Wabunge wataka Condester Sichwale aliyetolewa nje kisa mavazi aombwe radhi

Wabunge wataka Condester Sichwale aliyetolewa nje kisa mavazi aombwe radhi

Sakata la kutolewa nje kwa mbunge wa Momba, Condester Sichwale (CCM) kuhusu mavazi, limeibuka tena leo jioni katika kikao cha Bunge baada ya wabunge wanawake kutaka aombwe radhi na aliyetoa hoja.

Hata hivyo mbunge Hussein Amar amesema hawezi kuomba radhi kwa sababu alichosema alikuwa sahihi kwakuwa mavazi aliyovaa mbunge mwenzake hayakuwa na staha ndiyo maana Spika wa Bunge Job Ndugai aliridhia hoja aliyoitoa yeye (Amar).

Katika kikao cha leo jioni wabunge Jacqueline Ngonyani na Stella Manyanya waliomba mwongozo wa Spika kwa madai mbunge aliyetolewa nje alionewa.

Mapema leo Sichwale alitolewa nje kwa amri ya Spika baada ya Amar kuomba mwongozo kwa kutumia kanuni 170 kuhusu mavazi ya staha.

Ngonyani amesema kilichotokea ni kwamba mbunge huyo alionewa kwani alikuwa na vazi la staha ambalo halikuwa na shida lakini akasema huenda Spika hakuona.

"Mimi ni mjumbe wa Baraza Kuu la wanawake wa CCM, ninapoona kuna uonevu lazima niseme na hili sikiungi mkono huyu mwanamke mwenzetu ameonewa,"amesema Ngonyani.

Mbunge huyo amesisitiza kuwa uonevu wa namna hiyo haupaswi kuvumiliwa kwakuwa umemdhalilisha mbunge huyo na wapiga kura wake jimboni.

Kwa upande wake Manyanya amesema tangu asubuhi alikuwa anafuatilia kwenye mitandao na amebaini kuwa Sichwale hakuwa na vazi baya.

Hata hivyo Manyanya amesema haiwezekani wabunge vijana wavae mavazi kama wanayovaa wabunge wanawake watu wazima.

Amesema katika siku za karibuni limeibuka suala la kutoa lugha za kuwadhalilisha wabunge wanawake ndani ya ukumbi ambako wakati mwingine hutamkwa kiungo cha mwanamke halafu wengine wanafurahi.

Naibu Spika Dkt. Tulia Akson amesema atatoa mwongozo baada ya kufuatilia jambo hilo.

Tulia mwenyewe ni kimeo tu
 
Kama dini yake inamruhusu kuvaa kiuchiuchi angeachwa tu, kwani kuna ajabu gani? Hiyo mbona kawaida sana kwa jamii nyingine/ ingawa serikali haina dini?
Huyu mbunge wangu naona sasa kazi imemshinda, watu wake wa jimbo tuna changamoto nyingi mfano maji vijiji vingi havina maji mradi wa maji kutoka ziwa victoria pale nyamtukuza haujakamilia sasa kageukia kuangalia akinadada wamevaa nini bungeni badala ya kusimamia hoja za msingi juu ya wananchi wake
 
Badala kujadili mambo muhimu ya kitaifa, watumishi wanaiba kwa kujilipa posho hadi 300m kwa wiki. Bunge la ccm linajadili mavazi, afu mtu anasema Magufuli (aliewaleta hawa bungeni) ni shujaa.
Ilikuwa ni lazima aondoke kwani alituhatibia Sana Nchi...
 
Mwendazake alijipambanua kama mzalendo, lakini kwa maoni yangu mimi naona hakuwa Mzalendo, ila alikuwa na ajenda yake ambayo alitaka kuipitisha kupitia neno la uzalendo.
Mungu akamuwahi na kupitisha "ajenda" ya kumuondoa....
 
Pia waombe radhi kwa kuacha covid-19 ikae bungeni tu😷
 
Sakata la kutolewa nje kwa mbunge wa Momba, Condester Sichwale (CCM) kuhusu mavazi, limeibuka tena leo jioni katika kikao cha Bunge baada ya wabunge wanawake kutaka aombwe radhi na aliyetoa hoja.

Hata hivyo mbunge Hussein Amar amesema hawezi kuomba radhi kwa sababu alichosema alikuwa sahihi kwakuwa mavazi aliyovaa mbunge mwenzake hayakuwa na staha ndiyo maana Spika wa Bunge Job Ndugai aliridhia hoja aliyoitoa yeye (Amar).

Katika kikao cha leo jioni wabunge Jacqueline Ngonyani na Stella Manyanya waliomba mwongozo wa Spika kwa madai mbunge aliyetolewa nje alionewa.

Mapema leo Sichwale alitolewa nje kwa amri ya Spika baada ya Amar kuomba mwongozo kwa kutumia kanuni 170 kuhusu mavazi ya staha.

Ngonyani amesema kilichotokea ni kwamba mbunge huyo alionewa kwani alikuwa na vazi la staha ambalo halikuwa na shida lakini akasema huenda Spika hakuona.

"Mimi ni mjumbe wa Baraza Kuu la wanawake wa CCM, ninapoona kuna uonevu lazima niseme na hili sikiungi mkono huyu mwanamke mwenzetu ameonewa,"amesema Ngonyani.

Mbunge huyo amesisitiza kuwa uonevu wa namna hiyo haupaswi kuvumiliwa kwakuwa umemdhalilisha mbunge huyo na wapiga kura wake jimboni.

Kwa upande wake Manyanya amesema tangu asubuhi alikuwa anafuatilia kwenye mitandao na amebaini kuwa Sichwale hakuwa na vazi baya.

