Wabunge wataka Umri wa kugombea Urais uwe 35; Zitto asema umri mkubwa ni ushamba

Wabunge wataka Umri wa kugombea Urais uwe 35; Zitto asema umri mkubwa ni ushamba

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), ametaka umri wa kugombea urais ushushwe kutoka miaka 40 hadi kufikia 35.
Zitto ambaye amekuwa akihusishwa na harakati za kuusaka urais mwaka 2015, huku kigezo cha umri kikitajwa kuwa kikwazo, alitoa kauli hiyo jana wakati akitoa maoni yake kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyofika jana mjini hapa kukusanya maoni ya wabunge.
Akitoa maoni yake, Zitto alisema ni ushamba kwa nchi kama Tanzania kuweka umri mkubwa kama sifa ya kugombea urais.
“Umri wa kugombea urais, Rwanda wenzetu wanaruhusu miaka 35, Burundi miaka 35, Kenya miaka 35, Marekani miaka 35, Afrika Kusini miaka 35…Sisi ni ushamba tu, hakuna sababu ya kuweka umri mkubwa,” alisema Zitto ambaye wakati akianza kuchangia alitania akisema kuwa itakapofika mwaka 2015 atakuwa na umri wa miaka 39.
Mbali na Zitto, wengine waliounga mkono hoja hiyo ni pamoja na Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Keissy (CCM), Mbunge wa Tarime, Chacha Nyambari Nyangwine (CCM), Mbunge wa Nzega, Dk. Khamis Kigwangwala (CCM), Mbunge wa Viti Maalumu, Dk. Prudenciana Kikwembe (CCM) na Mbunge wa Kasulu Vijijini, Agripina Buyogera (NCCR-Mageuzi).
Kwa upande wake, Keissy alipendekeza umri wa kugombea urais iwe kati ya miaka 35-40 kwani umri huo ni watu wenye nguvu.
“Hii nchi ni kubwa sana… ina milima na mabonde, tunataka rais ambaye ataweza kutembea nchi nzima na mabonde yake, hatutaki kusikia rais ambaye baada ya siku mbili tukasikia ameenda India, Pakistan kutibiwa,” alisema.
Nyangwine alipendekeza miaka 35 na kuendelea na kuongeza kuwa, hali hiyo itatoa nafasi kwa vijana kushiriki, huku Dk. Kigwangala akisema haoni sababu ya umri kuwa zaidi ya miaka 35 kwa mtu kuwa rais.
Zitto amekuwa akitajwa kuusaka urais 2015, huku akipigania sifa ya umri kwa mtu kuwa nafasi hiyo ipunguzwe kutoka miaka 40 kwa mujibu wa katiba ya sasa hadi 35.
Tayari mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini amewahi kukaririwa mara kadhaa akisema kuwa hana mpango wa kugombea tena ubunge ifikapo mwaka 2015, badala yake anajipanga kuwania urais.
Mbali na hoja hiyo ya umri wa urais, nyingine ambayo ilionekana kuwagusa wabunge wengi ni ile ya Muungano.
Wabunge wengi hasa wa kutoka Zanzibar, walionekana kutotaka Muungano uvunjwe, badala yake walipendekeza kuwe na muundo mwingine tofauti na wa sasa.
Walipendekeza mifumo mitatu ya muundo wa Muungano. Muundo wa kwanza ni ule wa serikali tatu, muungano wa mkataba na tatu muungano wa kuwa na rais mmoja na mawaziri wakuu wawili; mmoja kutoka Tanzania bara na mwingine Zanzibar.
Wabunge waliopendekeza mfumo wa serikali tatu ni pamoja na Mbunge wa Mkanyageni, Mohamed Habib Mnyaa (CUF), ambaye alitaka pia uongozi uwe wa mkataba baada ya ule wa serikali mbili.
“Mfumo wa sasa umeleta matatizo sana, mimi napendekeza iwepo Serikali ya Bara ambayo sijui mtaamua kuiita Mzizima au lolote na ile ya Zanzibar, na Rais wa Muungano achaguliwe na wananchi wote kulingana na mzunguko wa kubadilishana,” alisema mbunge huyo.
