Wabunge 19 Viti Maalum CHADEMA wafungua kesi. Bunge lasema linasubiri uamuzi wa Mahakama Kuu

Wabunge 19 Viti Maalum CHADEMA wafungua kesi. Bunge lasema linasubiri uamuzi wa Mahakama Kuu

Hivi haya maamuzi ya Bunge yana double standards?

Mbona wake wabunge wa CUF walipofukuzwa na Mwenyekiti wanayemtambua wao Lipumba, wabunge wale walifukuzwa mara moja?

Mbona Sofia Simba alipofukuzwa na CCM, ilitekelezwa mara moja?

Iweje Hawa wabunge 19 wa viti maalum kutoka Chadema, ambapo vikao vyote 2 vya chama, kwa maana ya Kamati Kuu na Baraza Kuu, vikisema wazi kuwa hao wabunge, weshafukuzwa na chama chao cha Chadema, kuwepo na kigugumizi cha kuwatimua Bungeni?

Hivi huyo Spika wa Bunge, Tulia Ackson, ambaye ana Shahada ya PhD ya sheria, haoni namna anavyodhalilisha taaluma yake ya sheria, kwa ajili tu ya kuinufaisha CCM?🥺
Wabunge wa CCM walipofukuzwa hawakwenda mahakamani
 
Nimesoma kupitia mtandao wa Jamii foroums kuwa Wabunge 19 wa CHADEMA wamefungua kesi Mahakamani. Je CHADEMA itakubali kwenda kutoa utetezi Mahakamani?.
 
Hili Jambo tulilitegemea wengi...maamuzi ya mahakama yatatoka 2025...covid wanavuta mafao wanaelekea wanakostahili...
 
Hivi haya maamuzi ya Bunge yana double standards?

Mbona wale wabunge wa CUF walipofukuzwa na Mwenyekiti wanayemtambua wao Lipumba, wabunge wale walifukuzwa mara moja na Bunge hilo??

Mbona Sofia Simba alipofukuzwa na CCM, ilitekelezwa mara moja na Bunge hilo hilo??

Iweje Hawa wabunge 19 wa viti maalum kutoka Chadema, ambapo vikao vyote 2 vya chama, kwa maana ya Kamati Kuu na Baraza Kuu, vikisema wazi kuwa hao wabunge, weshafukuzwa na chama chao cha Chadema, kuwepo na kigugumizi cha kuwatimua Bungeni??

Hivi huyo Spika wa Bunge, Tulia Ackson, ambaye ana Shahada ya PhD ya sheria, haoni namna anavyodhalilisha taaluma yake ya sheria, kwa ajili tu ya kuinufaisha CCM?[emoji3064]
Tulia ww Bavicha ufundishwe uongozi.
 
Leo spika wa Bunge ameelezea sakata la wabunge 19 wa viti maalum CHADEMA waliofukuzwa na chama chao. Kwa ufupi, wabunge husika wamefungua kesi mahakamani kupinga maamuzi ya baraza kuu la CHADEMA na Bunge limesema halitaweza kutangaza viti hivyo kuwa wazi kuuheshimu muhimili mwenzake wa mahakama.

=====

Spika anasema wabunge 19 wa CHADEMA wamepeleka kesi mahakamani, pia amesema afisa wa CHADEMA alifika bungeni bila kukabidhi barua hiyo baada ya kuambiwa muda umekwisha bungeni. Bunge lilipokea barua pepe iliyosainiwa na katibu mkuu juu ya maamuzi ya kikao cha baraza kuu juu ya kukataliwa rufaa ya wabunge 19 wa Chadema.

Spika amesema tarehe 13 Mei, barua hiyo iliwasilishwa ofisini kwake kwa mkono na baada ikapokea barua hiyohiyo kwa DHL.

Spika amesema Mamlaka ya mwisho ya utoaji haki ni mahakama katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivyo Bunge haliwezi kuingilia mchakato wa mahakama hivyo inalazima kusubiri mpaka mahakama itapotoa uamuzi wake.

Mbona kwa Lissu mahakama ilisema haitawaingilia Bunge?
 
Hivi haya maamuzi ya Bunge yana double standards?

Mbona wale wabunge wa CUF walipofukuzwa na Mwenyekiti wanayemtambua wao Lipumba, wabunge wale walifukuzwa mara moja na Bunge hilo??

Mbona Sofia Simba alipofukuzwa na CCM, ilitekelezwa mara moja na Bunge hilo hilo??

Iweje Hawa wabunge 19 wa viti maalum kutoka Chadema, ambapo vikao vyote 2 vya juu vya chama hicho, kwa maana ya Kamati Kuu na Baraza Kuu, vikisema wazi kuwa hao wabunge, weshafukuzwa na chama chao cha Chadema, kuwepo na kigugumizi cha kuwatimua Bungeni??

Hivi huyo Spika wa Bunge, Tulia Ackson, ambaye ana Shahada ya PhD ya sheria, haoni namna anavyodhalilisha taaluma yake ya sheria, kwa ajili tu ya kuinufaisha CCM?[emoji3064]

Ni kwa sababu hawakuwahi kwenda mahakamani!
 
