kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Awamu ya Tano haikuwa awamu ya Sayansi, Sheria na Demokrasia. Ilikuwa ni awamu ya mambo yaende yatake yasitake, utake usitake. Awamu ya Tano iliamini kuwa sayansi, sheria na demokrasia ni nyenzo za kuchelewesha mambo kwa kuongeza ukiritimba.
Awamu ya Tano iliendesha nchi kama vile dereva anaendesha gari bovu limfikishe angalau sehemu salama hata kama kwa kuendelea kuliharibu zaidi na kuzidisha gharama za matengenezo baadaye kwa atakaetaka kulitengeneza.
Lazima tukubali kuwa awamu ya Tano kuna mambo imeyafanya vizuri sana, lakini Kuna ambayo imeyaharibu zaidi pia na yanaongeza gharama kwa awamu ya Sita na pengine na zijazo nyingi.
Baadhi ya mambo iliyoyaharibu zaidi ni demokrasia, utawala wa sheria, uhusiano wa kimataifa, kuhamia Dodoma, TANESCO, korosho, baadhi ya miradi mikubwa na biashara.
Awamu iliamini kuwa awamu zilizopita hazikuwa makini kwenye kila kitu hivyo ilitaka kurekebisha mapungufu ya awamu zote zilizopita kwenye awamu ya Tano. Rais wa Awamu ya tano aliamini kuwa aliletwa na Mungu kuikomboa Tanzania ili ifike kule walipo wazungu na pengine kuwapita. Kazi hii isingekuwa sawa na rahisi hata kidogo kwakuwa shida nyingi za Tanzania zinatoka nje ya Tanzania (neo colonialism, world trade market, IMF, UN, WB, EU, religions, NATO, etc.) ambazo zinautafuna uchumi na maisha yetu.
Hata kama hutaki na wala hupigani ni lazima ukanunue silaha kali na ya kisiasa kwa bei kubwa sana kwao hata kama silaha hiyo hutaitumia, maana jirani zako unaamini kuwa wanayo silaha ya aina hiyo. Maghala yetu ya silaha yamejaa silaha nyingi zilizonunuliwa kwa fedha nyingi sana ambazo zingetosha kusomesha watoto wote vyuo vikuu bure, kutoa ruzuku kwa wakulima na hata kujenga zahaniti kila kijiji. Silaha hizi zinakaa mpaka zina expire na kuagiza nyingine