OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Wanamaanisha tupatiwe rais wa kuyumbishwa kama Kabila wa Congo DRC
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwanini iwe umri wa miaka 35 na sie umri mwengine wowote?
Kwa sababu by 2015 yeye ndo atakuwa kaufikisha huo umri. Ikiwekwa 38 atakuwa hana sifa hiyo ya kugombea
Kwa mujibu wa vyanzo mbali mbali, ikifika wakati wa kupiga kura mwaka 2015, Zitto atakuwa na umri wa miaka 39
zitto atuambie ni kigezo gani alichutmia kuset umri wa chini kuwa miaka 35? au kwa kuwa yeye yuko above 35? kuna watu wana miaka 30 nao wanautaka Urais!
UBINAFSI BWANA!
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), ametaka umri wa kugombea urais ushushwe kutoka miaka 40 hadi kufikia 35.
Zitto ambaye amekuwa akihusishwa na harakati za kuusaka urais mwaka 2015, huku kigezo cha umri kikitajwa kuwa kikwazo, alitoa kauli hiyo jana wakati akitoa maoni yake kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyofika jana mjini hapa kukusanya maoni ya wabunge.
Akitoa maoni yake, Zitto alisema ni ushamba kwa nchi kama Tanzania kuweka umri mkubwa kama sifa ya kugombea urais.
"Umri wa kugombea urais, Rwanda wenzetu wanaruhusu miaka 35, Burundi miaka 35, Kenya miaka 35, Marekani miaka 35, Afrika Kusini miaka 35…Sisi ni ushamba tu, hakuna sababu ya kuweka umri mkubwa," alisema Zitto ambaye wakati akianza kuchangia alitania akisema kuwa itakapofika mwaka 2015 atakuwa na umri wa miaka 39.
Mbali na Zitto, wengine waliounga mkono hoja hiyo ni pamoja na Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Keissy (CCM), Mbunge wa Tarime, Chacha Nyambari Nyangwine (CCM), Mbunge wa Nzega, Dk. Khamis Kigwangwala (CCM), Mbunge wa Viti Maalumu, Dk. Prudenciana Kikwembe (CCM) na Mbunge wa Kasulu Vijijini, Agripina Buyogera (NCCR-Mageuzi).
ZZK ni bomu linaloandaliwa kuigawa na kuisambaratisha CDM kuelelekea 2015,CCm ikitambua kuwa wafuasi wa zzk nao si haba,inatengeza bomu la kupunguza umri kufanikisha mpango wao huo,kwani ni lini zzk alikana uhusiano wa karibu kati yake na Jack Zoka?