ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,040
- 7,303
Rais hajiingilii Ikulu kiholela, anapigiwa kura na watu, kwa hiyo hata ikiwa miaka 18 poa tu as long as majority ya wapiga kura wataamini kuwa ndiye mtu anayefaa kuongoza nchi.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
zitto atuambie ni kigezo gani alichutmia kuset umri wa chini kuwa miaka 35? au kwa kuwa yeye yuko above 35? kuna watu wana miaka 30 nao wanautaka Urais!
UBINAFSI BWANA!
humu jF naona kazi ya wengi humu ni kumponda zitto awe mpenzi wa chadema awe wa nyinyiem bado tu mnamwandama zitto.. kiukweli zitto siwezi mdharau maana yeye ndie alienifumbua macho na chadema kilipendwa na watu wengi kipindi cha zitto halafu mnasema pumba gani hapa? kwani mnataka raisi awe mwenye mvi? wana chadema wenzagu tumpe zitto nafasi agombee akishindwa atajua mwenyewe akishinda safi tu ilimradi ccm ametoka pale..kwisha habari
zito ameshaona watanzania ni wajinga kama anavyofikiri kwamba anaweza kutuchezea akili kipumbavu hivyo.. Aseme umri wake hautatosha kugombea urais km anavyotegemea. kwanini asiseme umri wa kugombea ni kati miaka 20 hadi 35??? akaona aseme 35 nad above.. Hatudanganyiki???? Atajipigia kura mwenyewe hata akigombea..
Ntakuwa na amani nikiku support wewe,una base na hoja yako, sio kwasababu usa wanafanya.uliwahi ona usa wana Raisi mwenye umri chini ya 45? zitto huna hoja,yako ni kuwa umezidi miaka 35 tu.bora hii ya kutimiza haki ya kila mtanzania kikatiba.kuchagua na kuchaguliwa.unaweza kusikilizwa na watu wenye akili.
Mods unganisheni na uzi huu hapa
www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/152109-jk-ataka-rais-ajaye-asiwe-wa-rika-lake-5.html
NB:Msimamo wangu uko pale pale sababu ya umri kuwa 40+ and above haielezwi
Tusiwazuie vijana kwa kutumia nguvu.Kama katiba inamtambua mtu mwenye miaka 18-35 kama kijana,ni kwa nini mwenye umri wa kati from35-40 usipewe uwezo wa kuongoza taasisi ya urais?Pia kwa nini tusiweke ukomo mwisho miaka 80 kwa sababu za kibaiolojia na kisaikolojia?
Hii age 35-40 imenyimwa baadhi ya haki za kuchaguliwa.Nyerere na Akina Lumumba walikua katika group hii walipochukua uongozi.Kwa nini tuwazuie ikiwa tunakubali wameshavuka ujana.Si wananchi wakiona hawafai wataamua wenyewe?tusitumie udikteta wa kisiasa kuhalalisha uhaini wa kidemokrasia kupitia mchakato wa kisheria kwa ghiliba
Zaidi ya vigezo vya umri tuangalie uadilifu na dira sahihi kwa Taifa.
Kwanza hao wabunge nao mbona walikomaa sana na umri wa urais?kuna suala la code of conduct,moral standard n.k
Hivi yeye alipopelekwa kutibiwa India alikuwa mzee?
Kwanza nataka kujua kama kuna ukweli ktk habari hii maana Wabunge wetu watakuwa wamefanya dharau kubwa sana kwa rais na wananchi wa Jamhuri ya Tanzania. Hoja hiyo Spika wa bunge hakutakiwa hata kuipa nafasi..
nasema hivi kwa sababu wananchi hawakuwatuma wabunge wao kwenda kuzungumzia haya bungeni, maana tayari tunayo Tume ya kukusanya maoni na tayari inaifanya kazi hiyo. Maoni yetu yanakusanywa na wao wabunge kama wananchi wanatakiwa kutoa maoni yao kwa tume hiyo na sio kuyapeleka Bungeni yajadiliwe.
Ifike wakati na mahala maamuzi ya kitaifa yaheshimiwe. Hatufanyi kurekebisha katiba iliyopo bali tunaandika katiba mpya na uamuzi umeshafikiwa kwamba kufikia mwaka 2014 katiba mpya itakuwa tayari..Mwisho wa yote haya mapendekezo yote yaloorodheshwa hapo juu ni kuhusu maslahi yao tu viongozi ktk ngazi zao hakuna mapendekezo yoyote yanayowahusu wananchi iwe vyombo vya kulinda na kusimamia maswala ya Wakulima, wafanyakazi, maliasili na rasilimali zetu - It's all about THEM.
Wabunge wanataka kipindi cha rais kiwe ni miaka 7 - na hakuna term ya pili. Kwa maana hiyo kama mtu atachaguliwa kuwa rais akiwa na miaka 35, atastaafu urais (kisheria) akiwa na umri wa miaka 42! At 42 years of age anakuwa 'pensioner'! Huu ni umaalun. 42!!! Imagine tutakuwa na marais wastaafu wangapi?
Kama ni hivyo basi rais mstaafu naye asiruhusiwe kuchukuwa mafao yake hadi afikishe umri wa miaka 60!
Kamanda Tupo ukurasa mmoja.Nakumbuka hii mada ya umri ililetwa hapa mwaka jana na nilisema age group ya 35-40 imekua deprived off haki yao ya kikatiba.Imebaki haki ya kupiga kura tu.
Pia niliongelea umuhimu wa vigezo vya kibaiolojia na kisaikolojia vya kuweka limit ya urais.Kuanzia miaka 80 and above iwe no.Tuangalie diminishing criteria katika reasoning capacity and tough/prudent desicion making capability.
Tuweke uadilifu na sifa nyingine mbele kwa kulenga maadili ya uongozi