Wabongo mlioko majuu hivi huko mnafanya kazi gani?

Wabongo mlioko majuu hivi huko mnafanya kazi gani?

Heshima isivunjike ya JK, anamchekelea sweetheart wako akinywa chai juu ya bati la nyumba uliyompangishia jangwani! Afu anamuuliza unaendeleaje, wakati anaona nyumba inaelea. Heshima ya NN haishuki bana, unless alete zile bhange zake za kidhungu manake nae si haba,lol

Onyesha heshima kwa raisi wewe. Chezeya raisi wewe?
 
Kuna kibosile mmoja kanijia na mchongo anatafuta mtu kuziba nafasi fulani, napata tabu kupata mtu mwenye uzoefu unaotakiwa na work ethic inayohusika. Siyo unapeleka mtu kazi hajui anachemsha unaonekana wewe uliyemleta nawe ovyo.

Itabidi nimwambie tu atafute kwenye channel nyingine.

Aisee ndo maana mimi huwa sitoi recommendation hovyo hovyo manake mwisho wa siku ukimrecommed mtu halafu aharibu ina reflect na kwako pia.

Hiyo ya kuzingatia work ethic ni muhimu saana. Na kwa wale watu wanaobeza maboksi, wengine work ethic zetu ndo tumezitoa huko kwenye maboksi. Tumejifunza kuheshimu kazi ya aina yoyote ile ili mradi ni halali na isiyo na dhulumati.

Watu tumepiga work study za maintenance kama hatuna akili nzuri.
 
supaermarket, kuweka stamp kwenye barua, restaurant/bar/club, kulea wazee kwenye vituo, nesi, udereva wa trucks/ taksi, kufundisha na kutafsiri nyaraka kuwa kiswahili, kutengeneza bustani, biashara, pia wapo wanaofanya kwenye makampuni makubwa nafasi mbali mbali zikiwemo za operation, telephone operator, warehouses/store, delivery n.k angalizo mtazamo wa kazi ni tofauti sana ulaya na hapa kazi ni kazi na zinaingiza kipato zaidi ya naafasi za menejimenti tz.
 
Tofauti ni ndogo tu jamani!!

Bongo kua na maisha mazuri asilimia kubwa sio halali wakati ulaya ukifanya kazi kwa bidii maisha ni mazuri na asalimia kubwa ni halali!

Usitake linganisha mazingira ya kama USA na TZ utakosea sana, kitu ambacho chasemwa hapo juu ni kazi na kipato cha mtu wa nje na ndani(TZ)
 
Jamaa yangu mmoja kanipigia anasema yeye kawa mashine ya kufanyishwa ngono na vibibi vizungu vizee
 
haijalishi unaishi ughaibuni au bongo, haijalishi ni kazi gani unafanya as long as sio muuaji(physically or emotionally),what matters is your attitude towards life,showing off also doesn't help because at the end of the day you are the only person who knows who you are and your true worth! Merry Christmas JF members!
 
mkuu nataka ujue watanzania hatukubahatika kuwa na skill'sasa hilo tatizo limesababissha wengi tuwe na maisha ya kubahatisha kwa sababu hatuna ujuzi maalum'sasa ukiwa nje ya nchi hii inabidi ufanye kazi yoyote ile ili uweze kuishi'sasa kama unataka kujua anzia hapo kufikiri
Sema hukubahatika siyo hatukubahatika!
 
mie nafanyakazi kwenye shamba moja na kwenye supermarket lakini pia nasoma. I can afford to pay my bils lakini siyo siri huwa najina tu kama mtumwa in slave plantation. Askwambie mtu, east or west home is best! Tz imekuwa betraye na watu wake(viongozi?) yenyewe
 
me nauza juisi za azamu aka vijoti huku germany,pesa ninayo haswwaa!!
 
....Kuna watu wana kazi za maana sana na wanavuta mkwanja mzuri sana lakini kwa sababu hawaoni umuhimu wa kujipigia debe kila uchao basi watu wanadhani Wabongo wote walio juu wanabeba box. Na asilimia kubwa ya hawa wamezaliwa, kukulia na pia kusomea Tanganyika. Na wanaiwakilisha nchi yetu vizuri sana na hivyo kuipa sifa nzuri nchi yetu.
 
....Kuna watu wana kazi za maana sana na wanavuta mkwanja mzuri sana lakini kwa sababu hawaoni umuhimu wa kujipigia debe kila uchao basi watu wanadhani Wabongo wote walio juu wanabeba box. Na asilimia kubwa ya hawa wamezaliwa, kukulia na pia kusomea Tanganyika. Na wanaiwakilisha nchi yetu vizuri sana na hivyo kuipa sifa nzuri nchi yetu.

krismas njema.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Basi kama unaweza uza baa Ulaya uje basi likizo uuze hapa Meeda...sijui kama huduma mnayotoa kwenye hayo mabaa huko ni kama huku kwetu maaana walevi wengine hapa bongo nooomaaaa...lazima wakupapase kidogo...sijui baa zahuko
 
mmmmh kuuza baa basi njooni huku bongo Meeda wanahitaji wahudumu walio na uzoefu wa kimataifa
 
Nabeba box kwa saa moja nalipwa 45000 za kitanzania. Na kila siku na nafanya masaa saba na nusu. Na kwa weekend inakuwa 75000 kwa saa. Na siku za sikukuu ni 90000 kwa saa. Nalipwa zaidi ya wabunge wako!!!

Wacha uzushi huwezi kuishi zaidi ya mbunge...

Maisha ya Nje haswa U.K na U.S.A. mtu unaweza kumiliki Gari ukapata pahari pazuri pa kuishi tena kwa kuchanga ili uweze kulipa bill zote .. Zaidi uki make vya kutosha ukakusanya kama Dollar elfu 10 uzitume fasta either kwa Dingi yako au Mother ako mshughulishe akitafutie kiwanja ununue tena usimpe yeye akipata muuzaji umlipe direct bila hivyo umeliwa na kuanzisha ugomvi na chuki..

wengi wakizipata huishiwa fasta kwa starehe wanakuwa wanachelewa makazini mwishowe wanafukuzwa kazi wanaanza kuishi kwenye train yaani ni matatizo balaa lakini kerejea home ni kama hadithi no..

Mbongo akizishika pesa utamuona atakuambia nataka kwenda Bongo kusalimia na akienda wiki mbili anatembelea taxi wiki ya tatu kwenye basi ya nne anaanza kukopa nauri ya Ndege arejee Nje...
 
Nina marafiki wengi wapo ulaya na marekani kazi yao ni kunitumia picha walizo piga kwenye majengo mbalimbali, lakini hawaniambii wanafanya kazi gani.Ninavyo wajua kwa kupenda sifa wangekuwa na kazi nzuri wangeniambia haraka .Kama kuna mtu mkweli aseme yeye anafanya nini? huko.

Kwani wewe unafanya kazi gani?Halafu sidhani kama wewe pia huwa unawatumia hao rafiki zako picha zako ukiwa ofisini najua lazima itakuwa unapiga upo mlimani city au posta kama siyo kwenye mahoteli nk!!
 
Watu nwanapiga kazi na Asikuambie Mtu Ukiwin Kuingia Israel utatumikishwa Sana na Utalipwa Sana Kuliko Japan USA Starehe tu Mambo Shekel
 
Back
Top Bottom