Wabunge 19 Viti Maalum CHADEMA wafungua kesi. Bunge lasema linasubiri uamuzi wa Mahakama Kuu

Wabunge 19 Viti Maalum CHADEMA wafungua kesi. Bunge lasema linasubiri uamuzi wa Mahakama Kuu

CHADEMA inaweza kufungua kesi dhidi ya wabunge 19 waliowafukuza kwenye chama chao kwamba hawawatambui, wasijitambulishe, wasitambuliwe na wasiitwe wanachama au wabunge wa CHADEMA.

Hiyo ndio kesi pekee CHADEMA wanayoweza kufungua mahakamani uamuzi ukatolewa ndani ya muda mfupi na kuna uwezekano mkubwa wa kushinda. Kesi nyingine yoyote inayohusu kutaka wabunge hao waondolewe bungeni itamalizika 2025.

Tatizo viongozi wetu wamerelax wakidhani CCM watawaonea huruma. Shauri zao. Kesi haijaanza hata kusikilizwa spika anasema anasubiri uamuzi wake.
 
Maswali fikirishi kwa wabobezi wa Sheria
-Kwani Kuna zuio la Mahakama (Court injunction) kwenda kwa spika na taasisi zingine mpaka shauri liliofunguliwa limalizike,wabobezi wa Sheria tusaidie.
-Kwa mujibu wa maelezo ya spika,hawa wabunge,wataendelea kuwa wabunge mpaka 2025,sioni uwezekano wa Mahakama kusikiliza Case na kumalizika mapema.
-Hata kama Mahakama Kuu itatoa hukumu mapema,Mdee na wenziwe watakata rufaa Mahakama Kuu ya Rufaa Tanzania (Tanzania High Court of Appeal).ili kuchelewesha mchakato wa kuondolewa bungeni.
-Kwa Mujibu wa barua ya John Mnyika inaonekana, CHADEMA wanataka spika aendeshe Bunge bila ya kuwa na kambi rasmi ya upinzani, hususani kwenye kamati za Bunge ambazo lazima wenyeviti wake watoke upinzani (PAC nk)
-Chadema walipaswa kutoa taarifa ya kuwaondoa uanachama akina Mdee na kupeleka majina ya wabunge wengine mbadala.
 
Hivi haya maamuzi ya Bunge yana double standards?

Mbona wale wabunge wa CUF walipofukuzwa na Mwenyekiti wanayemtambua wao Lipumba, wabunge wale walifukuzwa mara moja na Bunge hilo??

Mbona Sofia Simba alipofukuzwa na CCM, ilitekelezwa mara moja na Bunge hilo hilo??

Iweje Hawa wabunge 19 wa viti maalum kutoka Chadema, ambapo vikao vyote 2 vya juu vya chama hicho, kwa maana ya Kamati Kuu na Baraza Kuu, vikisema wazi kuwa hao wabunge, weshafukuzwa na chama chao cha Chadema, kuwepo na kigugumizi cha kuwatimua Bungeni??

Hivi huyo Spika wa Bunge, Tulia Ackson, ambaye ana Shahada ya PhD ya sheria, haoni namna anavyodhalilisha taaluma yake ya sheria, kwa ajili tu ya kuinufaisha CCM?[emoji3064]
Kwani wakiingia humo bungeni,mkiwa humuwatambui mnaumia nini?
Achaneni nao endeleeni na mambo yenu

Sent from my SM-G5500 using JamiiForums mobile app
 
Kwa mahesabu ninayo yaona hapa ,hao wabunge wa covid 19 wataendelea kuwa wabunge mpaka awamu hii iishe bila kufanya hivyo ni kuharamisha serekali yote ya awamu hii .
 
Maamuzi ya kukurupuka na hisia ya CHADEMA bila kuzingatia haki, sheria a katiba yake imepelekea haya yote.

mngefuata utaratibu hao wabunge hata wasingekwenda mahakamani

Ila dawa ya uhuni ni uhuni tu

nawapomgeza wabunge 19 kwa kutafuta haki yao mahakamani na iwe fundisho kwa CHADEMA kukandamiza sheria linapokuja suala la wanachama wake
Utaratibu upi unaozungumzia? Hawa wanachotaka ni ubunge na hamna kikingine. Hawana mpango wa kurudi Chadema maana wanajua hawakubaliki. Na wakishindwa Mahakama Kuu, watakata rufaa Mahakama ya Rufaa, wakishindwa watakata rufaa ya Afrika Mashariki, wakishindwa watakata ya rufaa ya Afrika, wakishindwa wataenda the Hague. Yote hayo ili mradi wafike 2025 na wawazuie Chadema kupeleka wabunge wao.
Mna haki ya kuwapongeza kwa sababu kwenu chochote ambacho mnadhani kitawaumiza Chadema ni furaha kwenu. Chadema waachane nao.

Amandla...
 
Sarakasi za Uviko 19. Spika yupo sahihi, Bunge haliwezi kuingilia mhimili mwingine wa Mahakama. Ni jambo la kusubiria maamuzi ya Mahakama.

