gspain
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 2,920
- 6,081
Ni kweli mkuu, bado hatutaki kukubali kuwa elimu ya mkoloni ililenga kutufuta ujinga na si kutupatia maarifa.Very true.
Na kinachosababisha kuwa hivyo ni kwamba Watanzania tuko nyuma kidunia kwenye mambo yote yanayohusu taaluma.
Yaani unakuta mtu akishamaliza chuo basi kamaliza anajiona ni expert tayari na anakuwa hana mpango wa kujiendeleza kwa kufuatilia kozi mbalimbali za kidunia.
Ingekuwa tunapata nafasi ya kujilinganisha na wataalamu wa nchi mbalimbali tungepata uhalisia ulivyo na tungekazana.
Mkoloni aligundua kuwa kuna uhitaji wa kutustaarabisha kwa kiwango cha kati ili tushiriki katika kutawaliwa huku tukijihisi ni watu huru. Hivyo alibuni elimu itakayompa urahisi wa kututawala huku akiwa mbali.
Cha ajabu miaka almost 60 baada ya uhuru bado tumeendelea kuamini kuwa ipo siku elimu hii itatukomboa. Kimsingi elimu tuliyo nayo haitupeleki tunapohitaji bali inatuongoza anapotaka tuelekee mkoloni.
Mataifa yote yaliyojikomboa yalikinzana na mfumo huu katika hatua zao za awali kabisa kuelekea ukombozi halisi.