Wabongo mkija majuu au ughaibuni acheni unafiki, majungu na ukora mnaliabisha Taifa lenu

Wabongo mkija majuu au ughaibuni acheni unafiki, majungu na ukora mnaliabisha Taifa lenu

Mimi naona hakuna haja ukifika nje kuanza tena kufuatana fuatana wabongo badala ya kutengeneza urafiki na wenyeji ambao ndo wanajua kila kitu kuhusu nchi yao. Kama unaenda nje na unaanza kutafuta wabongo wenzako bora ukabaki tu usiende. Mambo ya kufuatana fuatana kama nzi tuwaachie Machalii wa R maana wao hata wakiwa Dar lazima wajitenge.
Nawaambia kila siku integration.
Huwezi kwenda Ulaya we kila siku ni kukutana na wenzio toka Africa acha TZ.
Intergration unajichanganya nao na hawanaga tatizo.
Wabongo sasa.
Mkikutana mara moja tosha.
Unavunja mwezi muonane tena.
Hudaiwi.
 
"Those who would give up essential Liberty, to purchase a little temporary Safety, deserve neither Liberty nor Safety."

- Benjamin Franklin.

Tatizo liko hapa bhangosha, hicho kiinglish unitafisire sasa mi nshapata makengeza....😅😅😅😆.

By the way, Happy June, Happy Summer, Happy half year 2023 😉.
 
Kuna dogo flani nimeshawahi kuletaga uzi humu kitambo kidogo nadhani 2015 au 2016.

Dogo aliletwa mtoni akiwa mdogo kutoka bongo. Anapendaga kushindana na mimi hadi leo. Nampango wa kumuanzishia uzi humu jinsi nilivyomuwin kisaikolojia.

2009 nilipokuwa bado mgeni hapa dogo aliniudhi kichiz. Aliniambia sasa wote mkija huku nani atabaki bongo? Nilimaindi kichiz

Hadi akinunua kitanda ananiringia nabaki kushangaa kitanda tu mtoni jamani.

Kaeni mkao wa kula ntaleta uzi mwengine kumhusu karibuninilivyomuwin kisaikolojia nakumnyamazisha
Mko Nchi gani?
 
Yaani wabongo ni watu wa ajabu sana, yaani wao wamekalia majungu, chuki, unafiki na ukora tu. Yaani wao wakiona mwenzao amewazidi kwa chochote kile wanaanza kukupiga majungu, nasema hii tabia inakera.

Ndio maana mie huwa napenda kujitenga na wabongo, aisee yaani ni watu ambao wamekalia majungu, unafiki, uzandiki pamoja na ukora tu.

Juzi kuna watu wabongo wajinga wamemchoma mwenzao mpaka ameenda kwa sello kisa jamaa mambo yake yanaenda na anapiga hela nyingi, kwahiyo wajamaa wameamua kumchoma, upuuzi! Nyie wabongo tabia yenu ya kipuuzi huko kwenu muiachane huko huko.
Wabongo sisi ni wanafiki sana
 
Nahisi baridi sana...hapo nje hahahaaa! Manne ain’t try make jokes around y’all I didn’t worry about anything dryied me out... there’s no excuse and we just like light ahead so we make poppin and glory along as all time, but when comes shit 🤣🤣 it’s just click clack paaah...for real! Death is my wife! Hahahaa! Don’t believe so try me then🤣🤣
 
Marekani ni kawaida tu kuwa na extra fridge/freezer kwenye garage/ basement kwa sababu ya jikoni mara nyingi inakuwa inajaa.
My fridge in my ‘struggle’ garage 😀🙈

IMG_4417.jpeg
 
Ujuaji ni kitu kibaya sana na kinatugharimu sana watanzania
 
Nimewahi kuishi kidogo ulaya mkuu.
Ila bahati mbaya sikupapenda.
Binafsi kuna baadhi ya watu niliona kama kwenda ulaya kumewaharibia maisha yao na sikutaka kuwa mmoja wao na bila kupoteza muda nikaanza kujiandaa kurudi zangu bongo.
Sijutii kurudi bongo na ulaya ninarudigi kutembea.Huwa namiss scandnavian summer.
Hapa tatizo lako umegeneralise kwamba vitu vyako unavyotaka huko ulaya na wenzako ndio hivyo hivyo. Hakuna mtu alieharibikiwa kwenda ulaya kama alitimiza malengo yake. Wengine tuliondoka bongo hatuna shida yoyote, kama shule tulienda, pesa nono tulikua nazo ila malengo ni kwenda ulaya kuishi na wala sio kua kuna siku tutarudi bongo. Tuliondoka mazima, hata huo uraia pacha hatuuhitaji , we're living our dreams. Kuna wanaoenda kutafuta maisha ili warudi bongo wakiwa na pesa, na kuna tunaoenda kuishi, maana maisha hata hapo bongo tuliishi kama tupo ulaya tu kila siku ni Xmas. Acha kabisa kuweka watu wote kwenye kapu moja.
 
Sasa unauliza swali halafu hutaki jibu.

Wewe ushajiwekea negative thinking kwa hiyo husaidiki.

Badala ya kutaka kujua hao wawili ilikuwaje, nimewezaje kuwasaidia, unaniita muongo.

Hata kama nilikuwa na nia ya kukusaidia, unaondoa nia hiyo.

Wewe mwenyewe una negative mentality, ndiyo maana nikasema hubebeki.

Yani wewe mwenyewe huna mentality ya kuweza, hivyo ni vigumu mtu mwingine kukusaidia.
Sema nini una hoja yenye mashiko[emoji848]
 
Aliyekwambia nina negativity nani?

Mimi nataka nifike Marekani na nataka wewe Kiranga unisaidie.


Ishu ni kufika huko tu mambo mengine utaniachia mimi.

Haya twende kazi
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji13][emoji13]
 
South Africa ndio ughaibuni?
Naona wengi humu ni Mabaharia' waliopo Dizonga
 
Back
Top Bottom