Wabunge wataka Umri wa kugombea Urais uwe 35; Zitto asema umri mkubwa ni ushamba

Wabunge wataka Umri wa kugombea Urais uwe 35; Zitto asema umri mkubwa ni ushamba

hatuwezi kua na rais wa miaka 35...hao wa sasa tunaowachagua wa miaka 60 bado wanafanyaga kazi kitoto sasa tukimweka wa 35 itakuaje? au mnataka tue tunakutana na rais wetu billicanas, yaani ndio kazi wanayofanya bungeni sasa hivi kuongea na kujadiliana pumba
 
Sina Shida na umri wa Miaka 35 mtu kuwa raisi ni umri sahihi kama tukipata mtu sahihi mchapa kazi na mwenye uzalendo na nia ya dhati ya kuendeleza hii nchi ila nina shida sana na sababu za Zitto nadhani anasukumwa na ubinafsi na tamaa ya uraisi kutaja hizi sababu sidhani kama 2015 angekuwa na miaka arobaini angetoa haya maoni
 
Kwa sababu by 2015 yeye ndo atakuwa kaufikisha huo umri. Ikiwekwa 38 atakuwa hana sifa hiyo ya kugombea

Kwa mujibu wa vyanzo mbali mbali, ikifika wakati wa kupiga kura mwaka 2015, Zitto atakuwa na umri wa miaka 39
 
Nimenukuu haya maelezo toka Wanabidii kwenye mada hiyohiyo

"Zitto naona anakosea kuita watunga katiba iliyopo ni washamba; Hansard za mjadala wa utungaji wa katiba iliyopo zipo n wabunge walitoa sababu za kwa nini miaka ya kuruhusu kugombea urais iwe 40 na kuendelea.

Sababu moja iliyotolewa ni kuwa mtu akiwa rais at 40 na akatawala miaka 10 atalazimika kuachia ngazi akiwa na miaka 50. Umri huu unamruhusu atumikie jamii hadi 60 na kuingia ustaafu rasmi. Gharama ya kuhudumia mtaafu huyu kwa taifa hazitakuwa kubwa kama mtu ataacha urais akiwa miaka 45 au 40 kama atakuwa Rais at 30!

Pili, at 45 huyu mstaafu atakuwa bado active na kuweza kusumbua utawala uliochukua baada yake, na hivyo kuwa na miaka mingi sana ya kuhudumiwa na taifa akiwa!

Kuna sababu nyingine zilizozingatia mila na desturi za mwafrika ambazo zilitolewa. Kwa bahati kuna wanabidii walio bungeni wanaweza kuzipata nakala za hansard za mjadala huo wa katiba wa 1977, mabadiliko ya 1992, na 1997. Wakasaidia jukwaa kujua sababu zote zilizotolewa kuhusu suala la umri!"
 
Oooh then that explains it. So 40 haimfai. Pengine, thisis my own feeling; kigezo kikiwa miaka 30 hata Nassari nae atakwalifayi. Im just saying target binafsininahusika hapa.
Kwa mujibu wa vyanzo mbali mbali, ikifika wakati wa kupiga kura mwaka 2015, Zitto atakuwa na umri wa miaka 39
 
Mbona hata mie nina miaka 25 na ninautaka urais. Kwanini Zitto apendekeze kwenye range ya umri wake tu!?..
"Ikulu si mahala pa kukimbilia" Mwl Nyerere
My take;
Zitto Zuberi Kabwe ni Janga lingine la kitaifa
 
........uvccm nasisi tubadili umri uongezwe hadi 40yrs ili na mm nigombee uenyekiti 2017!!!!!! teh teh teh
 
Zitto ana hoja ya msingi sana.

Ni kwa wale tu wasiotaka kufikirisha bongo zao na kutumia mioyo yao ndio wanamu attack.

Tunajua kwamba vyama vikuu vya siasa hapa Tanzania kwa sasa yani CCM na CHADEMA vyote
vina jumuiya za vijana yani (UVCCM na BAVICHA). Nakwenye hizo Jumuiya wameweka wazi kuwa utakua elligible
kuwa mwanachama ukiwa na umri wa kati ya miaka 18 mpaka 35. Kwa maana hiyo, hata vyama vyetu vinatambua
kuwa mtu ukifika miaka 35, tayari unakua umekomaa, huwezi kuitwa kijana tena.

Sasa mathalan mtu ana miaka 37, ambaye vyama vyote vinasema ameshakomaa, ni hoja ipi inatosha kusema
asiruhusiwe kugombea Urais? Mtu apewe fursa halafu waachiwe wananchi wenyewe wachague?? Kwani mmelazimishwa kuchagua mtu mnayemuona ni " sharobaro"? Tatizo liko wapi? Au kwa vile tuna "mtu wetu" hatutaki mawazo mbadala kwa
kudhani atakua affected na mabadiliko hayo ya katiba? If that is the case then hakuna chama hapo kwa maana ya taasisi ila kuna genge la watu wanounganishwa na maslahi binafsi ya mtu mmoja mmoja.

