Wabunge 19 Viti Maalum CHADEMA wafungua kesi. Bunge lasema linasubiri uamuzi wa Mahakama Kuu

Wabunge 19 Viti Maalum CHADEMA wafungua kesi. Bunge lasema linasubiri uamuzi wa Mahakama Kuu

Rahaaa mustarehee
Spika ametoa taarifa Bungeni kwamba, Bunge halina mamlaka ya kusitisha uwakilishi wa wabunge 19 waliofukuzwa Chadema akieleza kwamba chombo pekee chenye mamlaka ya kufanya maamuzi ya mwisho kisheria ni Mahakama.

Hivyo watasalia Bungenimpaka hapo Mahakama itakapotoa hukumu.
 
Nchi ya ajabu Sana hii [emoji1787][emoji1787] Kuna Uzi kule jukwaa la GT kuhusu Bunge la Ndugai Na Huyu Dr kutoka dump university Kuna mdau alisema hakuta kuwa tofauti Kati ya Bunge la Ndugai na huyu Dr wa dump university.
Hao wote wana remote, spika hawezi kufanya tofauti na raisi anavyotaka.
 
Maadam jambo hili limefika mahakamani, ngoja mahakama itoe maamuzi ya mwisho wasije kusema wameonewa.

It is the last kicks of a dying horse.
Bado hamjaelewa tu mchezo ulivyo
Unajua kwa nn Spika amekimbilia kusema Hilo suala lipo mahakamani? Wanajua hadi kesi kuja kusikilizwa ni 2025
 
Na Msajili wa Vyama vya Siasa apitie Katiba za Vyama vya siasa nchini anone kama zina vipengele vinavyo nyima haki wanachama wao kama hicho cha CDM kinachosema, Mwanachama akikishitaki chama mahakamani kajifuta uanachama, avifanyie kazi vifutwe.
 
Ukiwahibmahakamani basi mambo yote yanasimama. Rejea kesi ya Zitto Kabwe alipofukuzwa na Chadema. Kesi ilikaa miaka miwili hadi bunge linavunjws na yeye kupata haki zake zote kama mbungr mstaafu! Hata hii inaweza kuunguruma miaka mitatu hadi 2025.

Ndio nchi ilivyo Hadi mahakama wanashiriki uonevu kisa Ni Chadema.
 
CHADEMA inaweza kufungua kesi dhidi ya wabunge 19 waliowafukuza kwenye chama chao kwamba hawawatambui, wasijitambulishe, wasitambuliwe na wasiitwe wanachama au wabunge wa CHADEMA.

Hiyo ndio kesi pekee CHADEMA wanayoweza kufungua mahakamani uamuzi ukatolewa ndani ya muda mfupi na kuna uwezekano mkubwa wa kushinda. Kesi nyingine yoyote inayohusu kutaka wabunge hao waondolewe bungeni itamalizika 2025.
 
Yaani kisheria, hata kama watakuwa wamefungua Kesi mahakamani, inabidi wake nje ya Bunge, Hadi pale shauri hilo litakapoamuliwa
Unapaswa kujua tu kuwa hao wabunge bado wanahitajika huko.
Hiyo kesi yenyewe kuja kuisha 2025.
Wangekuwa hawaitajiki wangeshaondolewa faster tu, kama spika tu aliondolewa faster tu kwa hao Wala isingeshindikana
 
Safi sana. Waende mahakamani wakashindane huko. Chadema ni chama kinachohubiri Sana HAKI na umuhimu wa kuzingatia Sheria katika maamuzi. Sasa ni Wakati wao kuishi Imani yao hiyo. Waache kulia Lia Kama last born, wakapambane Mahakamani.
 
Hii nchi ilibidi wakoloni waendelee kutawala angalau hadi mwaka 2050 pengine tungeweza kujitawala mambo madogo kama haya yanatutia aibu sana. Ndiyo maana watu wakipata upenye wanapiga hela tu vile wanajua nchi hii ni bora liende.
 
CHADEMA inaweza kufungua kesi dhidi ya wabunge 19 waliowafukuza kwenye chama chao kwamba hawawatambui, wasijitambulishe, wasitambuliwe na wasiitwe wanachama au wabunge wa CHADEMA.

