Wabongo mkija majuu au ughaibuni acheni unafiki, majungu na ukora mnaliabisha Taifa lenu

Wabongo mkija majuu au ughaibuni acheni unafiki, majungu na ukora mnaliabisha Taifa lenu

Mkuu umeongea kitu kizuri sana.Laiti kila mtu angesema huu ukweli watu wangefunguka macho wakatafuta maisha hapa hapa bongo.
Mim namuheshimu sana mtu asiyeshobokea ughaibuni.Raha ya ulaya ni uende kutembea na urudi bongo.
Watu hawajui tu unaweza ukatumia 30M kufika ulaya ila ukafika huko halafu ukakaa miaka hata 10 bila kuwa na uwezo wa kurudisha hiyo hela wala kuwa na sehemu yako ya kuishi.Unazeeka huna nyuma wala mbele na kurudi bongo unatamani ila huwezi.
Mkuu, kwa haya maoni yako, kama kweli hujawahi kufika Ulaya au Marekani na bado ukawa na maoni haya, basi wewe ni mtu uliyejibiidisha sana kupata maarifa ya maisha. Mie nimeishi Ulaya katika nchi mbili tofauti na ndio nimejionea ukweli wa maisha ulivyo. Sio tu Ulaya, nimeishi ktk nchi ambazo ni very civilized and well developed. Maana hata Ulaya kuna baadhi ya nchi mambo yake kama Afrika tu. Na sio kwamba nimeishi kwa kujifungia, nimejichanganya kwingi tena haswa. Ila kama wewe hujawahi kuishi na bado ukatoa haya maoni basi itoshe kusema wewe ni tajiri wa maarifa. Naomba nisiongeze jambo zaidi maana ninaweza haribu mwishowe.
 
Watu gani hao unaokaa nao hadi mnaringishiana misosi kwenye fridge? Hii tabia hata bongo haipo. This says more about you kuliko hao watu.
Mimi kuna mtu alinitumia picha ya friji na vyakula akaniambia nimuoneshe friji langu lilivyo.

Sikumjibu.

Kwanza nilishangaa, halafu nikataka kumuuliza friji gani, la juu ama la chini? Maana mimi nina mafriji, yote full size yana mpaka freezers na yamejaa, sina friji moja [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Man, ndo nasikia leo hii 🤣
 
Wakati wenzetu wanapanga kabisa mambo yao. Yani hata kama kuna bahati, unajitengenezea mazingira mazuri bahati ikuangukie wewe kwa kuwa na vigezo vyote.
Mkuu naomba sentensi hizi za mwisho wa andiko lako liwe 'take home message' kwangu kutoka JF siku ya leo. Umezungumza kitu kikubwa sana. Ndio maana nilisema ukiwa na maarifa mengi utaifahamu vizuri dunia, na unaweza kufahamu ufanyeje kupata unachotaka. Naomba nisiendelee kutia neno nikaharibu uzuri wa ujumbe wako. Hakika wewe ni mtu mwenye maarifa.

Tutatofautiana kidogo kuhusiana na mambo ya imani, hasa kuhusu Mungu ila naamini una maarifa mengi mazuri kunizidi mimi. Sitochoka kuwa mwanafunzi wako hapa Jukwaani. Hata kwenye masuala ya imani bado naendelea kujifunza zaidi. Na kila siku nafanya maboresho ya kile nachoamini. Leo nilivyo sivyo nilivyokuwa miaka minne iliyopita.

Kwanza nimefarijika sana kwako wewe kuendelea ku-interact na mie hapa jukwaani siku ya leo. Kwa namna ninavyokufahamu hapa jukwaani, siwezi kufikia hata robo ya maarifa uliyonayo. Nikutakie siku njema Mkuu.
 
It was a thing trending on social media.

Na wabongo si unatujua kwa kurukia trends tena?

Nikasema ukiona kichwa cha mtu kama friji la Idi Amin utafanya nini?

Oh really, I must be living under a rock.

Ukisema una freezer mbili watasema unajimwambafy waanze tena kuponda watu wa nje. Ushamba mzigo wa mwiba.
 
Naweza sema ni mindset ya kimasikini kudorishia wenzako vilivyomo kwenye fridge, mambo madogo sana.
Huoni kwamba tunatakiwa ku normalize tu mambo haya?

Trend haikuanzishwa na Watanzania, watu wanaoneshana jinsi ya kupanga vitu kwenye friji, vyakula tofauti wanavyokula, watu wanajifunza mambo tofauti kuhusu vyakula na mafriji.

Hapo kuna ubaya pia? Au tunaweka inferiority complex tu?

Kama friji ni kitu cha kawaida tu kwa nini tufanye big deal?
 
Oh really, I must be living under a rock.

Ukisema una freezer mbili watasema unajimwambafy waanze tena kuponda watu wa nje. Ushamba mzigo wa mwiba.
Marekani ni kawaida tu kuwa na extra fridge/freezer kwenye garage/ basement kwa sababu ya jikoni mara nyingi inakuwa inajaa.
 
