Wabunge tuache kufananisha awamu ya Tano na ya Sita, tunakosea sana

Wabunge tuache kufananisha awamu ya Tano na ya Sita, tunakosea sana

Umeme (Tanesco) na kuhamia Dodoma ni kati ya project bora za awamu ya 5 na hakuna ambaye angeweza kufanya zaidi ya pale kwa sababu zifuatazo;

Umeme Tanzania ulikuwa jipu lisilotumbulika lakini JPM aliweza kadili nalo na Tanesco wakakaa sawa, umeme haukukatika hovyo hovyo kama awamu ya 4 na sasa hivi ya 6. Hapa usije na sababu zenu ooh haikufanyiwa matengenezo na blabla kibao ukweli ni kuwa mitambo yote kama hufanyi matengenezo ita knock down tu sasa kwanini haikunock kipindi cha JPM? Sababu ni kuwa matengenezo yalifanyika kwa wakati na kwa weledi wa hali ya juu. Ila awamu ya 4 na 6 umeme umekuwa na utaendelea kuwa chocho za kupigia dili ukizingatia Waziri ni wa mchongo.

Kuhamia Dodoma, hakuna Rais angekuwa na uthubutu zaidi ya JPM kuhusu Selikari kuhamia Dodoma. Mnachotafuta sasa ni justification na sympathy za kurudi Dar mlete foleni. JPM amewaachia mji mzuri kazi kwenu kufanya finishing ili mji upendeze ila msije Dar mtaongeza joto na tuliopo huku tunatosha msije Dar kama hamtaki Dodoma amieni Zanzibar.
Yeeeees! Big up! Yaani sasa hivi population inakwenda 70mil, bado watu wanatamani kulundikana kama Dar es Salaam siafu!
Umewapa ukweli
 
Awamu ya Tano haikuwa awamu ya Sayansi, Sheria na Demokrasia. Ilikuwa ni awamu ya mambo yaende yatake yasitake, utake usitake. Awamu ya Tano iliamini kuwa sayansi, sheria na demokrasia ni nyenzo za kuchelewesha mambo.

Awamu ya Tano iliendesha nchi kama vile dereva anaendesha gari bovu limfikishe sehemu salama hata kwa kuendelea kuliharibu zaidi na kuzidisha gharama za matengenezo baadaye.

Lazima tukubali kuwa awamu ya Tano kuna mambo imeyafanya vizuri sana lakini Kuna ambayo imeyaharibu zaidi na yanaongeza gharama kwa awamu ya Sita na pengine na zijazo nyingi.

Baadhi ya mambo iliyoyaharibu zaidi ni demokrasia, utawala wa sheria, uhusiano wa kimataifa, kuhamia Dodoma, TANESCO, korosho, baadhi ya miradi mikubwa na biashara.

Awamu iliamini kuwa awamu zilizopita hazikuwa makini kwenye kila kitu hivyo ilitaka kurekebisha mapungufu Yao yote kwenye awamu ya Tano. Kazi hii isingekuwa sawa na rahisi hata kidogo kwakuwa shida nyingi za Tanzania zinatoka nje ya Tanzania (neo colonialism, world trade market, IMF, UN, WB, EU, religions, etc.) ambazo zinautafuna uchumi wetu.

Hata kama hutaki lazima ukanunue silaha kali na ya kisiasa kwa bei kubwa sana kwao hata kama silaha hiyo hutaitumia, maana jirani zako wanayo silaha ya aina hiyo.
Awamu ya vichwa maji yaani miili jumba kama nyumbu ila maarifa sifuri..

Acha wafananishe maana vitu kama hivi hawakuwahi kuviona huko Vijijini kwao 👇

Screenshot_20220402-230047.png

Screenshot_20220329-162800.png

Screenshot_20220329-160231.png

Screenshot_20220328-115637.png

Screenshot_20220328-114505.png
 
Gharama kubwa iliongezeka maana Rais muda mwingi alikuwa ikulu ya Dar es Salaam na akitoka hapo anafanya kuzuga Dodoma siku chache huyooo Chato akitoka huko yupo Dar tena.

