Tetesi: Wabunge waanza mkakati wa kupiga kura kutokuwa na imani na Waziri Mkuu Majaliwa

Tetesi: Wabunge waanza mkakati wa kupiga kura kutokuwa na imani na Waziri Mkuu Majaliwa

KUNA Tetesi zinaenea bungeni kuhusu wabunge kutaka kumwajibisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa baada ya kukithiri kwa vitendo viovu ndani ya Serikali na kama msimamizi mkuu wa SERIKALI hajachukua hatua zozote.

Miongoni mwa wabunge wanadai suala la Mbarali lazima litang'oka na Waziri Mkuu kutokana na manyanyaso makubwa yanayofanywa na maafisa wa Hifadhi kama yalivyoelezwa na Mbunge wa Mbarali, Mh. Mtega

Wiki ijayo baadhi ya wabunge wamejipanga kuanza kukusanya sahihi za wabunge ili kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye huku wakimlaumu Spika wa BUNGE kwa kushindwa kuusimamia mhimili huo ili serikali iwajibike.

Tusubiri tuone
Kwa bunge la Mwendazake nani ana uwezo huo?
 
Kwa hiyo raisi amewateua wazembe alafu hao wazembe wanafanya madudu raisi anawangalia tu awafanyi chocho Kisha lawama zinaenda Kwa waziri mkuu hi nchi Ina vilaza wengi sana
 
Wiki ijayo baadhi ya wabunge wamejipanga kuanza kukusanya sahihi za wabunge ili kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye huku wakimlaumu Spika wa
Hiyo itakuwa "mutiny" dhidi ya Mama. Jambo ambalo litawapa shida wakusanya saini.
 
Back
Top Bottom