Wabara ondoeni shaka, ardhi ya SMZ Bagamoyo si sehemu ya Zanzibar. SMZ haina hati; limetelekezwa miaka 45 ila Zanzibar inamiliki kihalali

Wabara ondoeni shaka, ardhi ya SMZ Bagamoyo si sehemu ya Zanzibar. SMZ haina hati; limetelekezwa miaka 45 ila Zanzibar inamiliki kihalali

Umesahau miaka ya nyuma wafungwa walikuwa wanatoka zenji
Na kuja kufanya kazi kwenye ranchi hiyo
Kulikuwa na mpaka gereza lao

Ova
Hili sikuwahi kulijua ndio nalisikia leo, ila hakuna tatizo, hao wafungwa ni Watanzania hivyo wanaweza kufanyishwa kazi popote. Hata wale masheikh wa uamsho, walishikiliwa kwenye magereza ya huku bara!.
P
 
Nampongeza sana Pasacl Mayalla, ni mtu mwenye IQ kubwa sana na kuweza kuelewa anachosema inabidi uwe umepata A au B kwenye somo la Constitutionalism and Legal Systems of East Africa; Kwetu sisi akina Shivji wadogo tunamwona kama Mchochezi na atakiwa kupingwa kwa nguvu ya HOJA,
ameonyesha uchochezi wa aina 2, sio kweli kuwa Zanzibar inapewa 4.5% ya Mikopo yote, huo ni uongo mkubwa sana. Pili, kwenye doctrine ya adverse Possession doesn't apply kwenye ardhi inayomilikiwa na mtu mwingine, doctine of adverse possession ina apply kama wavamizi wanamevamia bila kupewa na mtu yeyote na bila kuwa na taarifa kuwa hili eneo ni la Mtu mwingine
 
Hili sikuwahi kulikua ndio nalisikia leo, ila hakuna tatizo, hao wafungwa ni Watanzania hivyo wanaweza kufanyishwa kazi popote. Hata wale masheikh wa uamsho, tumewashikilia kwenye magereza ya huku bara!.
P
Huko nimezunguka kote miaka hiyo
Hadi nkaonaga vibao vimeandikwa
smz ,ndomana sioni jambo geni

Ova
 
Nimeshanga sana kuona watu huku wanaona jambo geni
Kweli watz wako nyuma sana kujua mambo

Ova
No sio wako nyuma, bali ni watu wa ajabu sana!. Utakuta hapa wanapiga kulele kusikia Zanzibar ina eneo bara, lakini kuna ma settles walikuwa na maeneo kama yule Mzungu Steyn mwenye ushamba ya ngano kule Malbadawi Hanang, Mashamba ya chai ya Mufindi yanamilikiwa na Brookebond, Pale Kisarawe Luna eneo la hectares 27,000 ni shamba la Sun Biofuels, walalima mibono kaburi kuzalisha Biofuels. Kule Machame Luna mzungu na mkewe, Silverdales, wamedhulumiwa shamba lao, no one complains lakini Mzanzibari kuwa na eneo bara... nongwa!.
P
 
Wanabodi,

Kama kawaida yangu kila nipatapo fursa huja na kwa maslahi ya taifa.

Maslahi ya leo ni hii issue ya SMZ kumiliki eneo la ekari 6000 Bagamoyo. Tangazo la SMZ Zanzibar: Hekta 6,000 zilizopo Bagamoyo ni mali yetu
limeleta taharuki na sintofahamu kubwa kwenye mitandao ya kijamii hadi baadhi ya watu kutoa povu!.

Kuna watu wanatafsiri potofu kuwa sehemu ya Ardhi ya Tanzania Bara ni sehemu ya Zanzibar!.

Ukweli ni huu
Anza na bandiko hili la mwaka 2014 iujue historia ya eneo hilo lilimilikiwa vipi na Zanzibar Zanzibar ndani ya Tanganyika ilianzia huku kisha soma majadiliano ya Bunge ya miaka ya nyuma kuhusu issue hii.

View attachment 2644793

Shamba la Mifugo Linalomilikiwa na SMZ huko Bagamoyo

MHE. MOSSY SULEIMANI MUSSA
aliuliza:-

Kwa kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliwahi kuwa na shamba kubwa la mifugo (ng’ombe) ranchi huko Bagamoyo:-

(a) Je, Serikali ya SMZ bado inamiliki shamba hilo?
(b) Je, hadi kufikia kuboreshwa kwa shamba hilo SMZ ilitumia shilingi ngapi?