Mantiki ya Dodoma ikawa imekufa maana kila wizara ama idara ilikuwa na ofisi mbili Dodoma na Dar.
Rais kutembea kwa gari ni gharama kubwa mnomno mnomno. Mbali ya kuhitaji msafara mkubwa na ulinzi mkubwa lakini hasara kubwa ni pale wananchi wengi zaidi kuzuiwa shughuli na safari zao kupisha msafara wa Rais upite kwanza barabarani. Hii inasababisha hasa kubwa na uhai wa watu kwa njia mbalimbali kama vile mgonjwa kufia barabarani kwenye foleni y magari yaliyozuiliwa kupisha msafara wa Rais, watumishi kuzuiwa kwenye msafara kufika sehemu ya kazi kupisha msafara,
 
Awamu ya vichwa maji yaani miili jumba kama nyumbu ila maarifa sifuri..

Acha wafananishe maana vitu kama hivi hawakuwahi kuviona huko Vijijini kwao 👇

View attachment 2175035

View attachment 2175037

View attachment 2175038

View attachment 2175039

View attachment 2175040
Huwezi kuadhibu wananchi kwa kutokupeleka pesa kwa kosa la wasimamizi wa miradi ya wananchi. Badala ya kumnyonga hadharani hadi kufa kiongozi aliyechezea fedha za mradi wa wananchi unaamua kuwaadhibu wananchi wanaosubiri huduma ya mradi huo.
 
Ukiondoa awamu ya tano, hakuna awamu yeyote hapa Tanzania iliyokuwa ya maana. Hii ya sasa chini ya huyu Mama tushaanza kuona uozo wake mapemaaaaaaaaa.
 
Sababu za kuhamia Dodoma alizozieleza Nyerere enzi zake bado zina umuhimu ktk zama hizi? Jiwe alikuwa anapoteza fedha za walipa kodi tu.

Kujenga bwawa la Nyerere likalogharimu trilioni kumi na tatu kwa miaka 13 halafu akatelekeza mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia gesi anabo upo hatua nzuri, unaona alikuwa na akili yule jiwe?
Unamjua mmiliki wa hiyo gas mkuu? JPM alikua mzalendo sana, kwenye umeme hata angepakwa matope vipi, wenye akili hawawezi kuelewa. Umeme limekua tatizo kubwa nchi hi since mwaka 1992 hadi JPM alivyo ingia madarakani. Hata kama tunamchukia JPM, kwenye umeme tuweni wakweli, hakuna wa kuivunja heshima alioiweka pale TANESCO, waziri wake alivyo ondolewa tu, kila kitu kikaanza kua shagala bagala, hadi sasa hivi hakuna utulivu
 
Ukiondoa awamu ya tano, hakuna awamu yeyote hapa Tanzania iliyokuwa ya maana. Hii ya sasa chini ya huyu Mama tushaanza kuona uozo wake mapemaaaaaaaaa.
sema uwozo kwenye kipi na nini ili watu waungane au kutofautiana na wewe. Hata mwanamke wako usimwambie ana tabia mabaya sena tabia yako ya kuchelewa kurudi nyumbani siipendi, au chakula usikiite kibaya bali sema kina chumvi nyingi, hakikuiva, kina mafuta mengi au kina mawe ili mpishi akuelewe na kukusaidia wewe specific, maana kuna wateja wengine wanapenda chumvi na sukari nyingi pia.
 
Andika "mlundikano",
Nyerere aliona ni vyema shughuli za serikali ziwe katikati ya nchi!,
Uliza awamu zote hawajawahi kuginga wazo hilo!
Siku hizi hata tiketi za mabasi tunakata tukiwa kitandani kwetu tumelala. Wazo lile la umbali na katikati ya nchi lilimezwa na maendeleo ya tehama, ndiyo maana awamu zilizofuata zote ziliendelea kukutana na vipaumbele vingine. Hivi unawazaje kutumia hata shilingi moja kwenda kujenga mji mpya na kuhamisha watu wakati kuna watu hawana maji ya kunywa, umeme, na zahanati? Mtoto ambae yuko kijiji ambacho hakina maji, umeme, zahanati, walimu, madawati wala barabara anafanya mtihani mmoja wa kuhitimu shule na mwanafunzi anaeishi kwenye kijiji chenye maji, umeme, zahanati, madawati na walimu, Huu ni udhalimu mkubwa wa kiongozi, maana hata mkoloni alikuwa na afadhali.

