Wabongo mkija majuu au ughaibuni acheni unafiki, majungu na ukora mnaliabisha Taifa lenu

Mimi naona hakuna haja ukifika nje kuanza tena kufuatana fuatana wabongo badala ya kutengeneza urafiki na wenyeji ambao ndo wanajua kila kitu kuhusu nchi yao. Kama unaenda nje na unaanza kutafuta wabongo wenzako bora ukabaki tu usiende. Mambo ya kufuatana fuatana kama nzi tuwaachie Machalii wa R maana wao hata wakiwa Dar lazima wajitenge.
 
Duuuh!
This is comedy🤣🤣
 
Acha kubebesha lawama watu wanaopambania maisha yao. Beba msalaba wako usimbebeshe mtu.
 
Unatoka bongo, unaenda nje kutafuta marafiki wa kibongo si uhanithi huo?
Kama usemavyo, ni afadhali kubaki nchini tu.
 
Inategemea na mtazamo wa mtu, gari kwangu naweza chukulia chombo cha usafiri mwingine ikawa ni kwa ajili aringishie wengine ana gari, nachosema mtazamo wa mtu, hasa wabongo mtazamo wao si kujifunza bali kujionesha.
 
Word. Kimsingi muanzisha Uzi anatetea uhalifu.

Nchi yeyote ile hasa nje huwezi shikwa kama hakuna grounds za kukushika.
Mkuu Bufa namtetea mtoa uzi.
Unaweza ukawa unajiona sio mhalifu na unafanya kazi halali na kodi unalipa lakini wewe ni 'mhalifu' na ukachomwa na grounds za kukushika zikawepo.

Kwa mfano katika kutafuta maisha watu wanajipa ukimbizi,watu "wanaoana" na ndugu zao,watu wanadanganya watoto wa ndugu ni wao wa kuwazaa n.k.

Sasa chukulia mfano ulipata permit kwa kusema wewe mkimbizi toka somalia/burundi then baada ya miaka kadhaa ukasoma ukapata kaz yako nzuri ya halali kabisa raia safi then unafikiri mtu anayejua siri ya ulivyopata permit akitaka kukuchoma hawezi?
 
Huyu mtu wako "Izzo" ni tapeli tu tulikuwa naye kwenye ile thread maalufu JF ya kujilipua kwenda mamtoni back in 2017. Akaleta mawenge. Kiufupi kama unataka kwenda mbele unapaswa upambane kivyako achaheni kulialia.

Kaveli

Mkuu, hizi mambo za ''koneksheni ughaibuni" ni uduwanzi mtupu.

Hao watoa michongo ni makanjanja tu... njaa plus!

Uhakika ni mtu apambane mwenyewe tu.

-Kaveli-
 
Upumbavu mwingi wa diaspora upo clubhouse. Majivuno dharau na kejel kibao kumbe ni homeless kwenye mataifa ya watu.
 
Huyu jamaa Kiranga kuna uzi niliwahi kusoma alikuwa na michango chanya mingi. Mtake radhi japo haamini ka Mungu atakusamehe.
 
Yaani.
Unakuta mtu anaishi Norway au Denmark zaidi ya 10 yrs ila hajui kidenish wala kiingereza cha kueleweka ila misemo yote mipya inayozuka bongo anaijua.
Kila kinachotrend bongo anakijua ila hana chochote anachojua cha nchi aliyoko sbb kutwa kugandana wao kwa wao.Mtu hata rafik wa kizungu hana
 
Nilikuwa nafikiri hivyo, nikadadisi, mtu ukiwa straight kila kitu watakuchomaje?

Nikaambiwa watu wanaweza hata kukupandikizia madawa ya kulevya na kukuchoma ionekane unafanya hiyo biashara.

Kwa hiyo nisijione clean sana, not to that extent!