Baadhi ya wabunge waliopendekeza muundo wa serikali tatu na ule wa mkataba ni pamoja na Mbunge wa Tumbe, Rashid Ali Abdallah (CUF), Mussa Kombo (Chake Chake), na Kombo Hamis Kombo (Magogoni) ambao wote ni wabunge wa CUF.
Wengine ni wabunge wa viti maalumu, Easter Bulaya na Diana Chilolo, wote kutoka CCM.
Kwa upande wa wabunge waliokuwa wakiunga mkono mfumo wa serikali mbili, wengi wao walionekana kuwa ni wa CCM.
Miongoni mwao ni pamoja na Mbunge wa Manyoni Mashariki John Chiligati (CCM), Mbunge wa Bunda, Steven Wassira (CCM), Mbunge wa Dole, Silvester Mabumba (CCM), Mbunge wa kuteuliwa na Rais, Zakhia Meghji, Mbunge wa Iramba, Mwigulu Nchemba (CCM) na wengine. Hata hivyo, wabunge hao waliokuwa wakitetea muundo wa serikali mbili walipendekeza uwepo utaratibu wa kushughulikia kero zinazowakabili Wazanzibari, huku wakitaka iundwe tume ya kushughulikia kero hizo.
Wengine walipendekeza Zanzibar iachwe huru katika masuala ya mafuta, bandari pamoja na kutaka isaidiwe kiuchumi.
Katika hilo, Chilligati alisema; “Kama muungano ungekuwa ni sumu inayojaribiwa, tungethubutu kuuvunja kwa muda kidogo, kule Zanzibar Watanzania elfu 15, na Wanzanzibari walioko bara laki 2.5 waonje adha ya kutafuta hati ya kusafiria au waambiwe wahame, tungejaribu kufanya hivyo.”
Alikosoa mfumo wa serikali tatu, Chiligati alisema unaongeza gharama kwa sababu utahitaji Baraza la Mawaziri na rais mwingine, na kwamba Tanganyika iliyokufa itabidi ifufuliwe.
Mbali na hilo, suala la mgombea binafsi nalo lilichukua nafasi kubwa katika maoni waliyokuwa wakichangia wabunge hao.
Wabunge wengi walipendekeza Katiba ijayo itamke wazi juu ya mgombea binafsi, ikiwa ni pamoja na uwepo wa Mahakama ya Katiba.
Aidha, wabunge wengi walitaka viti maalumu viondolewe na kupendekeza mfumo mwingine wa kuwanyanyua wanawake, ikiwa ni pamoja ule wa kutaka mbunge anayesimama katika jimbo asimame na mgombea mwenza mwanamke na atakapopita, mgombea mwenza naye atakuwa mbunge.
Suala la ukubwa wa madaraka ya rais nalo lilionekana kuwagusa wabunge wengi, ambao karibu wote waliochangia wakiwamo wachache wa CCM, walitaka yapunguzwe.
Pia walitaka utaratibu wa mawaziri kutokana na wabunge, ufutwe na kupendekeza mawaziri wateuliwe nje ya Bunge na wawe wataalamu wa wizara husika.
Kuhusu suala la mihimili mitatu, yaani Serikali, Bunge na Mahakama, wabunge wengi waliotoa maoni walitaka Katiba ijayo itamke wazi kuwa ni kosa kuingiliana na mihimili mingine.
Kwa upande wa wahujumu uchumi, baadhi ya wabunge waliotoa maoni walitaka watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo wanyongwe.
Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali (NCCR-Mageuzi), alisema hakuna sababu ya kulinda haki ya mhujumu uchumi ambaye amepewa mabilioni ya fedha kwa ajili ya kununulia dawa na badala yake anaweka fedha mfukoni halafu unalinda haki ya mtu mmoja.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, ambaye alipata wakati mgumu, alisema kabla ya kuanza kukusanya maoni kwa wabunge alipata woga.


