Tetesi: Wabunge waanza mkakati wa kupiga kura kutokuwa na imani na Waziri Mkuu Majaliwa

Stuka

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
282
Reaction score
906
KUNA Tetesi zinaenea bungeni kuhusu wabunge kutaka kumwajibisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa baada ya kukithiri kwa vitendo viovu ndani ya Serikali na kama msimamizi mkuu wa SERIKALI hajachukua hatua zozote.

Miongoni mwa wabunge wanadai suala la Mbarali lazima litang'oka na Waziri Mkuu kutokana na manyanyaso makubwa yanayofanywa na maafisa wa Hifadhi kama yalivyoelezwa na Mbunge wa Mbarali, Mh. Mtega

Wiki ijayo baadhi ya wabunge wamejipanga kuanza kukusanya sahihi za wabunge ili kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye huku wakimlaumu Spika wa BUNGE kwa kushindwa kuusimamia mhimili huo ili serikali iwajibike.

Tusubiri tuone
 
Kama wabunge wangekuwa mchanganyiko, i.e. kutoka vyama kadhaa ingekuwa rahisi
 
70% ya wabunge hawakuchaguliwa na wananchi.Ukitambua hilo kwanza utabaini wengi hawapo pale kwaajili ya wananchi.
 
Hizo ni hadithi tu mara Spika leo waziri mkuu,2025 hao watakao saini watakuwa na wakati mgumu,wengi wao walibebwa labda waende upinzani.
 
Wiki ijayo baadhi ya wabunge wamejipanga kuanza kukusanya sahihi za wabunge ili kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye huku wakimlaumu Spika wa BUNGE kwa kushindwa kuusimamia mhimili huo ili serikali iwajibike.
Huyo binti ni actress tu
 
Chama kipi? CCM?
 


Hilo halipo, kama ni tetesi zitakuwa za uongo 100%
 
Ila Pm hata mimi simwelewagi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…