Wabongo tuna sifa, sasa hadi CPA wameifanya kuwa kama Mr, Mrs, Dr, Sr katika majina yao

Nadhani hii huchagizwa na inferiority complex iliyopo ndani ya watu. Kwamba asipoweka hiyo initial ni kama hamtamtambua
wachungaji na masheikh nao wameiga kuitwa kwa kuanza na title, unaanza hivi: Askofu Dr. LOTH HEMA, Padri Dr. LOTH HEMA, Sheikh Dr. ...., Mchungaji Dr. ...., Mufti Mkuu Dr. ..., ENG. LOTH HEMA, Askofu mkuu CPA. .... Bado kidogo tutaanza kuona title zingine za heshima kwa viongozi wa dini
 
Inferiority complex it is a real complex,really do,!!iIt is killing au mental health kwa kweli
Jaribu tu kufuatilia sio kwa wanasiasa tu hata kwa wanaotuzunguka mtaani.. yaani wanatafuta namna yoyote kwenye mazungumzo wachomekee vimaneno ili watambulike kwa either kazi zao ,kipato chao au wanachomiliki.
 
Ni ulimbukeni tu, kuna mwingine anaitwa Eng. kila mahali wakati kazi yake kubwa ni siasa za mpira!
Eng. Masauni, muulize lini aliifanyia kazi fani yake.

Kina Dr. Kigwa, wale ni physicians ila leo hii akikosa kazi ya kisiasa hawezi tena kuingia wodini au kuattend wagonjwa.
 
Jaribu tu kufuatilia sio kwa wanasiasa tu hata kwa wanaotuzunguka mtaani.. yaani wanatafuta namna yoyote kwenye mazungumzo wachomekee vimaneno ili watambulike kwa either kazi zao ,kipato chao au wanachomiliki.
Kuna wengine wanatafuta namna wakuoneshe hata vyeti na taarifa zao kabisa
 
Sasa hivi imekuwa order of the day. Mtajuaje kama ana PhD asipojitambulisha na hiyo title ?
 
Artist LOTH HEMA, Mwalimu LOTH HEMA, painter, printer, carpenter, profesa LOTH HEMA, sipati picha kila mtu akianza kuitwa jina lake kwa kuanza kutaja fani/taaluma yake
CPA Makala, Dr. Msukuma, Eng. Hersi, Mwl. Jumanne, hizo acronyms zinaitwa kishangilio.
Ukiwa chuo kikuu usipomuaddress mhadhiri wako kwa kishangilio chake kama Prof. Au Dr. Unakula disco
 
Utata wa kuitwa hizi title ni kwamba mtu anaanza kuitwa hivyo muda mfupi tangu tusikie ameenda kusoma. Tunajua prossess mpaka uje uitwe hivyo ni ndefu. Kuna mmoja yeye alikuwa ni Dr. tayari anaitwa kwa kuanza na title hiyo, mara akawa waziri na kuanza kuitwa Profesa. Lini alirudi chuoni kutunukiwa hadhi hiyo?
 
Wenye taaluma za kihasibu ngazi ya shahada ya CPA waliapa kudumisha proffession kwa vitendo kwa ueledi wa hali ya juu na awe amenyooka katika utendaji wake.Hivyo, kwa mwenye CPA kuwa mwanasiasa kama makala ni changamoto kubwa kiproffession.Ukitaka kujua tofauti mlinganishe na prfo Assad
 
Nyerere alikuwa na phd ila hakuwahi jiita dokta nyerere. Mzee alikuwa anajitambua na kuishi kwa maadili ya uongozi sana.

Ila hawa wasasa utasikia, Mheshimiwa Professor Dokta engineer CPA advocate James Musimbugwane.

Sijui huwa wanahisi hizi title zinawapa mileage gani eneo la heshima wapuuzi hawa
 
Nabii ni mbongo pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…