Herbalist Dr MziziMkavu
Platinum Member
- Feb 3, 2009
- 43,112
- 34,951
Tunabeba Mabox, Tunasafisha Magari (Car Wash) tunajenga nyumba, tunasafisha Mabarabara, na kazi nyingi tu ngumu karibu unakaribishwa njoo uje ujionee huku majuu kulivyo kugumu ile mbaya lakini pesa zipo mishahara huku ni Euro ,Paund ya Malkia, na dollar ya Obama unakaribishwa karibu........Nina marafiki wengi wapo ulaya na marekani kazi yao ni kunitumia picha walizo piga kwenye majengo mbalimbali, lakini hawaniambii wanafanya kazi gani.Ninavyo wajua kwa kupenda sifa wangekuwa na kazi nzuri wangeniambia haraka .Kama kuna mtu mkweli aseme yeye anafanya nini? huko.
Usiwafanyie mambo ya Viza watakuja kuongezeka bure ulaya ya sasa ni ngumu hakuna kazi kila ulaya kumejaa Wa Romani,Wa Polland,Wa Bulgaria wa Chek wote hao ni Cheap Labor wanafanya kazi kwa bei ya chini mshahara kazi huku hakuna kabisa bibie.Boss nna dili la visa. . . UNATAKA?
Nabeba box kwa saa moja nalipwa 45000 za kitanzania. Na kila siku na nafanya masaa saba na nusu. Na kwa weekend inakuwa 75000 kwa saa. Na siku za sikukuu ni 90000 kwa saa. Nalipwa zaidi ya wabunge wako!!!
Tunapiga box ila linalipa,halafu mambo ya kulogana na maralia hamna huku.bila kusahau vibaka wa ovyoovyo
Wengine ni deiwaka tu; yoyote tu tunapiga karibu sana hapa Naperville, Illinois ndani ya Chicago
Vinyozi je hakuna? Wadada je,au ndo wanaokimbilia uuguzi.Sema hiyo kodi sasa ukianzisha biashara..