Wabunge wa CHADEMA waliohudhuria Bungeni, watakiwa kujiuzulu nafasi za uongozi Bungeni

Wabunge wa CHADEMA waliohudhuria Bungeni, watakiwa kujiuzulu nafasi za uongozi Bungeni

Mhe. Mbowe amekosa mbinu. Tunahitaji chama kingine cha upinzani kuwaongoza watz wenye mawazo mbadala. Chadema is no longer relevant for the job ahead. Lets go for ACT Wazelendo and NCCR Mageuzi.
Hao wamebaki wabunge wa CHADEMA kwa jina tu.

Lwakatare kama sijakosea alishasema hatarudi bungeni, huyo Jaffary nae hivyo hovyo alisema anataka kufanya biashara zake; hivyo sioni tatizo wakiamua kufuata njia wanazotaka wao, wacha wajikusanyie mitaji ya biashara zao.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi huwa nachanganya na zangu,ndio maana nilipoona JPM anakimbiza familia kuificha kijijini nami nikaikimbiza fastaa huko kijijini,nikabaki mwenyewe mjini napambana!
Kwenye hilo la kujiongeza niko makini!
Lakini ukija kwa mbowe akili unazificha 😁😁😁
Sawa ndugu nimekuelewa
 
Mi nadhani bora kuwafukuza kabisa kabisa uwanachama japo wataendelea kuwa wabunge kwa muda uliobaki na bunge lenyewe halina tena muda litaisha, wameonyesha usaliti dakika za mwisho si vizuri kuwaacha wanaweza kuja kukiathiri chama zaidi na zaidi hapo baadae. Na hawa ndio wale wabunge ambao chama kilikuwa hakiwafahamu kwamba ni wasaliti bora kuwafukuza kabisa.

Ni vyema uchaguzi ukija Upinzani kwa kadri watakavyojitahidi wasiburure watu wasiojulikana ndani ya chama. Wakajitahidi kuleta watu makini madhubuti wasionunulika.

Nadhani hawa upande wa pili huwa kuna maneno wanawambia hawa wabunge wa upinzani naamini ni hivyo tu na sasa usipokuwa makini ni rahisi kufuata upepo "Nadhani huwambia Uchaguzi ukija jimbo lako au nafasi yako hutaipata tena ukiendelea kuwa mpinzani lakini itakuwa bwerere ukijiunga nasi"
 

Wabunge wa Chadema kwa kauli moja wamependekeza kwamba Wabunge wasaliti walioamua kuhudhuria bunge la corona na kupuuza msimamo wa chama chao wa kujitenga na bunge hilo kwa wiki mbili kama mwongozo wa WHO unavyoelekeza ili kuzuia maambukizi ya Virus hatari vya corona , wametakiwa kuachia nafasi zao za uongozi ndani ya chama ukiwemo ujumbe wa kamati kuu

Kauli hiyo imetolewa na Mnadhimu wa Kambi rasmi bungeni Mh Ester Bulaya , amesema kwamba ni aibu kwa kiongozi anayeshiriki vikao vya maamuzi vya chama kwa nafasi yake ya uongozi halafu baada ya muda mfupi anapuuza mambo aliyoshiriki kuyaamua .

Ikumbukwe kwamba Chadema haihangaiki na Ubunge wa mtu yeyote , bali wasaliti wanatakiwa kuachia nafasi za uongozi ndani ya chama , ndio maana mpaka sasa Anthony Komu na Joseph Selasini bado ni wabunge .

Mnadhimu wa Kambi rasmi bungeni Mh Ester Bulaya ameandika hivi kwenye mtandao wa Twitter.





=====

UPDATES:

DAVID Silinde, Mbunge wa Momba, Songwe kupitia Chadema ametangaza kujizulu nafasi ya katibu wa wabunge wa chama hicho kuanzia jana Jumatatu tarehe 4 Mei 2020

Silinde ambaye amekuwa mbunge kwa miaka kumi mfululizo amesema amechukua hatua hiyo ya kujiuzulu na tayari barua yake ya imemfikia Freema Mbowe.

Amesema, licha ya barua hiyo kumpelekea Mbowe, pia nakala yake ameipeleka kwa John Mnyika, Katibu Mkuu wa chama hicho.

“Nilijiuzulu jana nafasi ya Katibu wa Wabunge wa Chadema, kwa sababu nimeshindwa kusimamia maagizo ya chama ya kutohudhuria bungeni,” amesema Silinde. Hata hivyo, Silinde hajaweka wazi kama atakihama chama hicho au la.

Wabunge wengine walioingia bungeni jana ni; Joseph Selasini (Rombo), Anthony Komu (Moshi Vijijini), Peter Lijualikali (Kilombero), Jafary Michael (Moshi Mjini) na wabunge viti maalumu, Ratifa Chande, Mariam Msabaha na Sabrina Sungura.

Baada ya Silinde kuchukua uamuzi huo, wabunge wa Chadema wamemtaka Mariam Sabaha kujiuzulu nafasi ya Ujumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, kufuatia hatua yake ya kukiuka maagizo ya chama.

=======

NYONGEZA :

David Silinde hakutia nia kugombea ubunge kwenye jimbo lake la Momba kama Chadema ilivyowataka wagombea wanaotaka kugombea ubunge na udiwani kupitia chama hicho , bali ametia nia kugombea Jimbo la Tunduma ambalo linaongozwa na Mh Mwakajoka .
Hao wabunge walioamua kuhudhuria bunge wana akili sana. Haiwezekani ususie bunge kwa kuhofia corona na ututangazie kuwa utajifungia ndani siku 14, badae tukuone unadanga mjini Dar ambapo ndipo maambukizi yapo kwa kiasi kikubwa, huu ni utani. Namshukuru Makonda kwa tangazo lake mkoani Dar.
 
Lakini ukija kwa mbowe akili unazificha 😁😁😁
Sawa ndugu nimekuelewa
Ndio nasema huwa najiongeza,kama anachokifanya ni sahihi nami namuunga mkono!
Kama Rais kajiweka karantini chato,iweje nione ajabu mbunge kufanya hivyo?
 
Back
Top Bottom