Wabunge tuache kufananisha awamu ya Tano na ya Sita, tunakosea sana

Kila awamu iachwe ifanye inavyoona inafaa kuitendea nchi na watu wake. Mfano, Mwl. Nyerere alipoingia madarakani kwa kuwaondoa wazungu aliachana na siasa za kibepari akaendelea na ujamaa na kujitegemea, akataifisha kila kitu. Mwinyi alipoingia madarakani aliachana na Azimio la Arusha la nyerere akaendelea na ruksa, Mkapa alipoingia madarakani iliachana na mashirika ya umma akauza na kuyabinafsisha mengi kama sio yote. Kikwete alipoingia madarakani aliachana na kuuza mashirika ya umma na nyumba za serika na ada kwa shule za msingi na sekondari; na Magufuli alipokamata madaraka aliachana na safari za nje ya nchi, kilimo kwanza na big results now (BRN). Mama Samia ni nani hadi aogope kuachana na baadhi ya mambo ya Magufuli? Kwanini ashinikizwe afanye kama Magufuli? Shida hapa ni kabila, jinsia na kanda ya JPM au ni kabila, jinsia na kanda ya Mama Samia?

Awamu ya sita chapa kazi kwamujibu wa kilichoko sasa, leo sio kilichokuwa jana. Hata Ilani hii ilitengenezwa kwa size ya viatu vya JPM, awamu hii haitakuwa ya kwanza kusema hadharani kuwa ilani hii haitekelezeki, wako waliotangulia waliowahi kupewa ilani zisizotekelezeka pia, wakapaza sauti na tuliwaelewa.

Taifa linataka maji, umeme, zahanati, shule, chakula, barabara, fedha mifukoni, na usalama wao leoleo na sasa sasa, sio kesho, tumechelewa sana. Tunataka tusikie na kuona maandamano ya watu wanaodai maji, mbolea, umeme, zahanati, shule, madawati, barabara na vituo vya polisi karibu na maeneo yao lakini sio maandamano ya katiba sijui nini kwa sasa. Katiba nzuri bila usalama wa chakula, maji, umeme, afya, shule na barabara za vijijini ni upuuzi mtupu, hata wananchi hawawezi kukuunga mkono kwa hiari yao {c/o Abraham Maslow's)
 
Ungemsifia kama angeondoa nguzo za umeme, transformers na nyaya zote mbovu nchi nzima, angejenga vituo vya kukuzia umeme kila Kona ya Nchi, angesafisha na kuondoa tope kwenye mabwawa yote ya kufua umeme hapo tungekuelewa unachosema.
 
Magufuli juu...
Alichofanya JPM TANESCO ni sawa na mwenye gari kumwambia dereva wake sitaki kusikia umelala njiani kwasababu ya gari limepata pancha bila kumpa dereva pesa ya kufanyia service ya gari Wala utengenezaji wa gari ikiharibika njiani. Dereva ataamua kuliendesha gari hata kama lina pancha ili kutii amri ya boss wake huyo. Gari la hivyo litamgharimu atakaelitengeneza kununua rim mpya, mpira wa ndani na nje na uharibifu mwingine wa gear box na mafuta yote yatakuwa yameisha. .mama Samia na timu yake ya akina January inawalazimu kutengeneza gari lililoendeshwa likiwa na pancha kutoka mwanza hadi Morogoro.
 
Ni mpumbavu sana huyo jamaa!

Tanesco kuliharibika nini,
Kuhamia Dodoma kuliharibu mini

Huyu huwenda ndio Waziri wa nishati huyu
Unafahamu Kuhamia dodoma kunagharimu taifa sh ngapi?
 
Unafahamu Kuhamia dodoma kunagharimu taifa sh ngapi?
Ikiwa kuhamia Dodoma ni mpango wa serikali na ni lazima kuhamia, unadhani kuna namna yoyote ya kukwepa hizo gharama? Na unadhani ni raisi yupi ambaye kwako wewe ingelikuwa ni afadhari ahamishie makao makuu ktk mkoa wa makao makuu ya nchi?

Shida yako ni JPm alihamishia Dodoma makao makuu..? Kwako wewe ni bora angelikuwa rais mwingine na sio JPM siyo?
 
Jambo si lazima wala si kipaumbele cha watz bali cha magufuli, lakini ingefaa kuhamisha wizara chache kidogo kidogo tusingehisi maumivu.
 
Hakukuwa na mpango mahususi Wala bajeti ya kuhamia Dodoma, tulivomoa TU any how. TANESCO ilikuwa " umeme ukikatika utakiona" hivyo watu waliogopa hata kufanya services za kawaida Wala kuondoa nguzo iliyoliwa na mchwa.
Unakuwa unaliwa ndogo si bure
 
Na hakuna lililo kwama... na huo ndio utofauti wa kifikira wakati wewe unaamini bila kutenda wengine wanatenda bila kuamini.
 
Umeelezea weee ya kuachana sijui nini lakini hukusema kuwa kila awamu iliingia madarakani na ilani yake, tuambie awamu ya Samia Suluhu ilani yake iliandaliwa lini? Anatumia ilani ya awamu ya 5 au anatembea tu bila dira?? 😁😁
 
Msukuma choka mbaya. Picha inaakisi hali halisi..Hao hali yao ndo kama hivyo. Picha inajionyesha. Hata DED wa Geita alipigwa fitina tu.
 
Umeelezea weee ya kuachana sijui nini lakini hukusema kuwa kila awamu iliingia madarakani na ilani yake, tuambie awamu ya Samia Suluhu ilani yake iliandaliwa lini? Anatumia ilani ya awamu ya 5 au anatembea tu bila dira?? 😁😁
Hapa ameachana na ilani ya 2020, maana ilani hii inaongelea zaidi habari za chato na Kanda ya ziwa. Ni mwendawazimu TU anaeweza kulithi ilani kama Ile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…