Wabongo tuko nyuma sana kwenye Customer Services, kibaya Hatuko serious na Kazi kabisa. Acha Wakenya wachukue nafasi zetu

Wabongo tuko nyuma sana kwenye Customer Services, kibaya Hatuko serious na Kazi kabisa. Acha Wakenya wachukue nafasi zetu

Kwenye migahawa kuna wateja huwa ni waxenge sana, unakuta mtu kutoa pesa yake anaionea uchungu kweli kweli, atamsumbua muhudumu hadi sisi wateja wengine tunakereka, unakuta dosari ndogo tu, mtu anaanza kuunguruma, sio migahawa midogo wala mikubwa kuna wateja chenga sana.

Ndugu wale wahudumu mishahara yao ni ipo chini sana, hawana cha kufanya, kuweni wakarimu na muache na tip utaona watakavyokuchangamkia next time ukienda.
 
Kila kazi ina taaluma na kuisomea pia
Sisi kila kazi tunajifanya tunajua na kuajiri watu wasiofaa kabisa mradi wanahitaji watu wa kazi
Niligairi kumsajili mwanangu Shule moja baada ya kuingia ofisini nikakuta mmoja kakaa juu ya meza na wengine wawili wanachat
Niliwaambia tu mnaharibu biashara za wenzenu
Nikaondoka bila neno lingine
Sasa watu kama hao ndio unawakuta kila sehemu kwanza hawana adabu
Na hawajali nani kaingia na anataka nini
Mpaka ofisi za Umma hivyo hivyo, halafu wakileta wenye taaluma yao wabongo wanaanza kulialia
Mpaka changu anataka achukue mzungu na lugha hana wakija wenzie wanapitia wanabaki kulia
Kila mahali ni hao hao sijui kazi gani wanaweza

Uko sahihi kabisa wacha waajiri wa nje
 
Si uende ukale hotel nyingine? Acha ukuda.
Husifikiri nimeandika kwa ajili yangu. Si umeona nilikula nikaodoka. Nimeandika kwa sababu hili suala la kutokuiwa serious kwenye kazi ni corss-cutting na likatuhus sector karibu zote za services; maofisini, kwenye wakandarasi, mashuleni, vyuoni, mashambabi etc kwa hiyo nimeandika kwa ajili yetu sote ili tubadilike. Na hili la kutoshout kwenye uvundo pia ni udhaifu wetu;eti si ungekula na kuondoka , na wewe basi si ungepita tu bila kusoma na kuondoka, au si ungesoma halafu ukaondoka zako ukawaacha waelewa wachangie
 
Husifikiri nimeandika kwa ajili yangu. Si umeona nilikula nikaondoka. Nimeandika kwa sababu hili suala la kutokuwa serious kwenye kazi ni cross-cutting na linahusu sector karibu zote za services; maofisini, kwenye wakandarasi, mashuleni, vyuoni, mashambabi etc kwa hiyo nimeandika kwa ajili yetu sote ili tubadilike. Na hili la kutoshout, kuogopa kushout kwenye uvundo pia ni udhaifu wetu;eti si ungekula na kuondoka , na wewe basi si ungepita tu bila kusoma na kuondoka, au si ungesoma halafu ukaondoka zako ukawaacha waelewa wachangie
 
Imagine limtu linatangaza biashara linaweka picha haliweki bei. ..ukiliuliza linakwambia njoo inbox huko inbox halijibu kwa wakati unajiuliza hili limjtu linauza bidhaa au linajiuza lenyewe..wafanyabiashara hawajui pesa jko kwenye matangazo,kujibu maulizo ya wateja kwa wakati,inagharimu nn kuweka bei moja kwa moja hadi ukatongozwe inbox ila waTZ bana..madirisha 6 ya bank moja mawili yanafanyakazi mmojaa nahudumia kwa nyodo mmoja anatoka kila baada ya dkk kumi ..shame..
 
Hilo swala Salim kikeke alishawahi kulisema ni changamoto kwa kweli.
 
Tuko slow sana. Kufanya kazi, kutembea, kufikiri, kuamuwa....
Ila kwenye WIZI?! Hatarii....
 
Back
Top Bottom