari ya hindi, lilikuwa eneo la Zanzibar, ikatugawia!, miji yote ya Pwani kuanzia Dar, Tanga, Bagamoyo imejengwa na Sultan of Zanzibar!
Hata mjengo wa Ikulu ya Magogoni, imejengwa na Sultan of Zanzibar, hata ile replica ya Ikulu pale Chamwino ni mjengo wa Kiarabu!, mbona watu mnakosa shukrani kwa mambo mazuri kama haya, mnaona nongwa Zanzibar kumiliki eneo huku Bara!
Mapinduzi Daima
Muungano Tutaulinda kwa gharama yoyote!.
Paskali.
Thanks my fellow leaned brother, eneo hilo ni kubwa na abandoned for 45 years mpaka juzi, kama mtu alivamia akiwa pale, ameoa, watoto wamezaliwa na sasa ni wajukuu!, mtu kama huyo unamuhamishaje?.Nampongeza sana Pasacl Mayalla, ni mtu mwenye IQ kubwa sana na kuweza kuelewa anachosema inabidi uwe umepata A au B kwenye somo la Constitutionalism and Legal Systems of East Africa; Kwetu sisi akina Shivji wadogo tunamwona kama Mchochezi na atakiwa kupingwa kwa nguvu ya HOJA,
ameonyesha uchochezi wa aina 2, sio kweli kuwa Zanzibar inapewa 4.5% ya Mikopo yote, huo ni uongo mkubwa sana. Pili, kwenye doctrine ya adverse Possession doesn't apply kwenye ardhi inayomilikiwa na mtu mwingine, doctine of adverse possession ina apply kama wavamizi wanamevamia bila kupewa na mtu yeyote na bila kuwa na taarifa kuwa hili eneo ni la Mtu mwingine
Usichanganye mambo katika uelewa wa umiliki mashamba.No sio wako nyuma, bali ni watu wa ajabu sana!. Utakuta hapa wanapiga kulele kusikia Zanzibar ina eneo bara, lakini kuna ma settles walikuwa na maeneo kama yule Mzungu Steyn mwenye ushamba ya ngano kule Malbadawi Hanang, Mashamba ya chai ya Mufindi yanamilikiwa na Brookebond, Pale Kisarawe Luna eneo la hectares 27,000 ni shamba la Sun Biofuels, walalima mibono kaburi kuzalisha Biofuels. Kule Machame Luna mzungu na mkewe, Silverdales, wamedhulumiwa shamba lao, no one complains lakini Mzanzibari kuwa na eneo bara... nongwa!.
P
Ikitokea serikali yetu haina eneo kubwa hivyo, huu ni uzembe wetu, ila kwenye Balozi nyingi, yale majengo ni yetu.Wewe Paskali serikali yako ina eka 6,000 katika nchi gani hapa duniani?
Hakuna tofauti umiliki huo wa Zanzibar na umiliki mwingine wowote, tofauti ni moja tuu, SMZ wana barua ya kibali, hawana hati!.Usichangane mabo katika uelewa wa umiliki mashamba.
Hao uliowataja ni eidha kampuni zilizoandikishwa kisheria na zikapewa umiliki wa ardhi kwa masharti yaliyopo Ardhi, au ni watu binafsi waliomilikishwa mashamba wa muda maalum na masharti maalum na watakuw na Certificates of Occuppacy yaani Title(Hati)
Kisheria hiyo barua haitambuliki.Hakuna tofauti umiliki huo wa Zanzibar na umiliki mwingine wowote, tofauti ni moja tuu, SMZ wana barua ya kibali, hawana hati!.
P
Asilimia kubwa ya watanzania wako nyuma kwenye kujuwa mambo ya nchi
Hii issue watu ndiyo wameijua leo
Poleni sana
Ova
Umeona nkilalamikaImekusaidia nn wewe kujua miaka 27 iliyopita?
Umeona nkilalamika
Si naelewa
Ova
Hao wamekuja kama wawekezaji wa kigeni. Na pengine wengine ni raia kamili. Sasa sisi na Zanzibar tulipoungana tulikubaliana kuwa kila mtu atabaki na ardhi yake. Kuwa ardhi siyo suala la Muungano. Ukitaka kwenda kwa mwingine utaenda kuwekeza kama raia wa kigeni. Hivyo ndivyo inavyotakiwa. SMZ inawakilisha raia wote wa Zanzibar. Wakitaka ardhi Tanganyika lazima waje kama wawekezaji wa kigeni.No sio wako nyuma, bali ni watu wa ajabu sana!. Utakuta hapa wanapiga kulele kusikia Zanzibar ina eneo bara, lakini kuna ma settles walikuwa na maeneo kama yule Mzungu Steyn mwenye ushamba ya ngano kule Malbadawi Hanang, Mashamba ya chai ya Mufindi yanamilikiwa na Brookebond, Pale Kisarawe Luna eneo la hectares 27,000 ni shamba la Sun Biofuels, walalima mibono kaburi kuzalisha Biofuels. Kule Machame Luna mzungu na mkewe, Silverdales, wamedhulumiwa shamba lao, no one complains lakini Mzanzibari kuwa na eneo bara... nongwa!.
P