Wabunge wa CHADEMA kurejea Bungeni kuanzia leo

Wabunge wa CHADEMA kurejea Bungeni kuanzia leo

CHADEMA

Political Party
Joined
Apr 13, 2013
Posts
495
Reaction score
2,540
Wabunge wote wa Chadema ambao hatimae wamehitimisha siku 14 za kujitenga (self isolation) kwa kukaa nyumbani na kutohudhuria shughuli za Bunge, vikiwemo vikao vya Bunge, ndani ya ukumbi na kamati zake katika maeneo mengine ya mhimili huo, leo Ijumaa, wanatarajiwa kurejea bungeni kuendelea na majukumu yao, baada ya kuwa na uhakika kuwa hawana maambukizi ya Ugonjwa wa COVID19.

Katibu Mkuu wa Chama, Mhe. John Mnyika (Mb) amesema kuwa Wabunge wa Chadema waliotekeleza uamuzi wa makubaliano ya Chama na wabunge, ya kujitenga kwa kutofika maeneo yote ya Bunge, walitekeleza masharti na ushauri unaotolewa na wataalam wa masuala ya afya kuhusu namna bora ya kujikinga au kupunguza maambukizi ya Virusi vya Corona, miongoni mwa watu hasa inapotokea mahali walipo zipo taarifa kuwa kati yao kuna maambukizi ya virusi hivyo vinavyosababisha Ugonjwa wa COVID19.

"Wabunge wetu wote waliotekeleza makubaliano na uamuzi wa Chama na Wabunge wa kujitenga kwa siku 14, ambayo yanatokana na maelekezo na ushauri wa wataalam wa afya, likiwemo Shirika la Afya Duniani, kwa sasa, kuanzia leo, watarejea bungeni kuendelea na shughuli za kuwawakilisha wananchi, huku wakiendelea kuzingatia tahadhari zote za kujikinga wao na kuwakinga wengine wakiwemo wabunge wengine, Watumishi wa Bunge na wananchi wetu," amesema Katibu Mkuu wa Chama, Mhe. Mnyika.

Itakumbukwa kuwa Wabunge wa Chadema walianza kutekeleza makubaliano hayo tarehe 1 Mei, mwaka huu, baada ya kuwepo kwa taarifa za maambukizi ya Ugonjwa wa COVID19 katika maeneo ya Bunge, hususan miongoni mwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hivyo siku hizo 14 zinazoelekezwa na wataalam wa afya zimemalizika jana na sasa wana uhakika na afya zao dhidi ya maambukizi ya COVID19.

Katibu Mkuu wa Chama, Mhe. Mnyika ameongeza kusema kuwa msingi wa makubaliano hayo, unatokana na maelekezo na ushauri wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ambayo yamethibitisha kuwa, kujitenga (self isolation) ni mojawapo ya njia muhimu zilizothibitishwa kisayansi katika kuzuia au kupunguza maambukizi ya Virusi vya Corona, kwa sababu inasaidia kuvunja au kupunguza muingiliano wa watu.

Imetolewa leo Ijumaa, Mei 15, 2020 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
Chadema


1589534261225.png

1589534370361.png
 
Ni Jambo jema japo kimsingi kuna mambo yameshawapita hasa hotuba za Kambi ya Upinzani kutokuwasilishwa, hili ndilo lilikuwa kosa kubwa sana na nasikitika kwanini mlilipuuza maana wananchi wamekosa uwakilishi ambao wengi wetu tunategemea kambi ya Upinzani wangekuwa wawakilishi wetu
 
unajifanya chadema wakati kufuani umekumbati nembo ya CCM
Chadema nichama Imara kuwai kutokea hapa Tanzania Tangu Dunia kuanza. Chini ya Alpha na omega Mbowe.
wewe ni msaliti ni miongoni mwa watu mnao wauza chadema asubuhi kweupee.
ila kwa sababu chadema akili haizifunguki wanakuona mwenzao na unaingia mpaka vikao vya siri vya chama.

upinzani unafeli sana kwa sababu ya mapandikizi kama wewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
unajifanya chadema wakati kufuani umekumbati nembo ya CCMwewe ni msaliti ni miongoni mwa watu mnao wauza chadema asubuhi kweupee.
ila kwa sababu chadema akili haizifunguki wanakuona mwenzao na unaingia mpaka vikao vya siri vya chama.

upinzani unafeli sana kwa sababu ya mapandikizi kama wewe

Sent using Jamii Forums mobile app


Mimi Niko ccm pia Niko chadema ndo hivyo Mbowe ndo Alpha na omega wasiasa za Upinzani hila Magufuli ni Kiongozi wa chattel tu
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Back
Top Bottom