UVCCM na BAVICHA vimeshasema mtu akifika miaka 35 huyo ameshakomaa.

Naunga mkono hoja ya ZZK.
 
Ndugu zangu great thinkers, chuki haijengi hata kidogo. Mnamchukia binadamu mwenzenu bila hata sababu za msingi, kisa tu ni zaid yenu! Hebu muacheni Zitto aendelee na ndoto zake za u rais. Hakuna hata mmoja anatoa sababu za msingi za kupinga umri kushushwa zaidi ya kusema "Zitto Zitto", mtakufa na vijiba vya roho.
Zitto nenda baba nenda, katimize ndoto zako, tena wala usigeuke nyuma. Watanzania tuko pamoja na wewe
 
zitto atuambie ni kigezo gani alichutmia kuset umri wa chini kuwa miaka 35? au kwa kuwa yeye yuko above 35? kuna watu wana miaka 30 nao wanautaka Urais!


UBINAFSI BWANA!

Huyo jamaa wa Kigoma ndiye mshamba zaidi.
Hana mke,hana known track record zaidi ya kubwabwaja bungeni.
Hana hata work experience.

Mbaya zaidi anaingilia mambo ayaonayo tu kwa kuperuzi, na anataka kuyongelea kana kwamba anayafahamu, kumbe ni kujiaminisha tu.

Mtu mwenye uchu wa urais wakati hana miundombinu ya kisisa kumfanya awe hivyo ni hatari.
 
jamani mie nitasupport mtu yoyote atakaeteuliwa na chadema kupepea bendela ya chama awe zitto ama slaa.....
 
ZZK ni bomu linaloandaliwa kuigawa na kuisambaratisha CDM kuelelekea 2015,CCm ikitambua kuwa wafuasi wa zzk nao si haba,inatengeza bomu la kupunguza umri kufanikisha mpango wao huo,kwani ni lini zzk alikana uhusiano wa karibu kati yake na Jack Zoka?
 
Wamechangia wabunge wengi mbona mnamshambulia yeye tu? Au ndio zile agenda zenu lazima apakwe tope Zitto! Go on ZZK siasa ina vikwazo but you will..
 
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), ametaka umri wa kugombea urais ushushwe kutoka miaka 40 hadi kufikia 35.

Zitto ambaye amekuwa akihusishwa na harakati za kuusaka urais mwaka 2015, huku kigezo cha umri kikitajwa kuwa kikwazo, alitoa kauli hiyo jana wakati akitoa maoni yake kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyofika jana mjini hapa kukusanya maoni ya wabunge.

Akitoa maoni yake, Zitto alisema ni ushamba kwa nchi kama Tanzania kuweka umri mkubwa kama sifa ya kugombea urais.

"Umri wa kugombea urais, Rwanda wenzetu wanaruhusu miaka 35, Burundi miaka 35, Kenya miaka 35, Marekani miaka 35, Afrika Kusini miaka 35…Sisi ni ushamba tu, hakuna sababu ya kuweka umri mkubwa," alisema Zitto ambaye wakati akianza kuchangia alitania akisema kuwa itakapofika mwaka 2015 atakuwa na umri wa miaka 39.

Mbali na Zitto, wengine waliounga mkono hoja hiyo ni pamoja na Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Keissy (CCM), Mbunge wa Tarime, Chacha Nyambari Nyangwine (CCM), Mbunge wa Nzega, Dk. Khamis Kigwangwala (CCM), Mbunge wa Viti Maalumu, Dk. Prudenciana Kikwembe (CCM) na Mbunge wa Kasulu Vijijini, Agripina Buyogera (NCCR-Mageuzi).

Chadema wacheni chuki binafsi!
 
ZZK ni bomu linaloandaliwa kuigawa na kuisambaratisha CDM kuelelekea 2015,CCm ikitambua kuwa wafuasi wa zzk nao si haba,inatengeza bomu la kupunguza umri kufanikisha mpango wao huo,kwani ni lini zzk alikana uhusiano wa karibu kati yake na Jack Zoka?

Who is Jack Zoka?
 
humu jF naona kazi ya wengi humu ni kumponda zitto awe mpenzi wa chadema awe wa nyinyiem bado tu mnamwandama zitto.. kiukweli zitto siwezi mdharau maana yeye ndie alienifumbua macho na chadema kilipendwa na watu wengi kipindi cha zitto halafu mnasema pumba gani hapa? kwani mnataka raisi awe mwenye mvi? wana chadema wenzagu tumpe zitto nafasi agombee akishindwa atajua mwenyewe akishinda safi tu ilimradi ccm ametoka pale..kwisha habari
 
Back
Top Bottom