[TD="bgcolor: #ffffff"]
Zitto: Umri kuwania urais uwe 35
• Asema ni ushamba kuweka umri mkubwa kama sifa ya kugombea urais

na Ratifa Baranyikwa, Dodoma


[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF, align: center"]
amka2.gif
[/TD]
:crazy::crazy
:

Ushamba urais, urais ushamba
 
kazi ipo na huyu mkigoma! kweli leka dutigite!!!
 
Tatizo kubwa ni kwa waliodhalilisha mamlaka ya urasi wa Jamhuri ya watu wa Tanganyika kufikia hatua ya kuwaona Watanganyika 'washamba' pale wanapohoji aina na malengo ya 'udikteta' wa vijana wanaotaka kuumeesha kwa kivuli cha ujana. Who said we need our president to swim in all valleys, lakes and ocean and climb all mountains of Tanganyika? Being a president is more than body physique other wise the Matumla's and Nyambui's are the very best presidential materials!
 
kwenye hiphop culture tunamuita zitto kabwe...SNITCH..FAKE ASS NIGGER😱hwell:
 
Nilishasema Zitto ni Sanguine, kwa jamii inayohitaji kwenda mbele ni hatari kuwa nae na kumpa mamlaka,

Akiwa rais anaweza kuja na ngonjera za kuongeza umri ilimradi adumu madarakani!

Kafanya perfect timing na kalender ya CCM ,ila wrong execution kama kawaida ya magamba.Sasa hakuona kuwa kuna watu kama nyinyi mtakaomuona kuwa ni perfect candidate wa kuongeza miaka.teh teh..kweli CCM walifanya kazi nzuri India,na wamempata mtu sahihi kwa kazi yao mtu mwenye baurning desires ila hawakuwa na uwezo wa kumpa mipango mizuri.
 
Zitto katika nafsi yake anajua fika kuwa hana ubavu wa kushindana na wagombea wa ccm,ilo analijua kuwa hayuko popular kiasi hicho,wengi tunamuona kama Kashibuda fulani tu,ni time bomb kwa CHADEMA very soon ata explode,kwa maono yangu tamaa yake very soon italeta madhara makubwa kwa CHADEMA na pia itamuweka Zito kwenye political archive
 
why 7 years for presidential post? ama wanadhani miaka 10 ni mingi sana,kwa hiyo wanapunguza kwa mtu kuongoza mfululizo miaka 7?,tuwe na kipindi cha miaka 8,na kila mhula uwe na miaka 4 tu na tunaingia ktk uchaguzi kila baada ya miaka 4
 
Zitto anautaka uraisi ili aifanyie nini Tanzania,
 
Oooh then that explains it. So 40 haimfai. Pengine, thisis my own feeling; kigezo kikiwa miaka 30 hata Nassari nae atakwalifayi. Im just saying target binafsininahusika hapa.

Kwani ana ugomvi na Nassari?
 
Maoni ya kipumbavu na kijuha na kama wabunge wa Chadema mmeshiriki maoni haya ya kuweka kipindi cha rais kiwe kimoja1 kwa miaka 7 basi mjue na nyie mmekuwa mafaalla pia na kama mnataka rais wa Zanzibar awe makamu wa rais basi na huo ni ufalllla.
Duh! Matusi ya nini sasa! hayo ni maoni yako na haimaanishi ndo katiba itakuwa hivyo...Hata hivyo na wewe unaruhusiwa kutoa maoni yako na si kutukana kwa kuwaita binadamu wenzio hivyo ulivyowaita...
 
why 7 years for presidential post? ama wanadhani miaka 10 ni mingi sana,kwa hiyo wanapunguza kwa mtu kuongoza mfululizo miaka 7?,tuwe na kipindi cha miaka 8,na kila mhula uwe na miaka 4 tu na tunaingia ktk uchaguzi kila baada ya miaka 4
Wazo lako pia ni jema...kama USA siyo!

 
hatuwezi kua na rais wa miaka 35...hao wa sasa tunaowachagua wa miaka 60 bado wanafanyaga kazi kitoto sasa tukimweka wa 35 itakuaje? au mnataka tue tunakutana na rais wetu billicanas, yaani ndio kazi wanayofanya bungeni sasa hivi kuongea na kujadiliana pumba
Ulaumu tu ndugu yangu...Toa solution..We ungependa wa kuanzia miaka mingapi!Mind you hata hao wa 60 bado wanafanya kazi kitoto kama ulivyo sema.
 
Asante kwa kutujuza, ila haya mambo kwa nini yanajadiliwa bungeni wakati tuko kwenye Mchakato Wa kuandika katiba mpya?

Ina maana CCM ikipitisha haya itakuwa imetudharau wananchi!
Tume ya Mabadiliko ya Katiba ikiongozwa na jaji Warioba, ilitembelea Bungeni kupata maoni ya wabunge...
 
Lengo la kutaka mgombea ubunge kuwa na mgombea mwenza ni nini hasa? Je mgombea anaposhinda huyo mwenza nae atahudumiwa kwa kodi hii hii? Au itakuaje? Ila kufanya wilaya kuwa majimbo ya uchaguzi ni bora zaidi maana itapumguza idadi ya wabunge na hivyo kupunguza gharama.

