Alex khalifa
JF-Expert Member
- Oct 22, 2025
- 278
- 516
Katika harakati za uchaguzi nilikua mwana CCM damudamu, nikimuombea kura rais wetu Samia. Nilileta Uzi, rejea Uzi wa tumuache Samia amalize muda wake, ukiisha ataondoka.
Lengo lilikua kumpigania ili aendelee na awamu nyingine. Sikufahamu kesho yangu na yetu. Nilipiga kura na kuondoka zangu.
Tarehe 30 ilinikuta nje. Ghafla nikapata taarifa kwamba hali si shwari bongo. Nilichukulia poa sana lakini mara ghafla nikajuzwa hali ni mbaya sana. Internet ilipozimwa bongo ndo nikaamini hali si nzuri.
Jana katika pitapita zangu mtandaoni nikakutana na tukio la kusikitisha. Mama mmoja mwenye sweta la purple anakimbia, mara akapigwa risasi akaanguka.
Mwanae sijui ni nani, alikuwa amevaa barakoa. Akainama chini akamgeuza na kuona damu. Nilihuzunika sana. Hivi ni kweli hawa polisi walio nilea Dodoma, nyumba ya hospitali ya rufaa, ndo wamekua wakatili hivi.
Wale polisi niliowahi kutazama nao mpira Simba na Yanga, tunashangilia pamoja, ndo hawa. Ndo hawa walionistili hapo Dodoma nilipokua nasoma DCA College. Kweli ndo wanafanya haya. Siamini bado.
Nilipoangalia hiyo clip nilitaka kulia barabarani. Hivi zile kampeni tulizopiga ndo malipo yake haya. Kumpiga risasi huyo mama ambaye hata jiwe hawezi kurusha vizuri.
Mama huyo ni kopi lait wa mama yangu mzazi alienisomesha kwa shida akichoma vitumbua. Sijui hiyo kesi ingekua inaishaje. Huenda nyumba yake na nyumba yangu zingekua mara kwanza najifunza ujambazi wa kutumia silaha. Sijui kisasi kingempata nani. Inaumiza kweli. Watz tumefikia hapo.
Naona clip eti hadi traffic nao walilia na mabunduki wakipiga watu risasi. Hawa traffic tunaocheka nao barabarani, kweli mnaua ndugu zetu simple like that. Nisameheni sitorudia tena ndugu zangu. Niko chini ya miguu yenu.
Yani unalundika watu kama unarundika kuni. Kweli hii ndo Tanzania tuitakayo. Nimeumia sana. Ogopa sana chozi la mtoto wa kiume lisilo na kelele. Mungu hatuna silaha kama wao, hatuna bunduki kama wao. Ila wewe ni wa wote.