Dhambi ya awamu ya tano ni kutumia fedha nyingi kwenye miradi ya kuhamia dodoma, mabwawa, reli na madaraja na kutumia fedha kwa miradi ya huduma za maendeleo ya wananchi kama maji, barabara, umeme, meli, nk kwenye kanda moja tu ya Tanzania.
 
Ukifikiria nje BOX ulichoeleza hapo hakina maana!,
Vyote ulivyo orodhesha mwamba alienda navyo sambamba!, mbona alitifuatifua nchi nzima kwa vimiradi ulivyotaja?
Ulizia shule ya msingi iliyokuwa jimbo la ubungo baada ya kuonekana kwenye mitandao ilijengwa siku ngapi?!!
SGR ina manufaa sana kuliko unavyofikiri!,
Watu walishauza scrapers za miundo mbinu ya reli, meli n,k, mwamba kafufua yote hayo!
 
nchi haijengwi kwa zima moto kama zile, shule kama zile ziko nyingi sana nchini, lazima kuwe na mpango mahususi wa kuzifikia zote. Ile pale ilikuwa kick baada ya vyombo vya habari kuimulika.
 
Nilikw
nchi haijengwi kwa zima moto kama zile, shule kama zile ziko nyingi sana nchini, lazima kuwe na mpango mahususi wa kuzifikia zote. Ile pale ilikuwa kick baada ya vyombo vya habari kuimulika.
Nilikwambia fikiria nje ya box! Hapo zima moto iko wapi?
Asingekatishwa safari yake watangulizi wake wangeona aibu!
 
Nilikw

Nilikwambia fikiria nje ya box! Hapo zima moto iko wapi?
Asingekatishwa safari yake watangulizi wake wangeona aibu!
kaka naona hujui mambo mengi sana. Ndugu yetu alikuwa na nia njema sema tu angeshindwa hata angekuwepo. Hazina ilikauka na madeni yalikuwa mengi sana. Wafanyabiashara walikimbia, watumishi wote wanamdai, wakandarasi wanamdai, misaada ilifungiwa, majirani zake kibiashara hawampendi, suppliers walianza kugoma, msd hakuna dawa, barrick halipi, nk. alikuwa anaelekea ukingoni
 
Wewe jamaa ni mwongo sana! Tatizo la nchi yetu ilikumbwa na wasomi waliofeli HESABU, na hii itatugharimu sana maana wengi waliingia KWENYE SIASA na ndo wanasema uongo!, Magu alijua kutafuta hela yake, sio kutembeza bakuli!, akili zako za utegemezi ndo zinakuponza!
 
Wewe jamaa ni noma sana, Mzee Magu alikuwa anatafutaje hizo hela zake? KUsamehe watuhumiwa walioko mahabusu kwa kubadilishana na fedha ndio kutafuta hela unakosema? Hivi unadhani waliyokuwa wakiyafanya akina Sabaya kupora watu fedha zao alikuwa hayajui, alikuwa hawaoni na alikuwa hayasikii? Watu walikuwa wanaporwa hela zao benki ulikuwa hujui? huko ndio kutafuta hela zake unakosema? Kaka alifika mahali anafungwa super, hata wanajeshi walikuwa wanamdai hana pesa.
 
Alizitoa bandarini mlikofunga mashine ya kimaghumashi!
Alikufungieni EFD machines na kuzuia wizi upigaji!, wale atumishi hewa na pesa za marehemu mlizotamba nazo mtaani aliziminya!
 
Alizitoa bandarini mlikofunga mashine ya kimaghumashi!
Alikufungieni EFD machines na kuzuia wizi upigaji!, wale atumishi hewa na pesa za marehemu mlizotamba nazo mtaani aliziminya!
Huko alikusanya hela ya kununua jogoo kwa laki moja na kula mahindi njiani, kick
 
Back
Top Bottom