Lengo ni kufuta viti maalum coz imeonekana viti maalum havina tija, ila kwa kuwa wanawake wanatakiwa kushiriki katika vyombo vya maamuzi kwa asilimia 50, ndo ikapendekezwa majimbo ya sasa yafutwe afu kila wilaya iwe jimbo..Na kila mwanaume akigombea jimbo basi awe na mgombea mwenza mwanamke na kama mwanamke atagombea asiwe na mgombea mwenza. Wanadai hii itapunguza ukubwa wa bunge kwa maana ya idadi ya wabunge hivyo kuokoa pesa nyingi lakini wakati huo huo kuwaempower wanawake...Pia wanadai hii itasaidia uwajibikaji kwani kutamfanya mgombea mweza kuona kachaguliwa na wanachi wa wilaya husika na si kikundi cha watu wachache..
 
Raisi akiwa na miaka 35, atakapoacha uraisi hata kama ni kwa miaka 10 atakuwa na miaka 45. Je na uchumi huu tutaweza kumtunza rais mstaafu mwenye miaka 45? Mimi naona rais awe ma miaka 55 na kuendelea.

Wabunge wanataka kipindi cha rais kiwe ni miaka 7 - na hakuna term ya pili. Kwa maana hiyo kama mtu atachaguliwa kuwa rais akiwa na miaka 35, atastaafu urais (kisheria) akiwa na umri wa miaka 42! At 42 years of age anakuwa 'pensioner'! Huu ni umaalun. 42!!! Imagine tutakuwa na marais wastaafu wangapi?

Kama ni hivyo basi rais mstaafu naye asiruhusiwe kuchukuwa mafao yake hadi afikishe umri wa miaka 60!
 
Lengo ni kufuta viti maalum coz imeonekana viti maalum havina tija, ila kwa kuwa wanawake wanatakiwa kushiriki katika vyombo vya maamuzi kwa asilimia 50, ndo ikapendekezwa majimbo ya sasa yafutwe afu kila wilaya iwe jimbo..Na kila mwanaume akigombea jimbo basi awe na mgombea mwenza mwanamke na kama mwanamke atagombea asiwe na mgombea mwenza. Wanadai hii itapunguza ukubwa wa bunge kwa maana ya idadi ya wabunge hivyo kuokoa pesa nyingi lakini wakati huo huo kuwaempower wanawake...Pia wanadai hii itasaidia uwajibikaji kwani kutamfanya mgombea mweza kuona kachaguliwa na wanachi wa wilaya husika na si kikundi cha watu wachache..

Kama lengo ni kupunguza idadai ya wabunge, wabaki na hoja hiyo hiyo tu ya kufanya wilaya kuwa majimbo (japo hapa idadi ya wakazi inabidi izingatiwe) hayo mambo ya kuwa na wagombea wenza hayana maana yoyote. Wanawake inabidi wakubali sasa kuwa wana uwezo wa kupambana na wanaume majukwaani. Haya mambo ya kupendelewa yameshapitwa na wakati maana yanalemaza sana na kudhalilisha pia. Kama ofisini naweza kufanya kazi yangu vizuri kuliko mwanaume, na kama mtoto wangu wa kike anaweza kufaulu vizuri kuliko watoto wa kiume kwanini asiweze kushindana nao katika ulingo wa siasa?
 
sifa iwe moja tu...18 yrs and above.mwenye sifa ya kupiga kura awe na sifa ya kupigiwa kura.

mkuu, umemaliza kila kitu wengine wote longolongo. Wanaopendekeza umri ubaki 40 yrs ni wabaguzi tu kama wale wanaotaka ushuke hadi 35. Haki ya below 35 hadi 18 abv iko wapi?!
 
zito ameshaona watanzania ni wajinga kama anavyofikiri kwamba anaweza kutuchezea akili kipumbavu hivyo.. Aseme umri wake hautatosha kugombea urais km anavyotegemea. kwanini asiseme umri wa kugombea ni kati miaka 20 hadi 35??? akaona aseme 35 nad above.. Hatudanganyiki???? Atajipigia kura mwenyewe hata akigombea..
 
Anajipigia debe! CDM wasafishe uvundo unaoitwa kabwela mara moja.
 
Back
Top Bottom