Wabunge walihongwa na DP World; ushahidi huu hapa!

Wabunge walihongwa na DP World; ushahidi huu hapa!

Unamuona Hayati Magufuli hapo au ni lawama kwa waliouza nchi kwa wajomba?

20141018_MAP004_0.jpg
 
Naingia kwenye mada moja kwa moja nisiwachoshe na maneno mengi. Ukimsikiliza huyu mbunge kwa umakini utakubaliana nami pasi na shaka kwamba wabunge wa CCM walihongwa na kampuni ya DP World ili kuwauzia nchi. Inauma sana. Kumbe mkataba ulisainiwa tangu mwaka jana, sasa hawa wezi wanatuchora tu jinsi tunavyolalamika mitandaoni.

View attachment 2668819
CCM ni Yuda Eskarioti, wametusaliti mchana kweupe!
Wakati watanzania tunapambana kila siku kujikusuru na umaskini, wabunge hawa wa CCM wamegeuka kuwa Yuda Eskarioti aliyemuuza Yesu kwa vipande 30 vya fedha. Uroho wa mali na uchumia tumbo ndivyo vinavyopewa kipaumbele kuliko utu na uzalendo kwa taifa. Hata kama wakituuza kwa hizo fedha kidogo wanadhani wataishi milele? Hawa wapuuzi wamelaaniwa sio bure.

View attachment 2668825
Magufuli alaumiwe 100%
Haya yote yamesababishwa na Magufuli pale alipoamua kuchezea uchaguzi wa 2020. Ndio. Kama wabunge wa upinzani wangekuwemo bungeni huu upumbavu wa kuwauza watanzania kwa mabeberu wa kiarabu usingefanyika. Huko aliko Mungu anamuona. Kama kaburi lake lingekuwa halilindwi 24/7 tungeenda kulipiga fimbo.

CCM ni ukoo wa panya
CCM ni ukoo wa panya—babu mwizi, baba mwizi, watoto wezi, wajukuu wezi, vitukuu wezi, vilembwe wezi na vining’ina wezi! Ukoo huu wa panya walikuwa wanasafiri katika boti la muhogo, lakini kwa sababu ya uroho wao, walianza kulitafuna boti! Kilichofuata ni ukoo mzima wa kizazi cha panya kuzama na kuangamia.

Ukoo huu wa panya badala ya kuangamia peke yao wameona wagugune mtumbwi ili tuzame wote. Kuchumiia tumbo kwao limekuwa janga la taifa. Ni afadhali nchi hii iuzwe tugawene hela kila mmoja atafute nchi ya kwenda kuishi.

Hii nchi sio mahali pa kuishi tena; imegeuka kuwa shamba la wanyama. Katika shamba la wanyama inasemekana wanyama wote ni sawa lakini baadhi yao ni sawa kuliko wengine. Katika nchi hii ukoo wa panya (CCM) ni sawa kuliko wengine. Ndio maana kila kukicha wanauza rasilimali za taifa kwa bei ya kutupa bila soni.
View attachment 2668810
Muda sio mrefu ujao zinaanza kusainiwa hizo HGAs na biashara inakwenda kuanza. Hivyo endeleeni tu na haya majungu yenu wakati nchi inakwenda kuongeza wigo wa mapato.

Pigeni tu kelele hizi hazina msaada wowote ni kama kupaka rangi upepo. Na mtakuwa wa kwanza kufaidika na mapato ya bandari yakiwa yanaongezeka. Mtakuwa wa kwanza kufaidika na matibabu bure siku zijazo, mtakuwa wa kwanza kupiga makofi wakati watoto wenu wakisoma mpaka shahada za pili kwa malipo ya pesa zitakazotokana na bandari hii hii leo hii mnayoiletea maneno ya fitina.
 
WALIVYOFUNGUA GETI LA KUJINUFAISHA KWA TAKRIMA, RUSHWA, KINGA MAALUMU N.K

Sasa tunaelewa kwanini waliondoa baadhi ya vifungu hivi na pia kutunga sheria za kujikinga wakati wakiwa madarakani

Ibara 28 za Tume ya Warioba zilizoondolewa​

updated on Machi 11, 2021

1687938752983.png

Jaji Warioba.PICHA|MAKTABA

Muktasari:​

  • Ibara ya 15 iliyokuwamo katika Rasimu ya Warioba ilisema: “Kiongozi wa umma wakati anapotekeleza shughuli za kiserikali, akipewa zawadi, zawadi hiyo itakuwa ni mali ya Jamhuri ya Muungano na ilitaka Bunge kutunga sheria itakayosimamia, pamoja na mambo mengine, thamani, kiwango, aina na uhifadhi wa zawadi kwa Jamhuri ya Muungano. Mbali na ibara hiyo, pia Ibara ya 16 iliyohusu ufunguaji akaunti nje ya nchi, imeondolewa.
Dar/Dodoma.

