Wabongo nimewakosea sana. Naomba radhi kwa kupiga magoti mbele yenu

Wabongo nimewakosea sana. Naomba radhi kwa kupiga magoti mbele yenu

Status
Not open for further replies.
Aseee nmejiuliza unapiga risasi watu kibarazani makwao dah, hivi lengo lilikua ni nini
Kuna namna naona kwa angle tofaut...kuna maaskari waliamua kuua makusudi ili hasira za wananchi ziwe juu na kuweza kuja front na kuiangusha serikali...lkn pia kuna wale walikuwa wanaua kwa aitha malipo au ni makada wa chama kindaki ndaki
 
Hapa umerudia tusi baada ya kuona hapo juu halijaonekana dadeqqq!! 🤣
Nisameheni ndugu zangu Kuna watu hawajui maumivu tunayopitia huyo ingekua live namjua nilikua nawasha gari nampitia namrudia kumalizia KABISA hao ndo wanao Fanya tunapoteza mama zetu, kaka zetu na wadogo zetu kisa vimishahara
 
Katika harakati za uchaguzi NILIKUA mwana ccm damudamu, nikimuombea kura rais wetu Samia nilileta Uzi, rejea Uzi wa, tumuache Samia amalize muda wake ukiisha ataondoka, lengo lilikua kumpigania ili aendelee na awamu nyingine, sikufahamu kesho yangu na yetu, nilipiga kura na kuondoka zangu, tarehe 30 ilinikuta nje, ghafla nilipata taarifa kwambia Hali si shwari bongo nilichukulia poa sana lakin mara ghafla nikajuzwa Hali ni mbaya sana internet ilipozimwa bongo ndo nikaamini Hali si nzuri,na kuendelea, Jana katika pitapita zangu, mtandaoni nikakutana natukio la kusikitisha, mama mmoja mwenye sweta la purple anakimbia mara akapigwa risasi akaanguka mwanae sijui ni nani ALIKUA amevaa barakoa, akainama chini huyo dada akamgeuza kuona damu chini nilisikitika sana hivi ni kweli Hawa polisi walio nilea Dodoma nyumba ya hospitali ya rufaa ndo wamekua wakatili hivi, wale polisi nilioangalia nao mpira Simba na yanga tunashangilia pamoja ndo Hawa?, ndo Hawa walioni stili hapo Dodoma nikisoma chuo dca college,kweli ndo wanafanya haya, no no no, siamini bado

Nilioangalia hiyo clip hakika nilitaka kulia barabarani hivi zile kampeni tulizo piga ndo malipo yake haya, kumpiga risasi huyo mama ambae hata jiwe hawezi rusha vizuri?, alafu mama huyo ni kopi lait na mama yangu mzazi alie nisomesha kwa shida akichoma vitumbua, aisee sijui TU hio kesi ili kua inaishaje huenda nyumba yake nyumba yangu ingekua mara kwanza najifunza ujambazi wa kutumia silaha sijui kisasi kinge mpata nani? Inaumiza kweli watz tumefikia hapo naona clip eti Hadi traffic nao walilia na mabunduki wakipiga watu risasi, Hawa traffic tunao Cheka nao barabarani kweliiii mnaua NDUG zetu simple like that, aisee nisameheni sitorudia tena ndugu zangu Niko chini ya miguu YENU Yani unalundika watu kawa unarundika Kuni kweli hii ndo tanzania tuitakayo kweliii nimeumia sana ogopa sana chozi la mtoto wa kiume lisilo na kelele, mungu hatuna silaha kama wao, hatuna bunduki kama wao ila wewe ni WA wote
Chai
 
Alex Khalifa, mshukuru Mungu aliyekuonesha na kukupa hekima ya kugundua kuwa ulikuwa upande wa shetani, ukimshabikia shetani, na sasa amekuonesha ubaya wa huyo shetani. Tambua kuwa wapo wengi wanaishi na kumtukuza shetani kwa kutenda uovu mpaka siku ya mwisho, wakiamini ni watu wema.

Nina imani, pale ulipouona uovu wa watawala wa nchi, na ukasononeka na kuumia moyoni, na kutambua kuwa kumbe ulikuwa unawashabikia wauaji, pale pale ulipokea msamaha wa Mungu.

Ukiwa umeokolewa kutoka kundi la wauaji, tambua kuwa Mungu wetu ni Mungu wa haki, anatutaka tutende haki, tuitangaze haki, tuitafute haki na kuilinda haki, hasa kwa wale wenzetu wanaonewa. Neno la Mungu linasema, "Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa. Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.
Nashukuru ndugu yangu mungu atubariki wote, waliobaki HUKO wengi sio watanzania amini mtanzania wa kweli huwezi jikaza kwa hizo clip ndugu yangu yule mjeda alizungumza Hilo na wengi Wana vyeo serikalin ndo mana hawateteleki tuikomboe Tanganyika NDUG zangu
 
Nisameheni ndugu zangu Kuna watu hawajui maumivu tunayopitia huyo ingekua live namjua nilikua nawasha gari nampitia namrudia kumalizia KABISA hao ndo wanao Fanya tunapoteza mama zetu, kaka zetu na wadogo zetu kisa vimishahara

Poleee Alex khalifa

Binadamu tunatofautiana vile tunavyoyachukulia mambo,huyo uliyemtukana unaona yanayotokea lakini kaamua kubaki anapoamini ni sawa kwake
 
Yeah, hata hivyo umetisha kumtukana back
Shukrani mkuu vita tunazipiga kotekote wakija huku tunao wakitupeleka KULE tunao ndo kama huyo angenijibu tena sijui NINGE pigwa ban ngapi nmeanda matusi lakin hakurudi
 
Kuna namna naona kwa angle tofaut...kuna maaskari waliamua kuua makusudi ili hasira za wananchi ziwe juu na kuweza kuja front na kuiangusha serikali...lkn pia kuna wale walikuwa wanaua kwa aitha malipo au ni makada wa chama kindaki ndaki
Inaweza kuwa ila Hawa jama ata elimu zao ni ndogo sana hawezi kung'amua mambo wao ni fatafata TU masikini
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom