Alex Khalifa, mshukuru Mungu aliyekuonesha na kukupa hekima ya kugundua kuwa ulikuwa upande wa shetani, ukimshabikia shetani, na sasa amekuonesha ubaya wa huyo shetani. Tambua kuwa wapo wengi wanaishi na kumtukuza shetani kwa kutenda uovu mpaka siku ya mwisho, wakiamini ni watu wema.
Nina imani, pale ulipouona uovu wa watawala wa nchi, na ukasononeka na kuumia moyoni, na kutambua kuwa kumbe ulikuwa unawashabikia wauaji, pale pale ulipokea msamaha wa Mungu.
Ukiwa umeokolewa kutoka kundi la wauaji, tambua kuwa Mungu wetu ni Mungu wa haki, anatutaka tutende haki, tuitangaze haki, tuotafute haki na kuilinda haki, hasa kwa wale wenzetu wanaonewa. Neno la Mungu linasema, "Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa. Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.