Basi leo mchana saa nane nikasema niende nikapate msosi kwenye hoteli moja kubwa na mpya hapa jiji la masamaki. Naingia tu nakutana na wahudumu wanne wamekaa, mteja alikuwa mmoja. Mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo:
Mimi: "Chakula kiko tayari?"
Muhudumu: "Sijajua ngoja nikaulizie kama kiko tayari"
Mimi: "Je leo kuna chakula gani:
Mhudumu: Ngoja nikaulize leo kuna nini?"
Mimi: "Sasa mbona ni saa nane mchana, kweli mmekaa hapa hamjaulizia kama kiko tayari na wamepika nini? Si mumeingia asubuhi nyinyi? Saa moja mpaka saa nane mhudumu hujui kinapikwa nini na saa ngapi kitakuwa tayari?"
Mhudumu: ndio tulikuwa tunajiandaa kuulizia, ila tulikuwa tunajua vifungua kinywa vya asubuhui
Mimi: Mh?
Hiyo hoteli ni mpya, ina karibu miezi mitatu tu na ilipofunguliwa ilikuwa inajaza hupati nafasi. Sasa nikajaribu kwenda kunawa hakuna maji mabomba yote, chooni nilipojaribu kuflash, kavu, nikatumia ndoo, ilibidi nitoke ndani nikae viti vya nje feni zote zimezimwa. Mbaya zaidi nimekaa zaidi ya dakika 15 nikisubiria chenji yangu na mhudumu hakuomba hata samahani. Kibaya zaidi quality ya chakula ni shida tupu, unakula kama makapi, hakuna tena taste food ya zamani.
Nikafikiria inawezekana boss hajui kinachoendelea hapa, Wahudumu hawako serious kabisa, wapishi hao ndio usiseme, msimamizi yeye yuko kama boya.
Ndio maana narudia kusema biashara nyingi hapa Bongo zinakufa kwa sababu ya wahudumu, wauzaji, waandaaji na wasimamizi. Ndio maana mabosi wengi hasa wa baa lazima wawepo asuhuhi, mchana na usiku. Usishangae pia pale unapokuta baa /hoteli kubwa wanaajiri wakenya, waganda, hao jamaa wana uzoefu na uvivu na kutokuwa serious kwa watu wetu.
Hivi nini kifanyike kutibu maradhi chronic haya?