Juzi kuna watu wabongo wajinga wamemchoma mwenzao mpaka ameenda kwa sello kisa jamaa mambo yake yanaenda na anapiga hela nyingi, kwahiyo wajamaa wameamua kumchoma, upuuzi! Nyie wabongo tabia yenu ya kipuuzi huko kwenu muiachane huko huko.
Unaposema "wamemchoma" unamaanisha wameripoti uharamia(ufisadi/ubadhirifu/wizi) aliokuwa anaufanya huyo mtanzania mwenzako huko nje.

Kwahiyo huyo jamaa yako ndiye hafai kabisa, ni mshenzi. Hao walioripoti ndiyo wamestaarabika na wanayaishi maisha ya binadamu kamili wa huko nje.

Tanzania haitoboi kwasbb ya fikra za kijinga kwamba ukipata kazi lazima uibe. Nyambafu!!!!
 
Unaposema "wamemvhoma" unamaanisha wameripoti uharamia(ufisadi/ubadhirifu/wizi) aliokuwa anaufanya huyo mtanzania mwenzako huko nje.

Kwahiyo huyo jamaa yako ndiye hafai kabisa, ni mshenzi. Hao walioripoti ndiyo wamestaarabika na wanayaishi maisha ya binadamu kamili wa huko nje.

Tanzania haitiboi kwasbb ya fikra za kijinga kwamba ukipata kazi lazima uibe. Nyambafu!!!!

Word. Kimsingi muanzisha Uzi anatetea uhalifu.

Nchi yeyote ile hasa nje huwezi shikwa kama hakuna grounds za kukushika.
 
Najua ila wabongo hawawezi elewa Hilo watasema unajipamba. Wanadandia trends wasizoziweza.
Mimi uzuri wangu nikiwa katika zone sijali kama wanaelewa au la, na pengine wasipoelewa najipa kazi ya kuwaelewesha.

Kuna mambo watu walikuwa hawaelewi lakini siku zinavyokwenda wanakuja wenyewe kunishukuru kwa kusema "tulikuwa tunakuona mbishi tu, au mjivuni tu, lakini siku zinavyoenda tunazidi kukuelewa".
 
Word. Kimsingi muanzisha Uzi anatetea uhalifu.

Nchi yeyote ile hasa nje huwezi shikwa kama hakuna grounds za kukushika.
Nilikuwa nafikiri hivyo, nikadadisi, mtu ukiwa straight kila kitu watakuchomaje?

Nikaambiwa watu wanaweza hata kukupandikizia madawa ya kulevya na kukuchoma ionekane unafanya hiyo biashara.

Kwa hiyo nisijione clean sana, not to that extent!
 
Ila wabongo wanachomana sana. Wanawapigia hadi polisi na migration kukuchongea eti urudishwe.

Halafu kuna katabia na hulka flani ka umaskini wabongo wanayo hadi mton. Msosi mtoni siyo big deal lakini eti wanashindana kujaza friji msosi na kuringishiana unabaki kushangaa tu Wtf!
Hizo tabia ni hawa waliotoka kkoo huko na ilala, migo migo.
Utapigaje picha vyakula kwenye friji uwaambie watu niko full.
Au picha eti umenunua raba mpya,
Kuna wengine wakinunua nguo mpya wanarudi nazo kwao huko kuringishia.
Wakati hayo ni mahitaji ya lazima🤦‍♂️
 
Mkuu, kwa haya maoni yako, kama kweli hujawahi kufika Ulaya au Marekani na bado ukawa na maoni haya, basi wewe ni mtu uliyejibiidisha sana kupata maarifa ya maisha. Mie nimeishi Ulaya katika nchi mbili tofauti na ndio nimejionea ukweli wa maisha ulivyo. Sio tu Ulaya, nimeishi ktk nchi ambazo ni very civilized and well developed. Maana hata Ulaya kuna baadhi ya nchi mambo yake kama Afrika tu. Na sio kwamba nimeishi kwa kujifungia, nimejichanganya kwingi tena haswa. Ila kama wewe hujawahi kuishi na bado ukatoa haya maoni basi itoshe kusema wewe ni tajiri wa maarifa. Naomba nisiongeze jambo zaidi maana ninaweza haribu mwishowe.
Nimewahi kuishi kidogo ulaya mkuu.
Ila bahati mbaya sikupapenda.
Binafsi kuna baadhi ya watu niliona kama kwenda ulaya kumewaharibia maisha yao na sikutaka kuwa mmoja wao na bila kupoteza muda nikaanza kujiandaa kurudi zangu bongo.
Sijutii kurudi bongo na ulaya ninarudigi kutembea.Huwa namiss scandnavian summer.
 
Nilikuwa nafikiri hivyo, nikadadisi, mtu ukiwa straight kila kitu watakuchomaje?

Nikaambiwa watu wanaweza hata kukupandikizia madawa ya kulevya na kukuchoma ionekane unafanya hiyo biashara.

Kwa hiyo nisijione clean sana, not to that extent!
Mkuu sasa unaonana na watu wa namna hiyo wanini?
Unaweza kukutana nao in 5 years mara moja, watakusakizia vipi?
Tena mtaani huko hata polisi wakija wanajua huyu jamaa hawezi kufanya hivyo kesi inarudi kwao wametoa wp huo unga kukupakazia.
Simpre
 
Back
Top Bottom