Wabunge 19 Viti Maalum CHADEMA wafungua kesi. Bunge lasema linasubiri uamuzi wa Mahakama Kuu

Wabunge 19 Viti Maalum CHADEMA wafungua kesi. Bunge lasema linasubiri uamuzi wa Mahakama Kuu

Mapambano ya riziki hayajawahi mepesi,nani anaweza kubali Mshahara wa zaidi ya milioni 10 umponyoke kirahisi🤣🤣🤣.Shida ya CDM hawapendi kuambiwa ukweli,Paskali alijaribu kuonesha upungufu wa uamuzi wa CC na Baraza kuu akashambuliwa!
Yeye Mbowe ana usafi gani wa kufukuza wasaliti wakati na yeye 2015 alikisaliti Chama kwa kumuweka Lowasa kuwa mgombea urais wakati walimuweka kwenye list of shame!🤣🤣🤣

Mbowe sio aliyewafukuzaa ni kamati kuu na baraza kuu uwe muelewa.
 
Wale wadada mnawaone sana chadema ila mmekutana na kisiki cha mpingo kipindi hiki.!
Mbona hamkujifunza kwa zitto , kuna tatizo pahala ndani ya chama, au hao wanasheria wa chama hawana msaada
 
Safi sana hatimaye tunarudi tena Mahakamani...hahahhahahaha Mahera na Ndugai kama nawaona wanavyokuja kutoa ushahidi namuoana pia askari magereza aliyemtoa yule mmoja ambaye alienda kuapa akitoke huko. Hapa ndio aibu uenda ikaipata CHADEMA ama serikali na Bunge kwa ujumla.
Mkuu wanachopinga ni kuvuliwa uanachama na si ubunge
 
Leo spika wa Bunge ameelezea sakata la wabunge 19 wa viti maalum CHADEMA waliofukuzwa na chama chao. Kwa ufupi, wabunge husika wamefungua kesi mahakamani kupinga maamuzi ya baraza kuu la CHADEMA na Bunge limesema halitaweza kutangaza viti hivyo kuwa wazi kuuheshimu muhimili mwenzake wa mahakama.

=====

Spika amesema taarifa walianza kuiona kwenye mitandao ya kijamii usiku wa tarehe 11 Mei kwamba baraza kuu la CHADEMA limeazimia kukubaliana na uamuzi wa kamati kuu ya CHADEMA kuwafukuza uanachama wabunge 19 kupitia chama hicho.

Tarehe 12 Mei kwa njia ya barua pepe, wabunge hao 19 walimfahamisha spika maamuzi yaliyofikiwa na baraza kuu kwamba si halali, yako kinyume na katiba ya Tanzania na hayakuzingatia haki ya msingi ya kuwasikiliza au kuwaruhusu kujitetea.

Wabunge hao 19 wa CHADEMA wamepeleka kesi mahakama kuu ya Tanzania kupinga uamuzi huo na mwenendo mzima wa maamuzi yaliyofanyika kupitia shauri namba 16 la mwaka 2022 dhidi ya baraza la wadhamini CHADEMA, tume ya Taifa ya uchaguzi na mwanasheia mkuu wa Serikali.

Pia Spika Tulia amesema Mei 12 saa 9:30 alasiri afisa wa CHADEMA alifika bungeni aliyejitambulisha kwa jina la Meshack alifika ofisi ya spika Dar kukabidhi barua kwa spika na aliambiwa asubiri kwani wakati wa Bunge maafisa wote wanakuwa Dodoma, akaondoka baada ya kufanya mawasiliano na viongozi wake.

Tarehe hiyo hiyo Bunge lilipokea barua pepe iliyosainiwa na katibu mkuu wa CHADEMA juu ya maamuzi ya kikao cha baraza kuu juu ya kukataliwa rufaa ya wanachama 19 wa Chadema.

Spika amesema tarehe 13 Mei, barua hiyo iliwasilishwa ofisini kwa Spika kwa mkono na naibu katibu mkuu wa CHADEMA, Singo Kigaila na baadae ikapokea barua hiyohiyo kwa DHL.

Spika amesema Mamlaka ya mwisho ya utoaji haki ni Mahakama katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivyo katika nchi yenye kuongozwa na sheria na kuheshimiana kati ya mhimili mmoja na mwingine, Bunge haliwezi kuingilia mchakato wa Mahakama hivyo inalazimika kusubiri mpaka mahakama itapotoa uamuzi wake kuhusu jambo hilo.

Spika amesema wabunge husika walimtaarifu mapema kabla hajapokea taarifa yoyote rasmi kutoka CHADEMA, hivyo analazimika kutotangaza nafasi za viti maalum 19 za CHADEMA ziko wazi hadi hapo mahakama itakapokamilisha kazi yake ya kutoa uamuzi.

Spika amesema endapo kutakuwa na maswali, msemaji wa jambo husika ni Spika.

Wabunge wamegonga meza kwa wingi kupongeza maamuzi yaliyosomwa na Spika.

Pia, Soma;

=> Kamati Kuu ya CHADEMA yawavua nyadhifa na uanachama Halima Mdee na wenzake 18 walioapishwa kuwa Wabunge wa Viti Maalum

=> Baraza Kuu la CHADEMA laridhia kufukuzwa kwa Halima Mdee na wenzake 18. Asilimia 97.6 waafikiana na maamuzi

=> Wabunge 19 kufungua kesi, vigogo CCM na ofisi ya Spika wahusishwa katika uratibu!
View attachment 2226708
Ngosha wa Voice from Within alitahadhalisha juu Kangaroo court. Now here we are at amazing status.
 
