Wabunge 19 kufungua kesi, vigogo CCM na ofisi ya Spika wahusishwa katika uratibu

Acha porojo,hujui kuwa Halima ni Mwanasheria kitaaluma?

Unadhani hajui jinsi ya kuulinda ubunge wake?

Kama mlimfukuza kihuni kama alivyosema Mahakama itamoa haki hake
Soma sheria na taratibu za chadema ndo utoe comments[emoji116][emoji116][emoji116]

Kanuni za kusimamia shughuli, mwenendo na maadili ya wabunge wa Chadema (2006), kifungu cha 8.0 (a) (x); zinasomeka ifuatavyo; “Chadema itashughulikia matatizo ya viongozi na wanachama kwa kufuata taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa katiba ya chama, wala hata siku moja haitashughulikia mambo kama hayo mahakamani. Mwanachama atakayeshindwa kufuata taratibu na ngazi za chama hatavumiliwa na atafukuzwa uanachama”

Sent from my SM-G973U using JamiiForums mobile app
 
Hapa kunaweza kutokea mgogoro wa kikatiba.

Hili ni suala la kisiasa na kibunge na mahakama inatakiwa ilirudishe kwenye chama na muhimili wa Bunge ili limalizwe katika chama na muhimili wa Bunge.

Mahakama ikibatilisha maamuzi ya chama itakuwa imeingilia demokrasia ya chama
 
It's very common under ccm regime.
 
Kwenye maelezo yako,hukubainisha ni nani alimwachia Nusrat Henje toka gerezani usiku wa manane na kumpeleka kuapishwa Dodoma.
Au ni mnene huyo huyo wa Chadema.
Mimi sizungumzii kuhusu watu, nazungumzia kukiukwa kwa katiba, sheria, taratibu na kanuni
P.
 
Mimi sizungumzii kuhusu watu, nazungumzia kukiukwa kwa katiba, sheria, taratibu na kanuni
P.
Soma sheria na taratibu za chadema ndo utoe comments[emoji116][emoji116][emoji116]

Kanuni za kusimamia shughuli, mwenendo na maadili ya wabunge wa Chadema (2006), kifungu cha 8.0 (a) (x); zinasomeka ifuatavyo; “Chadema itashughulikia matatizo ya viongozi na wanachama kwa kufuata taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa katiba ya chama, wala hata siku moja haitashughulikia mambo kama hayo mahakamani. Mwanachama atakayeshindwa kufuata taratibu na ngazi za chama hatavumiliwa na atafukuzwa uanachama”

Sent from my SM-G973U using JamiiForums mobile app
 
Serikali ya awamu ya 6 inaendeshwa na watu wengine kabisa , wala si hawa tunaowaona , wanapangiwa mambo yote na wahafidhina .
Ndiyo hapa ambapo mtu inafikia hatua anaongea hata ambayo hakujipanga kuongea, maana akikosea anapewa kimemo kukumbushwa, kisa cha late au nafasi hiyo sisi ndiyo tumekupa, daaa!
 
Sawa lakini kesi hii itafungua uvundo wa:
1. Uhalali wa ubunge wa hawa COVID-19 toka mwanzo.
2. Uhalali wa bunge lenyewe kuanzia Uchaguzi Mkuu wa 2020.
3. Uhalali wa Uchaguzi Mkuu wenyewe wa 2020.
 
Halima james mdee...ukivuka sana " hubofoka" pasuka" kaa jitafakar
 
Acha porojo,hujui kuwa Halima ni Mwanasheria kitaaluma?

Unadhani hajui jinsi ya kuulinda ubunge wake?

Kama mlimfukuza kihuni kama alivyosema Mahakama itamoa haki hake
Hata kingai alisomea Sheria bob
 
Mbowe angependa kuona wanabaki sema presha ya wahuni ndio imembana, sikuile alikuwa mnyonge sana.
 
Mahakama ndicho chombo pekee cha utoaji haki ndani ya JMT.
It's very unfortunately katiba ya Chadema, haikitambui hilo!.
P
Tunaamini kwamba mahakamani kuna haki?
Ni kweli sabaya hajafanya aliyohukumiwa nayo?
Wapo wangapi wanatupikia viungo na hawakufanya zaidi ya sabaya tu kwakuwa siyo kama sabaya?
Dhana ta uhuru wa makama ipo? Wewe unaiamini?
 
Watakuwa wamejifuta moja Kwa moja uanachama wa CHADEMA kwa mujibu wa Katiba ya CDM.
 
Mahakama ndicho chombo pekee cha utoaji haki ndani ya JMT.
It's very unfortunately katiba ya Chadema, haikitambui hilo!.
P
Kwa hiyo ili mtu avuliwe uanachama wa chama cha siasa inabidi chama kikamvulie uanachama huo makamani?
Kama ndivyo, ni mahakama IPI ilimvua uanachama Jesca Msambatavangu, Sofia Simba, Bernard Membe etc?

Hii double standard ndani ya bunge ktk kufanyia kazi maamuzi ya vyama vya siasa kwa wanachama wao ni sumu nyingine inayolitafuna taifa letu taratibu!

Ngoja tuendelee kusubiri mwisho wake!
Themnyonge,
Kwa sasa kijijini milima ya Livingston!
 
Unasema "wakikosa haki yao ndani ya CHADEMA wakimbilie wapi?"
Pascal Mayalla, tangu umekuwa mtu mzima, na kuelimika vya kutosha, naomba reference yoyote ya mwanachama wa C aliyewahi kufukuzwa uanachama akaenda mahakamani kukataa kufukuzwa uanachama, na mahakama ikamrudishia uanachama wake!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…