Mapovu Yaendelee...!
Jibu hoja ya msingi kwa kulinganisha na wale wa CUF. Hii double standard hata wewe inaweza kukuathiri.
 
Kwani wakiingia humo bungeni,mkiwa humuwatambui mnaumia nini?
Achaneni nao endeleeni na mambo yenu

Sent from my SM-G5500 using JamiiForums mobile app

Katiba inasema mbunge lazima adhaminiwe na chama. Sasa utakuwaje mbunge na hauna chama?. Haya yanafanyika kwa sababu Ni chadema hakuna jingine. Yani chadema inapambana na mihimili mitatu.
 
Wenye kuona mbali tulijaribu kuwashauri kwamba kwa kuwa hakuna asiyekosa hapa chini ya jua basi Hao wabunge wanaoitwa Covid wasamehewe tu ili kazi iendelee !! Hawakusikia !! Sasa itakuwa mguu na njia Kwenda Mahakamani mpaka year 2024 au 2025 !! Mapambano ya Sheria yanaanza stay tuned !!!
Aisee!.
Mama na JPM kumbe ni kitu kimoja.
 
Swala sio mahakama ila ni uhuni wa Mbowe ....anajua kila kitu kinavyokwenda na hata mkutano mkuu ulipo kaa juzi hakuruhusu kutenguliwa kwa maamuzi ya kamati kuu ila walibariki maamuzi yaliyovunja katiba yao wenyewe... akijua kabisa wataenda mahakamani na yeye kama mnufaika ataaendelea kupata fedha za kuendeshea chama na shughuli zake. So stay tune.
Wewe ni mpum.avu
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Chadomo ni wahuni sana, na wamekutana na wahuni wenzao!
Hivi ni kwa nini MaPsychopath MaCCM mmekosa huruma kabisa na kodi za masikini na bado mnawakamua MATOZO na hali ngumu yote hii.?! Huo sio uhuni ni UHAINI unafanywa na Tulia na CCM yake.
Chakufurahisha nini.
 
Maamuzi ya kukurupuka na hisia ya CHADEMA bila kuzingatia haki, sheria a katiba yake imepelekea haya yote.

mngefuata utaratibu hao wabunge hata wasingekwenda mahakamani

Ila dawa ya uhuni ni uhuni tu

nawapomgeza wabunge 19 kwa kutafuta haki yao mahakamani na iwe fundisho kwa CHADEMA kukandamiza sheria linapokuja suala la wanachama wake
Unadhani CHADEMA wangeweza kufanya jambo gani zaidi ya kuwafukuza mkuu? hebu tusaidie mawazo
 
Hivi haya maamuzi ya Bunge yana double standards?

Mbona wale wabunge wa CUF walipofukuzwa na Mwenyekiti wanayemtambua wao Lipumba, wabunge wale walifukuzwa mara moja na Bunge hilo??

Mbona Sofia Simba alipofukuzwa na CCM, ilitekelezwa mara moja na Bunge hilo hilo??

Iweje Hawa wabunge 19 wa viti maalum kutoka Chadema, ambapo vikao vyote 2 vya juu vya chama hicho, kwa maana ya Kamati Kuu na Baraza Kuu, vikisema wazi kuwa hao wabunge, weshafukuzwa na chama chao cha Chadema, kuwepo na kigugumizi cha kuwatimua Bungeni??

Hivi huyo Spika wa Bunge, Tulia Ackson, ambaye ana Shahada ya PhD ya sheria, haoni namna anavyodhalilisha taaluma yake ya sheria, kwa ajili tu ya kuinufaisha CCM?[emoji3064]
Hao wa cuf na ccm na wao walipekeka kesi mahakamani?
 
Utaratibu upi unaozungumzia? Hawa wanachotaka ni ubunge na hamna kikingine. Hawana mpango wa kurudi Chadema maana wanajua hawakubaliki. Na wakishindwa Mahakama Kuu, watakata rufaa Mahakama ya Rufaa, wakishindwa watakata rufaa ya Afrika Mashariki, wakishindwa watakata ya rufaa ya Afrika, wakishindwa wataenda the Hague. Yote hayo ili mradi wafike 2025 na wawazuie Chadema kupeleka wabunge wao.
Mna haki ya kuwapongeza kwa sababu kwenu chochote ambacho mnadhani kitawaumiza Chadema ni furaha kwenu. Chadema waachane nao.

Amandla...
Jibu hoja wacha kuleta hisia kwenye mambo ya msingi
 
Spika wa bunge mh TULIA acksoni mapema Leo amelitolea maelezo sakata la wabunge 19 wa chadema na kusema mahakama ndio itatoa uamuzi wa hatima ya wabunge 19 waliovuliwa uanachama na baraza kuu la chadema wiki iliyopita .

"Ninalazimika kutokutoa uamuzi wa wabunge 19 wa CHADEMA hadi pale mahakama itakapolitolea ufafanuzi na spika ndio atakayetoa uamuzi wa mwisho wa jambo hili sio vinginevyo"alisema mpika .

Kwa hiyo hii itawafanya wabunge 19 kuendelea kuwa bungeni mpaka hukumu

USSR
IMG-20220516-WA0026.jpg
 
Back
Top Bottom