Wabunge wa CHADEMA wakubaliana kutohudhuria tena vikao vya Bunge kutokana na janga la COVID-9, Kujiweka Karantini kwa wiki 2

Wabunge wa CHADEMA wakubaliana kutohudhuria tena vikao vya Bunge kutokana na janga la COVID-9, Kujiweka Karantini kwa wiki 2

1588351843995.png
 
Kuna vita ya Corona umeiona bungeni wewe? Kila inapoletwa hoja kuhusu Corona watu wanaongelea SITIGILAZI GOJI!! Nani kakwambia kuna vita dhidi ya Corona inapiganwa bungeni? Huko ni blaa blaa watu wanasaini posho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ujinga ule ule wa wakati wa Bunge la Katiba unajirudia tena. Chenge mwana CCM mwenzao tayari keshasema hiyo Bajeti si sahihi na ni LAZIMA itakuja kufumuliwa na kuandikwa upya mbele ya safari.

Lakini kupitisha Bajeti siyo vita iliyoko mbele yetu. Vita yetu ni dhidi ya COVID-19.
 
Mungu atende jambo kwenye hii corona ni aibu kuendelea kuongozwa na hizi Fisi zilizojaa tamaa na kushindwa kuthamini uhai wa Raia wao
 
Ujinga ule ule wa wakati wa Bunge la Katiba unajirudia tena. Chenge mwana CCM mwenzao tayari keshasema hiyo Bajeti si sahihi na ni LAZIMA itakuja kufumuliwa na kuandikwa upya mbele ya safari.

Lakini kupitisha Bajeti siyo vita iliyoko mbele yetu. Vita yetu ni dhidi ya COVID-19.
COVID-19 haitamalizwa kwa kujifungia ndani ya nyumba bali kuacha dhambi ambayo duniani kwa sasa imeshamiri sana ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile full stop!!
 
COVID-19 haitamalizwa kwa kujifungia ndani ya nyumba bali kuacha dhambi ambayo duniani kwa sasa imeshamiri sana ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile full stop!!
Khe!! Kwani COVID-19 chanzo chake ni watu kulawitiana?? Hapo Lumumba mkoje nyie watu!!
 
Kibarehe kichwani utaelewa nina maana gani.
Mara ya kwanza nilidhani ni kukosea kuandika lakini kumbe kweli hujui kuandika ama neno lenyewe hulijui. Ni "balehe" na siyo "Barehe" . Ile Ikulu ya Dodoma ilijengwa ya kazi gani kama si lazima itumiwe na Rais? Hivi Rais hana makazi yake Rasmi?
 
Sasa mkuu nimekujibu several times unataka nini sasa? Narudia tena Rais anamaeneo ya kukaa Tanzania yote siyo Dar au Dodoma tu. Ikulu unazozijua ni ceremonial tu hata hayo maeneo ya Dodoma na Dar pia ana maeneo mengi tu. Ndiyo nikasema ukibalehe kichwani utaelewa lakini kama muda wa kubalehe bado ni sawa na kumpigia gita mbuzi.
 
Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya amesema

"Hali ya Corona ni mbaya sana, wabunge kupitia Chadema, leo tumefikia makubaliano ya kutoingia Bungeni na kila mbunge kubaki nyumbani kwake Dodoma, niwatake wananchi huko mlipo mchukue tahadhari kubwa."

Wabunge wao waliotangaza kuhamia NCCR Mageuzi nao wanahusika ? Au watasubiri maelekezo kutoka kwa Mwenyekiti wao mtarajiwa?

Amandla.....
 
Just thinking aloud:

Baadhi ya wauguzi na watumishi wengine wa afya mahospitalini wakiwemo madaktari tumeambiwa wamekuwa wakikimbia vituo vyao vya kazi kuogopa kuambukizwa gonjwa hili hatari la corona. Hali hii imechangiwa zaidi kwa watumishi hawa kutopewa vifaa vya kujikinga na maambukizi haya, yaani PPE (personal protective equipment). PPE is not just a mere mask! It is more than that.

Tumeambiwa pia kuwa wabunge wa Chadema wamekimbia kituo chao cha kazi kwa kuogopa kuambukizwa gonjwa hili hatari. Tumeambiwa kuwa wabunge hawa wameenda kuji lockdown kabisa kabisa majumbani kwao hadi gonjwa hili litakapotoweka duniani. Wabunge hawa wakiwa kituoni kwao kazini hupatiwa barakoa za N95 free of charge, wakati wale wauguzi hospitalini hulazimika wengi wao (hasa wa hospitali za binafsi) kujinunulia barakoa zao za kiwango cha chini kwa bei ya sh 3,000/.

Sasa tofauti ni ipi kati ya wabunge hawa na wauguzi hawa ambao tunaamini wote wako kwenye frontline katika vita hii dhidi ya nduli Corona? Mbona wote wame-retreat siyo backline bali backhome?
 
Back
Top Bottom