Mkuu, kwa haya maoni yako, kama kweli hujawahi kufika Ulaya au Marekani na bado ukawa na maoni haya, basi wewe ni mtu uliyejibiidisha sana kupata maarifa ya maisha. Mie nimeishi Ulaya katika nchi mbili tofauti na ndio nimejionea ukweli wa maisha ulivyo. Sio tu Ulaya, nimeishi ktk nchi ambazo ni very civilized and well developed. Maana hata Ulaya kuna baadhi ya nchi mambo yake kama Afrika tu. Na sio kwamba nimeishi kwa kujifungia, nimejichanganya kwingi tena haswa. Ila kama wewe hujawahi kuishi na bado ukatoa haya maoni basi itoshe kusema wewe ni tajiri wa maarifa. Naomba nisiongeze jambo zaidi maana ninaweza haribu mwishowe.