Wabunge wanne - Anthony Komu, Joseph Selasini, David Silinde na Wilfred Lwakatare wafutwa uanachama wa CHADEMA

Wabunge wanne - Anthony Komu, Joseph Selasini, David Silinde na Wilfred Lwakatare wafutwa uanachama wa CHADEMA

Nasikitika kuona UPINZANI hasa chama kikuu CHADEMA kikipita katika wakati mgumu kiasi hiki.

Jambo pekee ambalo watu wengi hawalifahamu ni kwamba Udhaifu wa upinzani (vyama vya ukosoaji) ndiyo Udhaifu wa Serikali.

Kingine ambacho nakiona ni hofu ya CHADEMA dhidi ya ulaghai unaoweza kufanyika kwa wabunge hao waliokubali kuwasaliti wenzao pamoja na maagizo ya Chama.

Fikra zangu zinanishawishi kuwa endapo wangevuta subira kidogo wangeweza kupata mengi zaidi kuliko hivi sasa, japo ni ngumu sana kuwa na muda mrefu wa uvumilivu hasa katika kipindi hiki ambacho hujuma za kisiasa zimekithiri pande zote na wakati ambao kila upande ukitafuta namna ya kujiimarisha kisiasa.

Aidha Intelijensia ya Chama imeshapata infos za kutosha.

Mungu atuvushe salama katika janga hili la CORONA na kuwapa hekima wanaotakiwa kuwasemea/ kuwasaidia Watanzania walio wengi na wasijue cha kufanya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nasikitika kuona UPINZANI hasa chama kikuu CHADEMA kikipita katika wakati mgumu kiasi hiki.

Jambo pekee ambalo watu wengi hawalifahamu ni kwamba Udhaifu wa upinzani (vyama vya ukosoaji) ndiyo Udhaifu wa Serikali.

Kingine ambacho nakiona ni hofu ya CHADEMA dhidi ya ulaghai unaoweza kufanyika kwa wabunge hao waliokubali kuwasaliti wenzao pamoja na maagizo ya Chama. Fikra zangu zinanishawishi kuwa endapo wangevuta subira kidogo wangeweza kupata mengi zaidi kuliko hivi sasa, japo ni ngumu sana kuwa na muda mrefu wa uvumilivu hasa katika kipindi hiki ambacho hujuma za kisiasa zimekithiri pande zote na wakati ambao kila upande ukitafuta namna ya kujiimarisha kisiasa.
Aidha Intelijensia ya Chama imeshapata infos za kutosha.

Mungu atuvushe salama katika janga hili la CORONA na kuwapa hekima wanaotakiwa kuwasemea/ kuwasaidia Watanzania walio wengi na wasijue cha kufanya

Sent using Jamii Forums mobile app
Intelijensia inayogundua mambo baada ya kuharibika hiyo ni Intelijensia butu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka 1995 Mbowe alikuwa Marangu anakunywa Mbege??? Wakati mwingine huwa nawasikitikia sana kwa yale mnayoyaandika humu?

Mbowe was elected to the National Assembly in 2000 representing Hai Constituency. He won 64.5% of the vote, which was the highest percentage of votes won among constituencies with opposition MP's
Unafikiri ukiandika kwa lugha ya mabeberu ndiyo utatufanya tukuamini kwamba si mbumbumbu!!
 
Acha kujidanganya mwenyw hukumbuki kuna watu walikwenda kuungama Ikulu kwa bwana yule?au ulikuwa mtt?
Sasa Boss, hapo ni nani atakayetumia Busara?
Ni aibu kwamba Maelezo ya wote waliohama chama yanaonekana yako sahihi. Kwamba ukitaka kubaki CHADEMA, lazima utii amri za Mbowe. Hii ni hali wanayoiga toka CCM lakini, hawajitambui. CCM ina legacy ya chama kimoja na chama kushika hatamu. Vyama vya mageuzi kama CHADEMA walistahili kuwa watu wenye sayansi ya siasa na uwezo mkubwa wa ufahamu.

Kwa mtindo huu siyo tena jambo la kujiuliza eti waliohama walinunuliwa au hapana! Vijana walidhani ni chama kinachowafaa kwa mageuzi kumbe wapi! Utafuata mageuzi wakati kuna mtu ambaye hapingwi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unafikiri ukiandika kwa lugha ya mabeberu ndiyo utatufanya tukuamini kwamba si mbumbumbu!!
Sijaandika mimi ndugu yangu bali nimenukuu toka kwingine na kuweka hapa JF (Copy &Paste). Samahani isije ikaonekana nimefanya "plagiarism" kwenye maandishi ya watu!!
 