Rasimu ya Katiba inayopendekezwa iliyowasilishwa bungeni juzi, imeondoa Ibara 28 zikiwamo zinazowataka viongozi wa umma kutopokea zawadi kwa manufaa yao binafsi wala kufungua akaunti ya benki nje ya nchi pasipo sababu maalumu, Mwananchi limebaini.

Ibara ya 15 iliyokuwamo katika Rasimu ya Warioba ilisema: “Kiongozi wa umma wakati anapotekeleza shughuli za kiserikali, akipewa zawadi, zawadi hiyo itakuwa ni mali ya Jamhuri ya Muungano na ilitaka Bunge kutunga sheria itakayosimamia, pamoja na mambo mengine, thamani, kiwango, aina na uhifadhi wa zawadi kwa Jamhuri ya Muungano.

Mbali na ibara hiyo, pia Ibara ya 16 iliyohusu ufunguaji akaunti nje ya nchi, imeondolewa.

Ibara nyingine zilizo ondolewa ni pamoja na ya 17 iliyopendekeza uwazi wa mali ikimtaka kiongozi wa umma kutangaza thamani ya mali na madeni yake mara tu baada ya kupata uongozi.

Pia Ibara ya 129 iliyokuwa inawaruhusu wananchi kumvua madaraka mbunge ambaye atashindwa kuwasilisha au kutetea kwa dhati hoja zinazotokana na kero za wapigakura wake au ataacha kuishi au kuhamisha makazi yake kutoka eneo la jimbo la uchaguzi kwa zaidi ya miezi sita bila sababu za msingi imeondolewa.

Ibara 28 zilizoondolewa
15. (1)
Kiongozi wa umma wakati anapotekeleza shughuli za kiserikali, akipewa zawadi, itakuwa ni mali ya Jamhuri ya Muungano na ataiwasilisha kwa Katibu Mkuu Kiongozi kupitia kwa katibu mkuu wa wizara au kiongozi wa taasisi ya Serikali inayohusika, akiainisha:
(a) aina ya zawadi;
(b) thamani ya zawadi;
(c) sababu ya kupewa zawadi; na
(d) mtu au mamlaka iliyotoa zawadi hiyo.
(2) Neno “zawadi” kama lilivyotumika katika ibara hii linajumuisha kitu chochote chenye thamani atakacho pewa kiongozi wa umma katika utekelezaji wa shughuli za umma.

(3) Bunge litatunga sheria itakayosimamia, pamoja na mambo mengine, thamani, kiwango, aina na uhifadhi wa zawadi kwa Jamhuri ya Muungano.

16. Kiongozi wa umma-
(a)
Hatafungua au kumiliki akaunti ya benki nje ya Jamhuri ya Muungano isipokuwa tu kwa namna ambayo sheria za nchi zinaruhusu; na
(b) hataomba au kupokea mkopo au faida yoyote kwa namna au mazingira ambayo yanashusha hadhi au heshima ya utumishi wa umma.

17.-(1) Kiongozi wa umma atalazimika kutangaza na kuwasilisha, ndani ya siku thelathini baada ya kupata uongozi na baada ya kuacha uongozi, mali na thamani yake na madeni yake katika Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji.

(2) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (1), Kiongozi wa umma atalazimika kutangaza na kuwasilisha taarifa ya mali na madeni:
(a) yake binafsi;
(b) ya mwenza wake wa ndoa; na
(c) ya watoto wake walio chini ya umri wa miaka kumi na nane, mara moja kila mwaka kwa Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji.

(3) Bunge litatunga sheria itakayosimamia, pamoja na mambo mengine:
(a) ngazi au orodha ya viongozi wa umma wanaopaswa kutangaza mali na madeni yao; na
(b) utaratibu wa kuwasilisha taarifa ya mali na madeni kwa Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji kwa mujibu wa Katiba hii.

18.-(1) Kiongozi wa umma hatashiriki katika kufanya uamuzi wa jambo au shughuli yoyote ambayo ana masilahi nayo yeye binafsi, mwenza wake, mtoto wake, jamaa yake, rafiki au mtu yeyote wa karibu.
(2) Kiongozi wa umma hatazungumzia kitu chochote katika Baraza la Mawaziri, Bunge, Kamati au chombo kingine chochote rasmi ambacho ana masilahi nacho ya moja kwa moja au vinginevyo, isipokuwa tu kama atatoa taarifa ya mgongano huo wa masilahi katika chombo hicho.