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na uvuvi naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mossy Suleimani Mussa Mbunge wa Mfenesini lenye vipengele (a) na (b) kwa pamoja kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Spika kwa kuzingatia Ranchi ya Zanzibar Bagamoyo (RAZABA) iliyoko Makurunge katika Wilaya ya Bagamoyo inamilikiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Ranchi hiyo ilianzishwa mwaka 1976 baada ya kupata kibali kutoka kwa Kamishna wa Ardhi chenye kumbukumbu namba LD/70254/12/TBR cha tarehe 24/09/1971, hivyo kwa taarifa hizo Wizara yangu bado inaamini shamba la RAZABA bado ni mali ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, hata hivyo kwa vile swali linaloulizwa na Mheshimiwa Mbunge linahusu mali zilizo chini ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi sio Wizara ya Muungano napenda kumjulisha Mheshimiwa kuwa Wizara yangu haiwajibiki kujua kama Serikali ya Mapinduzi Zanzibar bado inamiliki au haimiliki shamba hilo.

(b) Mheshimiwa Spika, Wizara yangu haijui kama shamba hilo ambalo liko chini ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar lilitumia shilingi ngapi katika kuliboresha, namshauri Mheshimiwa Mbunge akapate majibu ya takwimu hizo Wizara inayohusika katika Serilkai ya Mapinduzi Zanzibar.

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI:

Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Naibu Waziri naomba kutoa maelezo ya nyongeza kama ifuatavyo.

Mheshimiwa Spika, shamba hilo ambalo ni kweli kama alivyosema Naibu Waziri lilimilikishwa kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar lakini kwa miaka mingi sana karibu 30 halitumiki, kwa hivi karibuni Serikali imemega sehemu na kuwapa wawekezaji, watawekeza katika mambo ya biofuel na Sehemu bado inaendelea kuwa mali ya SMZ.

View attachment 2644761

My Take
  1. Wabara ondoeni shaka kuhusu umiliki wa SMZ eneo Bagamoyo, SMZ inalimiliki eneo hilo kihalali kabisa kwa vile walipewa na Mwalimu Nyerere.
  2. Kitendo cha SMZ kumiliki eneo huku Tanzania bara, hakulifanyi eneo hilo kuwa sehemu ya Zanzibar, ni eneo halali la SMZ ila ardhi ni ya Tanzania bara.
  3. Nchi yoyote inaweza kumiliki eneo nchi nyingine yoyote, umiliki huo haulifanyi hilo eneo kuwa sio sehemu ya nchi husika.
  4. Japo SMZ inalimiliki eneo hilo lililokuwa hekta 6,000, kwanza SMZ, haina hati ya umiliki bali ina kibali cha umiliki No. LD/70254/12/TBR cha tarehe 24/09/1971.
  5. SMZ ililitelekeza eneo hilo kwa miaka 45, hivyo serikali ikalimega kumpa mwekezaji, Halmashauri ya Bagamoyo imelipima viwanja inaviuza.
  6. Kwa vile ni eneo halali la SMZ, na sasa SMZ imeibuka kuonyesha ina interest na eneo lake, then itarudi serikalini kuelezea hiyo interest, serikali itakwenda kulipima limebakia kiasi gani, SMZ itapimiwa upya na kugawa.
  7. Iwapo SMZ bado italihitaji eneo lote la awali la ekari 6,000, then italazimika kuwalipa fidia watu wote waliomegewa kihalali.
  8. Kama pia limevamiwa na wananchi, then sheria yetu ya Ardhi ya Vijiji No. 5 ya mwaka 1999 will apply kwa mtu aliyetelekeza eneo lake kwa miaka 45, wale wavamizi wana haki fulani.
  9. Ikionekana madhara ya kuwaondoa wavamizi ni makubwa kuliko kuirejeshea SMZ eneo hilo, then kile kibali cha umiliki wa SMZ kinafutwa, wananchi wanapimiwa, na SMZ wanapewa eneo jingine, tuna mapori kibao ya kumwaga, hata wakitaka heka 10,000 wanapewa.
  10. Hii ya kuwagaiya wavamizi imefanyika sana kwenye maeneo ya jeshi na maeneo ya RTD, wavamizi wamepimiwa na kuhalalishiwa!.
Hivyo Watanzania wenzangu isiwe na wasiwasi kabisa kuhusu hili, after all eneo lote la Zanzibar ni sehemu ya JMT hakuna sababu ya watu kutoa povu, Wanzanzibari kuniliki Ardhi Bara lakini Wabara hawewezi kumiliki ardhi Zanzibar, kwasababu Wazanzibari ni Watanzania wenzetu wana haki zote za Utanzania, ila Zanzibar ni the minority, visiwa vyao ni very tiny, tukiruhusu kila Mtanzania kumiliki ardhi Zanzibar, itaelemewa na kuvizamisha visiwa vile!.