Hata hivyo Manyanya amesema haiwezekani wabunge vijana wavae mavazi kama wanayovaa wabunge wanawake watu wazima.

Amesema katika siku za karibuni limeibuka suala la kutoa lugha za kuwadhalilisha wabunge wanawake ndani ya ukumbi ambako wakati mwingine hutamkwa kiungo cha mwanamke halafu wengine wanafurahi.

Naibu Spika Dkt. Tulia Akson amesema atatoa mwongozo baada ya kufuatilia jambo hilo.

Libunge linaleta mambo yake ya dini kwenye chombo kisicho cha dini,
 
Vizee kama hivyo vikitoka nje ya vikao unavikuta vinalilia nyapu za hao hao wanaowaponda pumbavu kabisa
 
Kwani wametumwa na wananchi au Magufuli ndio aliwaingiza bungeni kwa kunajisi uchaguzi, ili wamuongezee muda wa kukaa madarakani?
... Mungu kampunguzia muda wa kukaa duniani! Na ijulikane maisha ni zaidi ya madaraka!
 
Kwani spika alimtoa nje kwa utashi wake au kwa mujibu wa kanuni za bunge.....?? Na hata aliyeomba muongozo aliomba kwa mujibu wa kanuni za bunge.....
... tatizo maamuzi yale yalikuwa more subjective (mwomba mwongozo na mtoa maamuzi) than objectivity. "Vazi la staha" ndio lipi? Kwa vipimo vipi? Mjinga yeyote mle aki-colude na Speaker mbunge yeyote anaweza kufukuzwa simply baadhi ya kanuni ni za kipumbavu.

Bora hata wangepiga kura kufikia maamuzi would be more representative kuliko mtu mmoja kuropoka na ikawa final!
 
Ni kweli hakuna aliye juu ya sheria....

Hoja yangu ni kuwa ni sheria ipi iliyovunjwa ?!!

Una uhakika mbunge wa Nyang'wale alikusudia Kumdhalilisha mh.Condester ?!!!

Je mh.Spika naye amemdhalilisha mh.Condester?!!

Je hakuna taratibu za uvaaji mule bungeni ?!!!

Hivi unaelewa kuwa hata ukivaa KANZU na KIBARAGHASHIA bila ya KOTI unaweza kutolewa ?!!
Je ukitolewa utakuwa umedhalilishwa ?!!!

Ama unalalamika KIHISIA tu kujustify "HAKI ZA AKINAMAMA" pasina WAJIBU ?!!!

#KaziIendelee
Umemaliza mjadala,kama ni mwalimu,nina hakika darasa lako,wanapata A+ wote

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
 
BADALA YA KUJADILI REPORT YA CAG,NA MAMBO MENGINE MUHIMU KWA TAIFA HILI BADO WANAJADILI MAMBO YA KUVAA NGUO
WABUNGE MULE WANAPENDA KUJADILI VI ISSUE VIDOGO VISIVYOKUWA NA MAANA
ISSUE MUHIMU HAWAJADILI

OVA
 
Hakukuwa na shida na vazi la mbunge huyo...

Ni wazi kuna shida nyingine tu binafsi za baadhi ya wabunge wa kiume na baadhi ya wanawake na Spika pasipo kujiuliza mara mbili anakubali kuingia ktk mkenge huo...

Kuna wanawake wengine wana maumbo maalumu. Hata wavaeje tu, maumbo utayaona kwa uwazi sana na kama wewe ni mwanaume usiyeweza kudhibiti hisia zako za kingono, utamtamani tu mwanamke huyo huku ukijua huwezi kumpata...

Nadhani huyu mbunge wa kiislamu alitaka huyu mwanamke akavae ushungi au baibui - lile vazi maalumu la wanawake wa kiislamu
View attachment 1805717
Hao hapo wote ni wabunge na walikuwa ndani ya bunge Jana tarehe 1/6/202. Kulia ni Catherine Maggie na wa kushoto kwako kwenye picha ni Condester Schwale...

Sichwale aliyolewa nje lakini Catherine Magige alibaki ndani ya bunge akiendelea na shughuli kama kawaida kwamba, yeye yuko vizuri...

Mimi nasema, hili sakata halihusiani na mavazi. Kuna kitu nyuma ya pazia na bahati mbaya ni kuwa uongozi wa bunge unakubali kuyumbishwa na personal interests za baadhi ya wabunge kudhalilisha baadhi ya wabunge wanawake...
Acha udini.,usiingize udini katika mjadala huu.

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
 
Hawa wenzetu (baadhi) ni wa ajabu sana. Wanadhani ili Mungu muumba wa vyote amkubali mwanadamu kuwa mtakatifu na Mtoto wake, basi anaangalia mavazi...

Mungu hutazama ndani ya moyo/nafsi ya mtu kama ni msafi na mkamilifu au la...

Jamaa anatamani wanawake wote wavae baibui au ushungi na kanzu ndefu hadi kwenye vidole vya miguu. Hakuna kitu kama hicho...!!

Mavazi, kwa maana mtu avae nini na kivipi inabaki siku zote ni utashi wa mtu binafsi ili mradi ni yanafunika yale maungo nyeti ya mwili wa mtu huyo vyema...

Hakuna shida kwenye vazi la yule dada. Shida iko kwenye fikra za baadhi ya wanaume ambao wanaweza kuwatamani kingono hadi mama au dada zao kwa sababu tu eti hawajafunika vichwa na nywele zao kichwani...!!

Lol, hili ni balaa kubwa kabisa...
Acha udini,kwenye mjadala.Wapo wasio na ushungu wa buibui Hujawahi kuona picha za mama wa Yesu,Maria kavyaa ushungu,na na picha na sanamu hizo zipo makanisani na kwenye vitabu vya kanisani

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom