Sooth
JF-Expert Member
- Apr 27, 2009
- 3,922
- 5,620
Mimi nataka ushushwe.Mataifa mengi yanatambua mtu mwenye miaka 35 anaweza kuwa Rais.Sisi kwa nini tunaweka vizuizi? je watanzania tunachelewa kukomaa?Mbona umri wa ukomavu kisheria katika kufanya maamuzi na kupiga kura ni miaka 18 kama ilivyo kwa nchi nyingine?
Mbona Nyerere alikua Rais akiwa under 40?
Nakubali kuna watu walikua marais wakiwa under 40 lakini walifanikiwa kuongoza kwa weledi na kuna wengine waliofeli vibaya.
Come on Filipo!
Bila kuja na ushahidi wa kibaioloia, kisaikolojia au kisosholojia utakaoonyesha kwamba umri wa miaka 35 ndo umri muafaka wa kugombea urais, hoja hii itakuwa na ni ya ushabiki tu. Binafsi ningependa umri ushushwe hadi miaka 18 maana ndo umri ambao mtu anaweza kupiga kura na inaleta maana kwa mpiga kura naye kuweza kupiga kura.
Binafsi ningependa tuandike katiba ya wananchi wote, sio katiba ya kumwezesha Zitto au kikundi chochote kuwa rais. Kufanya hivyo ni aina fulani ya udikteta na mfano mzuri ni Mseveni anayebadilisha katiba kila anapojisikia ili aendelee kugombea. Tunatakiwa tujiulize tunataka rais mwenye sifa zipi ndipo tujaribu kuoanisha na umri mwafaka na sio kuanza na maslahi ya kundi au watu ndipo tupendekeze umri.