Mwendelezo wa ushenzi wa awamu iliopita. Upuuzi huu unamchafua hadi mama. Mahakama iliyo wapiga dana dana masheikh wa Zanzibar na Mbowe siyo chombo cha kutenda haki.
Kwa hiyo unataka Rais aingilie maamuzi ya mahakama?

Mama anaheshimu sheria

Mambo ya bunge yabaki bungeni

Mahakama pia ibaki kuwa mahakama

Msimpe mama lawama asizohusika nazo
 
Leo spika wa Bunge ameelezea sakata la wabunge 19 wa viti maalum CHADEMA waliofukuzwa na chama chao. Kwa ufupi, wabunge husika wamefungua kesi mahakamani kupinga maamuzi ya baraza kuu la CHADEMA na Bunge limesema halitaweza kutangaza viti hivyo kuwa wazi kuuheshimu muhimili mwenzake wa mahakama.

=====

Spika amesema taarifa walianza kuiona kwenye mitandao ya kijamii usiku wa tarehe 11 Mei kwamba baraza kuu la CHADEMA limeazimia kukubaliana na uamuzi wa kamati kuu ya CHADEMA kuwafukuza uanachama wabunge 19 kupitia chama hicho.

Tarehe 12 Mei kwa njia ya barua pepe, wabunge hao 19 walimfahamisha spika maamuzi yaliyofikiwa na baraza kuu kwamba si halali, yako kinyume na katiba ya Tanzania na hayakuzingatia haki ya msingi ya kuwasikiliza au kuwaruhusu kujitetea.

Wabunge 19 wa CHADEMA wamepeleka kesi mahakamani, pia amesema afisa wa CHADEMA alifika bungeni bila kukabidhi barua hiyo baada ya kuambiwa muda umekwisha bungeni. Bunge lilipokea barua pepe iliyosainiwa na katibu mkuu juu ya maamuzi ya kikao cha baraza kuu juu ya kukataliwa rufaa ya wabunge 19 wa Chadema.

Spika amesema tarehe 13 Mei, barua hiyo iliwasilishwa ofisini kwake kwa mkono na baada ikapokea barua hiyohiyo kwa DHL.

Spika amesema Mamlaka ya mwisho ya utoaji haki ni mahakama katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivyo Bunge haliwezi kuingilia mchakato wa mahakama hivyo inalazima kusubiri mpaka mahakama itapotoa uamuzi wake.

Yote haya kisa Ni chadema. Yani katika nchi Chadema haina haki hata kwa wanachama wake?.
 
At least amekubali kuwa CHADEMA wamefanya maamuzi yao na Bunge limepokea uamuzi wa chama cha hao wanawake..

Hii maana yake ni kubwa, mpira upo kwa Bunge/Spika. CHADEMA wamemaliza ya upande wao. Hawadaiwi tena...

Now, the game is between COVID 19 vs BUNGE vs SHERIA na KATIBA YA NCHI..!
Wewe na wewe unajifanya unaakili kumbe ni kichwa cha panzi tu, Bunge ndilo limemaliza na sasa ni mapambano ya kesi kati Wabunge 19 na chadema mahakamani, na Kule wanaenda kuangalia km mchakato wa kuwafukuza ulifanyika sahihi aunque batili pamoja na hoja nyingine ambazo zitakuwa zimefika mahakamani dhidi ya kesi Hiyo ambayo sasa ni mpambano kati ya Kinahalima Mdee na Chadema
 
Kwanza huyu Tulia anasubiri simu kutoka Ikulu, hana maajabu yoyote yale, yupo yupo tu kusubiria maelekezo ya Samia na system juu ya hawa covid 19.
 
Hivi haya maamuzi ya Bunge yana double standards?

Mbona wale wabunge wa CUF walipofukuzwa na Mwenyekiti wanayemtambua wao Lipumba, wabunge wale walifukuzwa mara moja na Bunge hilo??

Mbona Sofia Simba alipofukuzwa na CCM, ilitekelezwa mara moja na Bunge hilo hilo??

Iweje Hawa wabunge 19 wa viti maalum kutoka Chadema, ambapo vikao vyote 2 vya juu vya chama hicho, kwa maana ya Kamati Kuu na Baraza Kuu, vikisema wazi kuwa hao wabunge, weshafukuzwa na chama chao cha Chadema, kuwepo na kigugumizi cha kuwatimua Bungeni??

Hivi huyo Spika wa Bunge, Tulia Ackson, ambaye ana Shahada ya PhD ya sheria, haoni namna anavyodhalilisha taaluma yake ya sheria, kwa ajili tu ya kuinufaisha CCM?[emoji3064]

Ukiwahibmahakamani basi mambo yote yanasimama. Rejea kesi ya Zitto Kabwe alipofukuzwa na Chadema. Kesi ilikaa miaka miwili hadi bunge linavunjws na yeye kupata haki zake zote kama mbungr mstaafu! Hata hii inaweza kuunguruma miaka mitatu hadi 2025.
 
Huwa najiuliza maswali mengi sipati majibu.. hivi CCM inafaidika vp na hao wabunge 19? Kwanini mnahubiri maridhiano wakati nyie hampo tayari? Mnaturudisha nyuma Sana. Achanane na siasa za kukomoana tusonge mbele.
 
Back
Top Bottom