Hiyo ndio kesi pekee CHADEMA wanayoweza kufungua mahakamani uamuzi ukatolewa ndani ya muda mfupi na kuna uwezekano mkubwa wa kushinda. Kesi nyingine yoyote inayohusu kutaka wabunge hao waondolewe bungeni itamalizika 2025.

Hili Jambo lilitakiwa kufanywa mwanzoni.
 
Hii ilijulikana wazi. Mihimili ya nchi inashindana kwa ujinga. Muhimili huu ukipanda kwenye level za ujinga mwingine unapambana kufanya ujinga mkubwa zaidi
Hao kina mdee bado wanahitajika huko, wangekuwa hawaitajiki ni faster tu wangetolewa. Ndugai mwenyewe faster tu alitoleea, Sasa ndio ije kushindikana hawa kina mdee
 
Leo spika wa Bunge ameelezea sakata la wabunge 19 wa viti maalum CHADEMA waliofukuzwa na chama chao. Kwa ufupi, wabunge husika wamefungua kesi mahakamani kupinga maamuzi ya baraza kuu la CHADEMA na Bunge limesema halitaweza kutangaza viti hivyo kuwa wazi kuuheshimu muhimili mwenzake wa mahakama.

=====

Spika amesema taarifa walianza kuiona kwenye mitandao ya kijamii usiku wa tarehe 11 Mei kwamba baraza kuu la CHADEMA limeazimia kukubaliana na uamuzi wa kamati kuu ya CHADEMA kuwafukuza uanachama wabunge 19 kupitia chama hicho.

Tarehe 12 Mei kwa njia ya barua pepe, wabunge hao 19 walimfahamisha spika maamuzi yaliyofikiwa na baraza kuu kwamba si halali, yako kinyume na katiba ya Tanzania na hayakuzingatia haki ya msingi ya kuwasikiliza au kuwaruhusu kujitetea.

Wabunge hao 19 wa CHADEMA wamepeleka kesi mahakama kuu ya Tanzania kupinga uamuzi huo na mwenendo mzima wa maamuzi yaliyofanyika kupitia shauri namba 16 la mwaka 2022 dhidi ya baraza la wadhamini CHADEMA, tume ya Taifa ya uchaguzi na mwanasheia mkuu wa Serikali.

Pia Spika Tulia amesema Mei 12 saa 9:30 alasiri afisa wa CHADEMA alifika bungeni aliyejitambulisha kwa jina la Meshack alifika ofisi ya spika Dar kukabidhi barua kwa spika na aliambiwa asubiri kwani wakati wa Bunge maafisa wote wanakuwa Dodoma, akaondoka baada ya kufanya mawasiliano na viongozi wake.

Tarehe hiyo hiyo Bunge lilipokea barua pepe iliyosainiwa na katibu mkuu wa CHADEMA juu ya maamuzi ya kikao cha baraza kuu juu ya kukataliwa rufaa ya wanachama 19 wa Chadema.

Spika amesema tarehe 13 Mei, barua hiyo iliwasilishwa ofisini kwa Spika kwa mkono na naibu katibu mkuu wa CHADEMA, Singo Kigaila na baadae ikapokea barua hiyohiyo kwa DHL.

Spika amesema Mamlaka ya mwisho ya utoaji haki ni Mahakama katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivyo katika nchi yenye kuongozwa na sheria na kuheshimiana kati ya mhimili mmoja na mwingine, Bunge haliwezi kuingilia mchakato wa Mahakama hivyo inalazima kusubiri mpaka mahakama itapotoa uamuzi wake kuhusu jambo hilo.

Spika amesema wabunge husika walimtaarifu mapema kabla hajapokea taarifa yoyote rasmi kutoka CHADEMA, hivyo analazimika kutotangaza nafasi za viti maalum 19 za CHADEMA ziko wazi hadi hapo mahakama itakapokamilisha kazi yake ya kutoa uamuzi.

Spika amesema endapo kutakuwa na maswali, msemaji wa jambo husika ni Spika.

Wabunge wamegonga meza
 
Back
Top Bottom