Wakati wa kuumbika nchi, Zanzibar ilikuwa eneo la bara likamegeka kwa sea erosion, hivyo Visiwa vya Zanzibar ni sehemu halali ya Tanzania bara ndio maana dhima ya muungano wetu adhimu ni udugu, sisi ni ndugu moja, Waarabu walipokuja Zanzibar ile 1732 Sultan Seyyid Said alipohamoshia Sultanet take toka Oman kuja Zanzibar, aliwakuta wenyeji halisi ni Wahadimu, kutoka Bara, alivitwaa visiwa hivyo toka ukoo wa Mwinyimkuu, na waliompindua Sultan kwenye yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ni wajukuu wa Mwinyimkuu wenye Zanzibar yao, ndio maana slogan ya Mapinduzi Daima ipo, na baada ya muungano tumekuwa kitu kimoja, ndio maana slogan ya muungano ni tutaulinda kwa gharama yoyote.

Miongoni mwa gharama hizo ni kumsamehe madeni, kumpa 4.5% ya fedha za mikopo na misaada, ajira na hata kumpa eneo lolote Wazanzibari watakalotaka.

Watanzania bara tujifunze kuwa na shukrani, tushukuru sana Zanzibar, ukanda wa eneo la maili 10 ya Pwani ya ya bahari ya hindi, lilikuwa eneo la Zanzibar, ikatugawia!, miji yote ya Pwani kuanzia Dar, Tanga, Bagamoyo imejengwa na Sultan of Zanzibar!

Hata mjengo wa Ikulu ya Magogoni, imejengwa na Sultan of Zanzibar, hata ile replica ya Ikulu pale Chamwino ni mjengo wa Kiarabu!, mbona watu mnakosa shukrani kwa mambo mazuri kama haya, mnaona nongwa Zanzibar kumiliki eneo huku Bara!

Mapinduzi Daima
Muungano Tutaulinda kwa gharama yoyote!.

Paskali.
Wewe Paskali serikali yako ina eka 6,000 katika nchi gani hapa duniani?
 
Nampongeza sana Pasacl Mayalla, ni mtu mwenye IQ kubwa sana na kuweza kuelewa anachosema inabidi uwe umepata A au B kwenye somo la Constitutionalism and Legal Systems of East Africa; Kwetu sisi akina Shivji wadogo tunamwona kama Mchochezi na atakiwa kupingwa kwa nguvu ya HOJA,
ameonyesha uchochezi wa aina 2, sio kweli kuwa Zanzibar inapewa 4.5% ya Mikopo yote, huo ni uongo mkubwa sana. Pili, kwenye doctrine ya adverse Possession doesn't apply kwenye ardhi inayomilikiwa na mtu mwingine, doctine of adverse possession ina apply kama wavamizi wanamevamia bila kupewa na mtu yeyote na bila kuwa na taarifa kuwa hili eneo ni la Mtu mwingine
Thanks my fellow leaned brother, eneo hilo ni kubwa na abandoned for 45 years mpaka juzi, kama mtu alivamia akiwa pale, ameoa, watoto wamezaliwa na sasa ni wajukuu!, mtu kama huyo unamuhamishaje?.
P
 
No sio wako nyuma, bali ni watu wa ajabu sana!. Utakuta hapa wanapiga kulele kusikia Zanzibar ina eneo bara, lakini kuna ma settles walikuwa na maeneo kama yule Mzungu Steyn mwenye ushamba ya ngano kule Malbadawi Hanang, Mashamba ya chai ya Mufindi yanamilikiwa na Brookebond, Pale Kisarawe Luna eneo la hectares 27,000 ni shamba la Sun Biofuels, walalima mibono kaburi kuzalisha Biofuels. Kule Machame Luna mzungu na mkewe, Silverdales, wamedhulumiwa shamba lao, no one complains lakini Mzanzibari kuwa na eneo bara... nongwa!.
P
Usichanganye mambo katika uelewa wa umiliki mashamba.
Hao uliowataja ni aidha kampuni zilizoandikishwa kisheria na zikapewa umiliki wa ardhi kwa masharti yaliyopo Ardhi, au ni watu binafsi waliomilikishwa mashamba wa muda maalum na masharti maalum na watakuw na Certificates of Occuppacy yaani Title(Hati)
 