(3) Itakuwa ni marufuku kwa kiongozi wa umma kushiriki katika uamuzi unaohusu kuongeza au kuboresha masilahi kwa namna yoyote ile yanayohusu wadhifa alionao na endapo atashiriki, basi masharti hayo mapya yataanza kutumika kwa kiongozi wa umma atakayekuja baada ya kiongozi husika kuondoka au kumaliza muda wa kukaa katika nafasi ya madaraka iliyompatia fursa ya kushiriki katika kuamua masilahi husika.

(4) Masharti ya ibara ndogo ya (3), hayatamhusu kiongozi wa umma ambaye kutokana na asili ya nafasi ya madaraka au aina ya kazi zake anapaswa kushiriki katika upangaji wa mishahara au maslahi mengine ya watumishi wa umma.

(5) Kiongozi wa umma hataruhusiwa kushika nafasi za madaraka zaidi ya moja au kutumikia mihimili ya dola zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja.

19. Kiongozi wa umma hataruhusiwa kutumia au kuruhusu kutumika kwa mali yoyote ya umma, zikiwemo zilizokodishwa kwa Serikali, kwa madhumuni ya kujipatia yeye binafsi au kumpatia mtu mwingine manufaa yoyote.

20.-(1) Bunge litatunga sheria itakayosimamia, pamoja na mambo mengine:
(a) utaratibu wa utwaaji wa mali za viongozi wa umma zilizopatikana kwa kukiuka sheria;
(b) utaratibu wa kumwajibisha kiongozi wa umma aliyekiuka maadili na Miiko ya Uongozi; na
(c) uanzishaji wa mitalaa inayohusu Katiba, maadili na uraia, shuleni na vyuoni.
(2) Masharti yaliyoainishwa katika sehemu hii ya Sura ya Tatu yatatumika pia kwa watumishi wa umma baada ya kufanyiwa marekebisho stahiki.

63. Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano na kwa ajili ya mgawanyo wa madaraka juu ya shughuli hizo baina ya vyombo vilivyotajwa katika Ibara ya 61, Serikali ya Jamhuri ya Muungano itakuwa na mamlaka juu ya mambo ya Muungano kama yalivyoorodheshwa katika Nyongeza ya Katiba hii. Nchi Washirika.

Source : gazeti la mwananchi
 
Bandiko hilo juu na jinsi vifungu vilivyonyofolewa na kuainishwa ktk comment #90 kwa ukubwa linazua shaka kuwa walioenda Dubai kwa wingi ule wanaweza kuwa wamehongwa hata kwa kuchomekwa ktk safari wasizostahili, zawadi ndogo ya takrima, malazi, airline ticket, posho na shopping ndogondogo ambazo walitakiwa wazijaze katika fomu ya maadili ya viongozi

1687939692952.png
 
Sasa Nyumbu hapo nyuma si walikuwepo bungeni je kuna mikataba ilijadiliwa na kusimamishwa na hao nyumbu? hata nyumbu wangekuwepo bungeni nao wangeimba mapambio tu kama akina Musukuma, nani asiyependa rushwa nchi hii?
 
Ulipomtaja Magufuli na wewe unaingia kwenye kulaumiwa kwa sababu kuhongwa fedha kwa wabunge kunauhusiano gani na Magufuli?
 
Ulipomtaja Magufuli na wewe unaingia kwenye kulaumiwa kwa sababu kuhongwa fedha kwa wabunge kunauhusiano gani na Magufuli?
Magufuli ndiye alicheza rafu ya uchaguzi wa mwaka 2020 ili kuua upinzani. Wabunge wa upinzani wangekuwa bungeni, wahongaji wasingethubutu kutoa mlungula. Umeona uhusiano wa kuhongwa unavyomgusa Magufuli?
 
Sasa Nyumbu hapo nyuma si walikuwepo bungeni je kuna mikataba ilijadiliwa na kusimamishwa na hao nyumbu? hata nyumbu wangekuwepo bungeni nao wangeimba mapambio tu kama akina Musukuma, nani asiyependa rushwa nchi hii?
Kwani hukuwahi kuwaona wapinzani wakitoka nje ya bunge pale wanapoona uchache wao hauwasaidii kukwamisha hoja za maCCM? Tatizo ni wewe na wananchi wengine kuwapigia kura mafisadi ya CCM badala ya kuwapigia wapinzani ili wawe wengi bungeni watusaidie kupinga hoja za mafisi wa CCM.
 
