Wabunge 19 Viti Maalum CHADEMA wafungua kesi. Bunge lasema linasubiri uamuzi wa Mahakama Kuu

Wabunge 19 Viti Maalum CHADEMA wafungua kesi. Bunge lasema linasubiri uamuzi wa Mahakama Kuu

At least amekubali kuwa CHADEMA wamefanya maamuzi yao na Bunge limepokea uamuzi wa chama cha hao wanawake..

Hii maana yake ni kubwa, mpira upo kwa Bunge/Spika. CHADEMA wamemaliza ya upande wao. Hawadaiwi tena...

Now, the game is between COVID 19 vs BUNGE vs SHERIA na KATIBA YA NCHI..!
 
Spika anasema Wabunge 19 wa CHADEMA wamepeleka kesi mahakamani, pia amesema afisa wa CHADEMA alifika bungeni bila kukabidhi barua hiyo baada ya kuambiwa muda umekwisha bungeni. Bunge lilipokea barua pepe iliyosainiwa na katibu mkuu juu ya maamuzi ya kikao cha baraza kuu juu ya kukataliwa rufaa ya wabunge 19 wa Chadema.

Spika amesema tarehe 13 Mei, barua hiyo iliwasilishwa ofisini kwake kwa mkono na baada ikapokea barua hiyohiyo kwa DHL.

Spika amesema Mamlaka ya mwisho ya utoaji haki ni mahakama katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivyo Bunge haliwezi kuingilia mchakato wa mahakama hivyo inalazima kusubiri mpaka mahakama itapotoa uamuzi wake.
Lete ushahidi
 
Hivi haya maamuzi ya Bunge Yana double standards?

Mbona wake wabunge wa CUF walipofukuzwa na Mwenyekiti wanayemtambua wao Lipumba, wabunge wale wakifukuzwa mara moja?

Mbona Sofia Simba alipofukuzwa na CCM, ilitekelezwa mara MOJA?

Iweje Hawa wabunge 19 wa viti maalum, kuwepo na kigugumizi cha kuwatimua Bungeni?
Abiria ndani ya meli tunaiona pwani ileeeee!! Soon meli itatia nanga BANDARI SALAMA.
 
Taarifa niliyo ipata HV punde kutoka bungeni Ni kwamba spika Dr tulia amelitolea ufafanuzi swala la kina mdee na wenzake na kusema ni kweli amepokea barua ingawa hawez kuwaondoa bungeni hvyo wataendelea kuwa bungeni had mahakama itakavyo amua vinginevyo ila yey Hana mamlaka ya kuwa fukuza ....

Nina haraka kdg nawai tabata dampo

JMT ....KAZI IENDELEEEEEEEEE
 
Lakini eleweni mnaowaumiza ni wananchi! Kuna kipindi kama wananchi inabidi tuwe serious. Wakishindwa na huko mahakamani, Watarudisha hizi pesa ambazo wataendelea kuzipokea?

Tuna wasomi wapumbavu nchii hii mmoja wapo ni huyo Tulia.
 
Kuna uzi wa Ushimen ulisema hili na nilicomment kuwa mwisho wa siku kisingizio kitakuwa mahakama. Hii nchi ni rahisi sana kuitabiri.
Swala sio mahakama ila ni uhuni wa Mbowe ....anajua kila kitu kinavyokwenda na hata mkutano mkuu ulipo kaa juzi hakuruhusu kutenguliwa kwa maamuzi ya kamati kuu ila walibariki maamuzi yaliyovunja katiba yao wenyewe... akijua kabisa wataenda mahakamani na yeye kama mnufaika ataaendelea kupata fedha za kuendeshea chama na shughuli zake. So stay tune.
 
Hivi haya maamuzi ya Bunge yana double standards?

Mbona wake wabunge wa CUF walipofukuzwa na Mwenyekiti wanayemtambua wao Lipumba, wabunge wale walifukuzwa mara moja?

Mbona Sofia Simba alipofukuzwa na CCM, ilitekelezwa mara moja?

Iweje Hawa wabunge 19 wa viti maalum kutoka Chadema, ambapo vikao vyote 2 vya chama, kwa maana ya Kamati Kuu na Baraza Kuu, vikisema wazi kuwa hao wabunge, weshafukuzwa na chama chao cha Chadema, kuwepo na kigugumizi cha kuwatimua Bungeni?

Hivi huyo Spika wa Bunge, Tulia Ackson, ambaye ana Shahada ya PhD ya sheria, haoni namna anavyodhalilisha taaluma hii ya sheria?
Walikwenda mahakamani kabla ya kufukuzwa?
 
Leo spika wa Bunge ameelezea sakata la wabunge 19 wa viti maalum CHADEMA waliofukuzwa na chama chao. Kwa ufupi, wabunge husika wamefungua kesi mahakamani kupinga maamuzi ya baraza kuu la CHADEMA na Bunge limesema halitaweza kutangaza viti hivyo kuwa wazi kuuheshimu muhimili mwenzake wa mahakama.

=====

Spika anasema wabunge 19 wa CHADEMA wamepeleka kesi mahakamani, pia amesema afisa wa CHADEMA alifika bungeni bila kukabidhi barua hiyo baada ya kuambiwa muda umekwisha bungeni. Bunge lilipokea barua pepe iliyosainiwa na katibu mkuu juu ya maamuzi ya kikao cha baraza kuu juu ya kukataliwa rufaa ya wabunge 19 wa Chadema.

Spika amesema tarehe 13 Mei, barua hiyo iliwasilishwa ofisini kwake kwa mkono na baada ikapokea barua hiyohiyo kwa DHL.

Spika amesema Mamlaka ya mwisho ya utoaji haki ni mahakama katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivyo Bunge haliwezi kuingilia mchakato wa mahakama hivyo inalazima kusubiri mpaka mahakama itapotoa uamuzi wake.

Nchi ya kijinga Sana.
 
Maamuzi ya kukurupuka na hisia ya CHADEMA bila kuzingatia haki, sheria a katiba yake imepelekea haya yote.

mngefuata utaratibu hao wabunge hata wasingekwenda mahakamani

Ila dawa ya uhuni ni uhuni tu

nawapomgeza wabunge 19 kwa kutafuta haki yao mahakamani na iwe fundisho kwa CHADEMA kukandamiza sheria linapokuja suala la wanachama wake
 
Back
Top Bottom