Wabunge wa CHADEMA wakubaliana kutohudhuria tena vikao vya Bunge kutokana na janga la COVID-9, Kujiweka Karantini kwa wiki 2

Wabunge wa CHADEMA wakubaliana kutohudhuria tena vikao vya Bunge kutokana na janga la COVID-9, Kujiweka Karantini kwa wiki 2

Saccos wamekimbia Bunge lakini tulishawazoea siyo mara ya kwanza kukimbia hata bunge la katiba walikimbia lakini leo wanataka Katiba Mpya!
Ni kitendo cha uzalendo sana, wabunge kwa siku posho 300,000/= wameokoa posho ngapi?
 
Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya amesema

"Hali ya Corona ni mbaya sana, wabunge kupitia Chadema, leo tumefikia makubaliano ya kutoingia Bungeni na kila mbunge kubaki nyumbani kwake Dodoma, niwatake wananchi huko mlipo mchukue tahadhari kubwa."

Nchi inaendeshwa kwa utaratibu na sio anavyotaka kila mtu. Janga la corona lisichukuliwe kwa minajili ya kujipatia umaarufu wa kisiasa.
Wakifukuzwa ubunge na kukosa mafao wasije kulia lia baadae .
 
Nawapongeza
Mradi kila mtu kwa sehemu yake achukue hatua ili kujiokoa na kuokoa wengine. akili za kuambiwa changanya na zako.

Kuna haja ya kuendesha Bunge kwa video conference.
 
Ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni

Wabunge wa Chadema wameweka silaha chini za vita dhidi ya corona mitaani wametoroka wameenda kujifungia ndani yaani Lockdown .

Mitaani wamewaachia na kuwazitia wanachama wao ndio wapambane NATO

Kuwa wao watakuwa wanauliza tu wanachama wao kwa simu au kwa watsap kuwa vipi vita ya corona huko mitaani inaendeleaje wakiwa vyumbani!!!!

Hawa ndio hupenda kujiita makamanda huku wakivaa nguo za jeshi la mgambao!!!
Hili ni gazeti la lini?
 
Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya amesema

"Hali ya Corona ni mbaya sana, wabunge kupitia Chadema, leo tumefikia makubaliano ya kutoingia Bungeni na kila mbunge kubaki nyumbani kwake Dodoma, niwatake wananchi huko mlipo mchukue tahadhari kubwa."

Utashangaza wabunge vilaza wanaendelea kwenda bungeni ili waambukizane vizuri

kush and Wisdom
 
YEHODAYA,
Ujinga ni silaha pia,japo yakuangamiza huku ukiona.Wenye ufinyu wa tafakuri wataamini ulichoweka jukwaani.
NDATAS.jpg
 
Watanzania inabid ifikie wakati tutumie vizuri akili alizotupa mungu..kiliko kujikita kwenye mkate peke ake..
Hatua zilizochukuliwa naziunga mkono asilimia Mia moja..
Linapokuja swala la uhai wako,pesa si chochote..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili ni gazeti la lini?
Ila hawa jamaa ni wapuuzi sana,serikali inasisitiza kuepuka mikusanyiko lakini kama si lazima sana mtu abaki ndani!Yenyewe inakuja kutetea mikusanyiko,kwamba watu waende wakusanyike kupambana na Corona!
Jinga kabisa hili lileta mada,au linajua kupambana na corona ni kutoka kwenda kupigana!shame
 
Back
Top Bottom