Hapa si ndiyo yale ya kutaka NDIYO MZEE!
Tofauti gani na CCM?
Hivi ndio kuenzi demokrasia?
Ndio Mzee? Hivi Kiongozi Mkuu wa Kambi ya Upinzani ni Mzee? Halafu wanawezaje kuchagua mtu mwingine na kumwita Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bila ya baraka za chama??

Kati ya wote aliyekuwa ni mtu wa kudharau chama kuliko wengine ni Silinde! Jamaa hata hivyo wamemvumilia sana!!
 
Wewe jamaa tangu magufail kaingia kusikomfaa, akili zako zimehamia chini. Acheni ushabiki wa kibwege kama wa gwajiboy.

Dah; nilikuwa sijakusikia siku nyingi sana, takriban miaka kumi sasa.

Sasa ndugu yangu wewe inaonekana kuwa tangu Magufuli alipoingia madarakani na Lowasa (aliyekuwa anaimbwa kila siku kama fisadi wa Richmond) akaletwa CHADEMA na kupewa bendera ya kuwania uraisi kwa amri ya mwenyekiti bila kupitia taratibu za chama,

ni wazi kuwa na wewe akili yako ilitumbukia chooni (kwa vile umenitukana) na kuvurugikiwa kiasi cha kutokuona mapungufu hayo. Sasa hivi unaongea ama ushabiki usioona mbali kutokana na akili kuvurugikiwa au kwa kumchukia Magufuli,

ambayo ndiyo sera ya CHADEMA sasa. Unfortunately hakuna ninaloweza kukusaidia kati hayo mawili. Yaani wale wabunge wa CHADEMA wenywe ambao ni nguzo ya uongozi wa chama nao wanaona mapungufu hayo na kujiondoka eti wewe hulioni
 
https://millardayo.com/wabunge-wanne-chadema-watimuliwa-wametoa-kashafa-kwa-chama-video/#respond

maxresdefault-2-3-660x400.jpg


Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetanganza kuwafukuza uanachama Mbunge wa Rombo Joseph Selasini na Mbunge wa Moshi Vijijini Anthony Komu kwa kuwa wamepoteza sifa ya kuwa wanachama wa chama hicho.

“Kamati Kuu CHADEMA imeazimia Wabunge Anthony Komu na Joseph Selasini pamoja na kuwa wamejipotezea sifa ya uanachama wa CHADEMA, wameendelea kutoka kauli za kejeli, kashfa na kukiuka maagizo ya Chama, hivyo Chama kimeazimia kuwafukuza uanachama” -John Mnyika, Katibu Mkuu CHADEMA

“Mbunge David Silinde na Wilfred Rwakatare sio tu wamekiuka agizo la Chama bali wamekuwa wakijitokeza kwenye vyombo vya habari kutoa maneno ya kashfa na kejeli dhidi ya maagizo ya Chama na Viongozi wa Chama, Kamati Kuu CHADEMA imefikia uamuzi wa kuwafuta uanachama”- MNYIKA

“Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA, Mariamu Msabaha, ameshiriki kukiuka maagizo ya Chama, ilitakiwa awe mfano na kwakuwa amekwenda kinyume, amevuliwa nafasi zake zote ndani ya Chama na kubaki na Ubunge na atatakiwa ajieleze kwanini asichukuliwe hatua zaidi kwa kukiuka maagizo”-MNYIKA

“Kuhusu Wabunge wengine ambao wamekwena kinyume na maagizo ya Chama lakini hawajaonesha utovu wa nidhamu kwa kutoa kashfa kwa Chama, watatakiwa wajieleze kwanini wasichukuliwe hatua zaidi kwa kukiuka maagizo” -MNYIKA
 
Wa kuwaachia wapo wengi tu ndio maana kamsogeza mnyika ukatibu na Lissu makamu yeyote kati ya hao anaweza kuibeba CHADEMA kwa miaka 10 ijayo.

Zitto alikua insubordinate, chama kilimvumilia sana ila kiukweli alipata alichostahili. Ilifika kipindi zitto anakejeli chama wazi wazi utadhani yye hayupo CHADEMA. Mara chama kikaguliwe na CAG utadhani yye sio Naibu KM wa kutekeleza hilo, mara mitambo ya dowans iletwe ilihali chama kiliweka msimamo wa kupinga!!

Kiufupi Zitto alishakua mkubwa kuliko chama ilikua either wampe uenyekiti au autafute kwingine. Angekua loyal kma Mnyika au Lisu leo hii angekua KUB
Watakosa 340,000 x 19 = 6,460,000 kila mmoja, lakini kuna chama kipya cha spika watabaki huko
 
chadema nawapata sana nikiwa huku botiswana, nimependa maamzi yenu, niko pamoja nanyie katika kujenga nidhamu chaman!
 
Back
Top Bottom