Usichangane mabo katika uelewa wa umiliki mashamba.
Hao uliowataja ni eidha kampuni zilizoandikishwa kisheria na zikapewa umiliki wa ardhi kwa masharti yaliyopo Ardhi, au ni watu binafsi waliomilikishwa mashamba wa muda maalum na masharti maalum na watakuw na Certificates of Occuppacy yaani Title(Hati)
Hakuna tofauti umiliki huo wa Zanzibar na umiliki mwingine wowote, tofauti ni moja tuu, SMZ wana barua ya kibali, hawana hati!.
P
 
Hoja ya kwamba wa bara wakiruhusiwa kumiliki ardhi Zanzibar kisiwa kitazama yani ukimaanisha kitajaa sana haina mashiko

Lakini umesema Zanzibar ni sehemu ya bara iliyomumunyika na kuwa kisiwa mistari michache chini yake ukayataja maeneo ya bara ambayo yalikuwa ni sehemu ya Zanzibar ikaipatia bara

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Tatizo kubwa la Zanzibar Chao ni Chao wakati Cha kwetu ni Cha wote. Ardhi SI swala la Muungano, mtanzania bara kumiliki ardhi ni dhambi kubwa sana.
Hoja ya kwamba wao Wana eneo dogo Haina nguvu kwani hata population Yao ni ndogo na kwa Kasi tuliyonayo SI muda mrefu hii ardhi itakuwa haitoshi.
Kwa mujibu wa katiba ya Muungano Kuna mambo manane ya Muungano ikiwamo gesi na mafuta na utaratibu wa kuyaondoa ni kupata theruthi mbili za Baraza la wawakilishi na theruthi mbili za bunge la jamhuri ya Muungano ila walipohisi Wana mafuta waliliondoa kinyemela hili swala kuwa la Muungano kwa hofu rais akitoka bara hawatanufaika nitaomba siku Moja Pascal kwa sababu wewe sio tu mwandishi ila umesomea sheria uliandikie Makala. Ila rais alipokuwa Toka upande wao mkataba wa gesi ndio wa kwanza kukusanya na Kenya je sisi watanganyika kwanini tusiwe baa wasiwasi kuwa wanatapanya Mali zetu.
Kwa kifupi kama katiba ya Muungano ilivunjwa wakakaa kimya ni swala la muda huu Muungano wa kimchongo kuvunjika.
Warioba katika rasimu Yao alisema ni hero watanganyika wakapewa serikali Yao kabla hawajaidai ikifikoa hatua ya kudai uwekezaji na uporaji unaofanywa na Zanzibar kwa kisingizio Cha Muungano vyote vitataifishwa
 
Wakati Nyerere anawapa Zanzibar ardhi huko Bagamoyo miaka ya 1970s kulikuwa na sababu ya msingi. Biashara zote zilikuwa zikifanywa na serikali (mfano RTC, NMC. NAFCO, nk). Hakukuwa na wafanya biashara binafsi ambao wangepeleka ng'ombe Zanzibar. Hivyo, ilikuwa muhimu SMZ ifanye kazi ya kununua ng'ombe bara, kuwapa malisho kwenye Ranchi bara, na kisha kuwapeleka Zanzibar kwa ajili ya nyama, nk.

Mambo yalipobadilika kukawa na wafanya biashara binafsi (private enterprise), hilo jambo halikuwa muhimu tena, ndo maana Znz walitelekeza Ranchi Kwa miaka 45!

Hata kwa sasa, awamu ya sita, hakuna sababu za msingi za Smz kutaka tena hilo eneo.
 
No sio wako nyuma, bali ni watu wa ajabu sana!. Utakuta hapa wanapiga kulele kusikia Zanzibar ina eneo bara, lakini kuna ma settles walikuwa na maeneo kama yule Mzungu Steyn mwenye ushamba ya ngano kule Malbadawi Hanang, Mashamba ya chai ya Mufindi yanamilikiwa na Brookebond, Pale Kisarawe Luna eneo la hectares 27,000 ni shamba la Sun Biofuels, walalima mibono kaburi kuzalisha Biofuels. Kule Machame Luna mzungu na mkewe, Silverdales, wamedhulumiwa shamba lao, no one complains lakini Mzanzibari kuwa na eneo bara... nongwa!.
P
Hao wamekuja kama wawekezaji wa kigeni. Na pengine wengine ni raia kamili. Sasa sisi na Zanzibar tulipoungana tulikubaliana kuwa kila mtu atabaki na ardhi yake. Kuwa ardhi siyo suala la Muungano. Ukitaka kwenda kwa mwingine utaenda kuwekeza kama raia wa kigeni. Hivyo ndivyo inavyotakiwa. SMZ inawakilisha raia wote wa Zanzibar. Wakitaka ardhi Tanganyika lazima waje kama wawekezaji wa kigeni.
 
Back
Top Bottom