Mungu atatushangaa sana endapo hawa wakina Msukuma.and Company watarudi Bungeni Ingawa najua asilimia 90 watarudi but Mungu anatushangaa sana kwa hili.

Hili sakata lilikuwa ni moja ya sehemu ya kudili na hawa wahuni wa Bungeni, ambao wao masilahi yao binafisi na ya Mwenyekiti wao ndio kipa umbele chao.

Hawa najua watarudi, ila Mungu hata jinsi ya kuja kutusaidia tena anashindwa sasa, make hatuwezi jisaidia wenyewe.

Na kinacho wapa nguvu ni hicho kwamba watarudi Bungeni tena na tena.

Je hatuna namna ya kuhakikisha hawarudi tena Bungeni?
 
Mungu atatushangaa sana endapo hawa wakina Msukuma.and Company watarudi Bungeni Ingawa najua asilimia 90 watarudi but Mungu anatushangaa sana kwa hili.

Hili sakata lilikuwa ni moja ya sehemu ya kudili na hawa wahuni wa Bungeni, ambao wao masilahi yao binafisi na ya Mwenyekiti wao ndio kipa umbele chao.

Hawa najua watarudi, ila Mungu hata jinsi ya kuja kutusaidia tena anashindwa sasa, make hatuwezi jisaidia wenyewe.

Na kinacho wapa nguvu ni hicho kwamba watarudi Bungeni tena na tena.

Je hatuna namna ya kuhakikisha hawarudi tena Bungeni?
Hao kurudi labda utawala utuletee mambo ya nireteeeenii gwajimaaaa nireteeeenii gwajimaaaa nireteeeenii gwajimaaaa!! Bila ivo hawatoboi 2025!!
 
Mungu atatushangaa sana endapo hawa wakina Msukuma.and Company watarudi Bungeni Ingawa najua asilimia 90 watarudi but Mungu anatushangaa sana kwa hili.

Hili sakata lilikuwa ni moja ya sehemu ya kudili na hawa wahuni wa Bungeni, ambao wao masilahi yao binafisi na ya Mwenyekiti wao ndio kipa umbele chao.

Hawa najua watarudi, ila Mungu hata jinsi ya kuja kutusaidia tena anashindwa sasa, make hatuwezi jisaidia wenyewe.

Na kinacho wapa nguvu ni hicho kwamba watarudi Bungeni tena na tena.

Je hatuna namna ya kuhakikisha hawarudi tena Bungeni?
Wakati wamatokeo ya uchaguzi kwa asilimia zile zile ndoziwabakishe majumbani mwao,,
 
Mtawarudisha tu,wabongo walivyo na njaa na watu wa kusahau,
Mtapigwa na show za mondi zuchu konde +wasani bongo movie
Mtapewa kanga,ubwabwa,vitenge na buku10 kwishneyyy

Ova
 
Unadhani ukibadilisha Chupa bila ku-deal na kilichomo ndani ya Chupa itabadilisha maji kuwa mvinyo ?!!!!

 
Nchi haijauzwa

CCM wataendelea tawala sababu Watanzania bado ni wajinga
 
Mijitu ni MIPUMBAVU mnoo,kwani 2020 nyie wananchi mliwapeleka bungeni hao wabunge? CCM hatutegemei kura zenu kushinda uchaguzi.
 
Mungu atatushangaa sana endapo hawa wakina Msukuma.and Company watarudi Bungeni Ingawa najua asilimia 90 watarudi but Mungu anatushangaa sana kwa hili.

Hili sakata lilikuwa ni moja ya sehemu ya kudili na hawa wahuni wa Bungeni, ambao wao masilahi yao binafisi na ya Mwenyekiti wao ndio kipa umbele chao.

Hawa najua watarudi, ila Mungu hata jinsi ya kuja kutusaidia tena anashindwa sasa, make hatuwezi jisaidia wenyewe.

Na kinacho wapa nguvu ni hicho kwamba watarudi Bungeni tena na tena.

Je hatuna namna ya kuhakikisha hawarudi tena Bungeni?
Njia ni kuhakikisha hawachezei uchaguzi kama ilivyotokea 2020 Magufuli alipochezea uchaguzi. Kama mle bungeni tungekuwa na wabunge wa upinzani angalau 50 tu kusingekuwa na ufisadi wa kutisha kama huu tunaouona leo.
 
Back
Top Bottom