Wabunge wapigwa darasa kuhusu nishati safi na salama ya kupikia. Kila mbunge kupewa mitungi 100 ya gesi

Kugawa hela na mitungi kwa wabunge sio rushwaa?? au wee unaona nn??
Hilo la hela huwezi thibitisha kwamba ni Rushwa Kwa sababu ni pesa ya semina na sio kweli kwamba unaweza thibitisha kwamba ni milioni 10?
Issue ya Mitungi ya gas alianza kugawa Makamba kitambo sana kama njia ya kuhimiza ajenda yake ya Nishati safi na Sasa Serikali imeunda sera ya Nishati safi na kikosi kazi.

Mwisho yaani najiukiza Kwa kipi Cha ajabu huko Wizara ya Nishati Hadi ihitajike Rushwa kuoutisha Bajeti? Huu ni uzushi usio na msingi.
 
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo, tarehe 27 Mei, 2023 wamepata nafasi ya kujifunza kuhusu nishati safi ya kupikia pamoja na kupitishwa kwenye ...
it's just a coincidence ya kucoincidencesika karibu na bajeti yake!.
P
 
Hilo la hela huwezi thibitisha kwamba ni Rushwa Kwa sababu ni pesa ya semina na sio kweli kwamba unaweza thibitisha kwamba ni milioni 10...
Kama hakuna cha ajabu kwanini atoe rushwa ya fedha na majiko? Kama ni programu ya Serikali kwanini haikutolewa miezi 6 iliyopita ndio itolewe leo kesho ni bajeti yake? hata kama hujasoma utaona picha
 
Hakuna rushwa hapo. Ni mjinga tu akayeiona hiyo kuwa ni rushwa.
 
Wale wa majungu endeleeni wenzenu wako site wanachapa kazi
 
Kila mbuzi ale kwa urefu wa kam gesi kwenye mitungi ni nani

Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo, tarehe 27 Mei, 2023 wamepata nafasi ya kujifunza kuhusu nishati safi ya kupikia pamoja...
Gharama za kujaza mitungi ya gesi pindi inapoisha nani atawapa kuendeleza matumizi ya nishati safi ?Nishati ya gesi haiwezi kuivisha ubwabwa vizuri bila kuathiri uhalisia wa chakula chenyewe na kijijini ni ngumu kukubalika
 
Waziri wa Nishati, Januari Makamba anatuhumiwa kuhonga wabunge wote milioni 10 kila mbunge pamoja na kuwapa rushwa ya majiko 300 ya gesi kwa kila mbunge kama shinikizo la kupitisha bajeti ya Wizara ya Nishati wiki wiki hii.
"Ukitaka kula lazima uliwe" Kikwete
 
Huenda jicho likaona lakini moyo na ubongo vikawa likizo,
siasa kama pulizo,
shingo yake kidole ndio kishikizo,

Dah! Siasa za mbogo raha sana. Wabunge wanapewa semina za nishati mbadala wa mkaa na kuni?!
 
January Makamba alitoa wapi pesa ya kugawa mitungi ya gesi mia moja kwa kila mbunge?!

Bajeti ya kununua hiyo mitungi ilipitishwa lini na Bunge kama pesa ni ya wizara?!

Kwa nini Tulia kalitolea ufafanuzi jambo hilo kwa mda mrefu?
 
Wabunge 400@100 gas cylinders! Hii serikali hii!
Kuna mwingine aliingiza yutong bus mamia hakuulizwa. Hata makamba hawezi kuulizwa.
 
January Makamba alitoa wapi pesa ya kugawa mitungi ya gesi mia moja kwa kila mbunge?!

Bajeti ya kununua hiyo mitungi ilipitishwa lini na Bunge kama pesa ni ya wizara?!

Kwa nini Tulia kalitolea ufafanuzi jambo hilo kwa mda mrefu?
Kwenye Mfuko wa Nishati safi
 
Huyu wakati anasimamia ole wizara inayoshugulika na mambo ya simu aligawa simu kwa Kila mbunge ni kawaida yake kutoa rushwa hiyo time ya maadili sijui inafanya Kazi gani
 
January Makamba alitoa wapi pesa ya kugawa mitungi ya gesi mia moja kwa kila mbunge?!

Bajeti ya kununua hiyo mitungi ilipitishwa lini na Bunge kama pesa ni ya wizara?!

Kwa nini Tulia kalitolea ufafanuzi jambo hilo kwa mda mrefu?
Mutungi ya kampuni gani?Kama ni taifa gas au mihan gas ni promotion for rostam aziz
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…