Wabunge wapigwa darasa kuhusu nishati safi na salama ya kupikia. Kila mbunge kupewa mitungi 100 ya gesi

January Makamba alitoa wapi pesa ya kugawa mitungi ya gesi mia moja kwa kila mbunge?!

Bajeti ya kununua hiyo mitungi ilipitishwa lini na Bunge kama pesa ni ya wizara?!

Kwa nini Tulia kalitolea ufafanuzi jambo hilo kwa mda mrefu?
Niliwaambia kinachoendelea Bungeni ni full drama. Ndo maana watapitisha mabadiliko ya sheria ya TISS kwa kishindo.

Ndege wanaofanana huruka pamoja
 
Nchi ina vituko sana ,hivi kuna mbunge kwake anapikia mkaa au kuni mpaka wapigwe msasa, kama nchi sasa tumeanza mazalau ya wazi ya kutoeshimiana, iyo kazi wangepewa watendaji wa kata na vijiji ,ingetosha sana kufikisha elimu kwa wananchi ,vinginevyo ni ufisadi kama ulivyo ufisadi mwingine
 
January Makamba aweka historia kwa kuhonga Bunge zima la Tanzania


January Makamba ameandika historia.

Kiwango cha hii rushwa hakijawahi kutokea tangu Tanzania ipate uhuru.

Akiwa mtoa rushwa mkuu, January Makamba, amehonga Bunge zima la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa waziri

Je, ndoto yake ya kuwa Rais ikitimia si itakuwa jinamizi kwa taifa na atauza nchi nzima?

January ametumia taasisi chini ya Wizara ya Nishati, ikiwemo TANESCO, EWURA na TPDC kutoa rushwa ya zaidi ya Shilingi milioni 10 kwa kila mbunge

Aliwahonga wabunge kupitia posho za semina za mfululizo siku 2 kabla ya kusoma hotuba ya bajeti, akihalalisha pesa hizo kwa kutumia maonesho ya sekta ya nishati kwenye viwanja vya Bunge na semina za wabunge

Pia aliwahonga wabunge mitungi ya gesi 100 kila mmoja

Jumla ya pesa za umma alizotumia kuhonga wabunge ni zaidi ya Shilingi Bilioni 2

Tulia Ackson, ambaye mume wake ni bosi wa EWURA, alishirikiana kikamilifu na January kuhakikisha bajeti ya wizara yake inapita, licha ya usimamizi wake mbovu wa sekta ya nishati na tuhuma za ufisadi

Kwa rushwa hii, January amepoteza sifa zote za kuwa kiongozi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…