Mtumishi wa umma hazuiliwi kuwa mwanacha wa chama cha siasa, ila anazuiliwa kuwa kiongozi katika chama cha siasa lakini pia hatakiwi kufanya siasa katika sehemu yake ya kazi!.Tume ya utumishi wa umma na ile ya utawala bora watuambie kama alichokifanya Kitila Mkumbo ni sahihi kwa mtumishi wa umma kuvaa sare za chama na kujitangaza hadharani kujihusisha na siasa za chama hicho huku bado ni Katibu Mkuu wa wizara. Hii nchi tuliikuta ikiwa na kanuni na taratibu na miiko ya utumishi wa umma, tusiharibu.