Wanaweza kukupandikizia ila kiuhalisia it's far fetched. Hadi mtu akufanyie hivyo lazima kuna some shady dealings unajihusisha nazo, kama upo clean haya mambo utayasikia tu.

Mimi napinga vikali hii notion kwamba wabongo waliopo nje hawapatani, wanaendekeza majungu na umbea. Kama hutaki majungu na umbea huwezi letewa hizo habari.

Last wk community yetu ya wabongo huku nilipo tumemchangia mbongo mwenzetu aliyepatwa na matatizo. Huyu jamaa alikua against hii community na alikua anapinga wazi wazi kabisa ila watu wamejitokeza na kachangiwa, hii ni hela nje ya mfuko wa community.

Community yetu tuna ushirikiano mzuri sana, tuna-hang out pamoja tukipata nafasi, tunasaidiana na kupeana michongo. Hamna umbea, majungu whatsoever.
 
Ni hivi, dunia ina takers and givers.

Givers are mostly silent, yani wewe umekuja kutoa story hii kwa sababu hoja imechokonolewa, hujaanzisha thread kusifia jumuiya yenu, umeona kawaida tu, wajibu wenu.

Ila takers sasa, wao wako so entitled na so vocal. Hawa ndio wanaanzisha thread za kulalamika sana.

Yani kukiwa na mambo 10, 9 ya givers na 1 la takers, utasikia malalamiko ya lile moja la takers kabla hujasikia lolote kati ya yale 9 ya givers.
 

I couldn't agree more.
 
Mimi huwa nikitoka nje ya Bongo huwa kiswahili ni kabla sijaingia kwenye ndege. Nikiwa ndani ya ndege sitaki mazoea kabisa.
 
Mkuu Kiranga, nimeku pm, naomba nipate uzoefu kidogo kutoka kwako, naamini uzoefu huu utanitoa sehemu moja kwenda nyingine.
Mkuu umesha acha utoto wa kuandika nyuzi zisizo na kichwa wala miguu?[emoji1]
 

EBM anatoa elimu bure kabisa lakini kule hutoona watu wanafuatilia sijui kwa nini?
 

Mkuu, mara ngapi umesikia hizo kesi za kuchomana hivyo? Wangapi wamevuliwa karatasi au kuwa deported sababu walidanganya jinsi walivyopata karatasi zao?

Unajua kumtishia mtu kwamba utamripoti immigration inaweza chukuliwa kama abuse na sheria zipo zinazowalinda?

Kesi za namna hiyo huwa zinaenda court na judge wana power ya ku-override matakwa ya immigration law na kumuacha mtu aendelee kuishi nchini kwa kigezo cha "good moral character." Hii inatokea pale mtuhumiwa anapokuwa ni mtu mwema kwenye jamii yake, mfanyakazi na mlipa kodi. Jaji hata siku moja hawezi fukuza mtu wa namna hiyo.

Mathalani watu wengi wanoomba ukimbizi huwa wanapata makaratasi kwa kigezo hicho japokuwa huwa inachukua muda mrefu. Wakipelekwa mahakamani jaji akiona hawa ni watu wema kwenye jamii na wanamchango kwenye jamii hakuna sababu ya kuwafukuza japo uhamiaji huwa wanataka waondoke nchini kwa kigezo madai yao ya ukimbizi hayana tija ila majaji huwa wanawapa makaratasi right away. Nawajua watu zaidi ya 20 wenye makaratasi kwa njia hiyo toka TZ na nchi zingine.

Ukiona mtu kachomwa aidha kwa sababu hii au nyingine yeyote ile ujue kuna sababu nyingine strong enough mtu huyo kutiwa nguvuni mara nyingi ni criminal offense kama domestic violence, wizi, DUI nk. Hizi offense zinavunja kinga ya good moral character.
 
Hasa kujaza msosi na bia kwenye friji hata mtu asiyekuwa na kazi anaweza.Hao wanaolingishia msosi wakiua wataacha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…