CHADEMA HAWANA MUDA WA KUHANGAIKA NA HII KESI,WALISHAMALIZA UPANDE WAO,WAKAE MPAKA 2025 NI SAWA TU.
Kwa hiyo mkipewa summons ya kwenda kujibu hoja ndivyo mtakavyoijibu mahakama?
 
Kwani yeye Spika ameambiwa na mahakama asitekeleze majukumu yake au wale akina mama ndo wamemuambia wanafungua kesi Mahakamani?
 
Maadam jambo hili limefika mahakamani, ngoja mahakama itoe maamuzi ya mwisho wasije kusema wameonewa.

It is the last kicks of a dying horse.

Maamuzi ya mahakama yataendana na utashi wa serikali.
 
Leo spika wa Bunge ameelezea sakata la wabunge 19 wa viti maalum CHADEMA waliofukuzwa na chama chao. Kwa ufupi, wabunge husika wamefungua kesi mahakamani kupinga maamuzi ya baraza kuu la CHADEMA na Bunge limesema halitaweza kutangaza viti hivyo kuwa wazi kuuheshimu muhimili mwenzake wa mahakama.
Tunaamini hii sio 'delaying tactics'.
Mag3 Pascal Mayalla

zitto junior Tindo JokaKuu Nguruvi3
 
Watu wanashangaa nini, mbona hili lilitegemewa. CHADEMA wamefanya kosa kwa maana ya timing.
Na itawagharimu, Wana option moja, compromise na Hawa akina mama.
Hili litakua kosa jingine Kama like la kumzingua Dr. Slaa.
Sijui kwanini Chadema wanaendelea kufanya makosa Kama haya.
Wenye akili walijua itaishia hapa, wamama wale wanaimage ya Chadema unaanzaje kuwazingua?!
 
Hivi haya maamuzi ya Bunge yana double standards?

Mbona wale wabunge wa CUF walipofukuzwa na Mwenyekiti wanayemtambua wao Lipumba, wabunge wale walifukuzwa mara moja na Bunge hilo??

Mbona Sofia Simba alipofukuzwa na CCM, ilitekelezwa mara moja na Bunge hilo hilo??

Iweje Hawa wabunge 19 wa viti maalum kutoka Chadema, ambapo vikao vyote 2 vya juu vya chama hicho, kwa maana ya Kamati Kuu na Baraza Kuu, vikisema wazi kuwa hao wabunge, weshafukuzwa na chama chao cha Chadema, kuwepo na kigugumizi cha kuwatimua Bungeni??

Hivi huyo Spika anapata wapi "kiburi" hicho, wakati anajua wazi kuwa Katiba yetu ya Jamhuri, inatamka wazi kuwa kila Mbunge, ni LAZIMA atokane na chama cha siasa??

Hivi huyo Spika Tulia Ackson, haoni kuwa atakuwa anavunja Katiba ya nchi, kwa kuwakumbatia wabunge, ambao hawatokani na chama chochote cha siasa nchini??

Hivi huyo Spika wa Bunge, Tulia Ackson, ambaye ana Shahada ya PhD ya sheria, haoni namna anavyodhalilisha taaluma yake ya sheria, kwa ajili tu ya kuinufaisha CCM?🥺
Huyu ni mjinga na sijui hata anafanya nini?
 
Hivi haya maamuzi ya Bunge yana double standards?

Mbona wale wabunge wa CUF walipofukuzwa na Mwenyekiti wanayemtambua wao Lipumba, wabunge wale walifukuzwa mara moja na Bunge hilo??

Mbona Sofia Simba alipofukuzwa na CCM, ilitekelezwa mara moja na Bunge hilo hilo??

Iweje Hawa wabunge 19 wa viti maalum kutoka Chadema, ambapo vikao vyote 2 vya juu vya chama hicho, kwa maana ya Kamati Kuu na Baraza Kuu, vikisema wazi kuwa hao wabunge, weshafukuzwa na chama chao cha Chadema, kuwepo na kigugumizi cha kuwatimua Bungeni??

Hivi huyo Spika anapata wapi "kiburi" hicho, wakati anajua wazi kuwa Katiba yetu ya Jamhuri, inatamka wazi kuwa kila Mbunge, ni LAZIMA atokane na chama cha siasa??

Hivi huyo Spika Tulia Ackson, haoni kuwa atakuwa anavunja Katiba ya nchi, kwa kuwakumbatia wabunge, ambao hawatokani na chama chochote cha siasa nchini??

Hivi huyo Spika wa Bunge, Tulia Ackson, ambaye ana Shahada ya PhD ya sheria, haoni namna anavyodhalilisha taaluma yake ya sheria, kwa ajili tu ya kuinufaisha CCM?[emoji3064]
huu ni wakat wa sheria.tuache tusiibgilie mihimili ya mahakaama.ova

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
 
Hamna zuio la mahakama bali ni Barua za mdee Sasa hizo Barua za mdee zinauhalali gani kutengua uamuzi wa Chadema?
 
Back
Top Bottom