Hatutaki mapendekezo yao walikuwa wapi siku zote, hizi ni njama za kutaka kuhodhi maoni ya katiba waache wananchi watoe maoni yao/yetu
Hili la urais kuwa miaka 35 linalenga zaidi kuisambaratisha CDM, kwani Mh.Zitto lazima atalianzisha tu hapo 2015.
Hatutaki mapendekezo yao walikuwa wapi siku zote, hizi ni njama za kutaka kuhodhi maoni ya katiba waache wananchi watoe maoni yao/yetu
-Nakubaliana na suala la kushusha umri wa Urais.Inawezekana kuna uwezekano wa kupata wenye uwezo wa kuwa Rais
-Nakubaliana na hoja ya kuwa na approval ya uteuzi wa CDF,Chief Justice,IGP,AG na CAG
-Pia tufikirie kuwa na bicameral parliamentary system.Kama ni uwakilishi tuachane na ukuu wa wilaya na mkoa kwa kufanya decentralization
-Hapo kwa serikali tatu tungekuwa na federal system ambayo inakidhi hoja yangu hapo juu ya decentralization
-Nashindwa kuelewa ni kwa nini wabunge hawajaongelea kuhusu impeachment ya Rais.
Pia ningependekeza vipindi vya urais viwe miaka 4 kwa twi terms
-Pia hapo kwenye bicamneral parliament.Bunge la law chamber liwe miaka 3 kwa vipindi viwili na chaguzi zifanyike kwa kupishana na uchaguzi wa Rais uwe baada ya uchaguzi wa Bunge na magavana
Kwa tulipofikia tutangaze tenda wazungu waje kututawala kwa mkataba tumeshindwa tumejaribu hatuwezi tumelala
sikubaliani na wewe kwenye swala la umri wa raisi. Tunahitaji mtu aliyepevuka vya kutosha. Miaka 35 bado sana!
Binafsi nataka muungano uvunjwe. Kwahiyo hoja ya rais wa z'bar kuwa makamu wa rais inakufa!
Kuna points tatu za kipuuzi kabisa ambazo kwa namna yoyote ile wananchi wazipinge.
1. Umri wa urais usiwe chini ya miaka 40. Cheo cha urais kimeharibika to the point kwamba kila mtu anaona anaweza kuwa rais. Tunahitaji mtu ambaye ameshakuwa tested. Kwa nchi kama yetu ambayo 'institutions' zake sio imara ni hatari sana kuweka rais-mtoto. Na mbaya zaidi Tanzania ina madini mengi, mafuta na gas. Mafioso wengata sana kupata rais-dogo ili wamplekeshe kama Kabila wa DRC.
2. Kipindi cha urais 7 yrs na kiwe kimoja. Mtu aliyetoa hii hoja anatakiwa apelekwe Keko! 7 yrs kama unakuwa na rais mwizi hakutakuwa na kitu kimabakia, na akijua kwamba hana nafasi ya pili atachukua hadi shuka!
3. Mbunge kuwa na mgombea mwenza. Another silly point. Mgombea wa ubunge awe ni mtu mmoja na asimame kwa miguu yake. Bunge la mbeleko ni kitanzi. Maana mgombea mwenza anawajibika kwa nani?
sio zitto tu januari makamba je atatulia ipite kimya hiyo bahati? hata mimi nitagombea kupitia vile vyama vyetu vya dharura na nyongeza mfano cck!
Nyerere alichukua nchi akiwa na umri gani? Na mbona leo anaitwa mpaka baba wa taifa kwa performance yake? Zinduka usifate mkumbo.Hizi hoja walichangia Asubuhi au Jioni?
Kama ni jioni, mmhh! Maana huwa vikao wanakula kwanza mambo yao ya kuvuruga ubongo, wanafikiria Anticlockwise.
Hapo kuna hoja za kipuuzi.
1. Kupunguza umri wa Raisi.
2. Kipindi cha raisi kuwa kimoja cha 7yrs.
3. Mbunge kuwa na mgombea mwenza, huu ni upuuzi uliokithiri.
sikubaliani na wewe kwenye swala la umri wa raisi. Tunahitaji mtu aliyepevuka vya kutosha. Miaka 35 bado sana!
Binafsi nataka muungano uvunjwe. Kwahiyo hoja ya rais wa z'bar kuwa makamu wa rais inakufa!
bunge la kifala sana hili
kama kupevuka kunapimwa kwa umri huu ni wakati wa kuwazungumzia kina mzee makamba, malecela na mtei kuwa wagombea urais!
na huyu aliyetambulika kama rais kijana aliyotutenda tumeyaona na bado anaendelea kutuumiza!
kwetu sisi kama taifa tunahitaji sifa ya ziada kwa rais ajae na hakika umri si suala la msingi ikiwa tutaweka vigezo vingine vya msingi tutakuta umri unajinyambua wenyewe,mfano tukihitaji sifa kiongozi ziwe
1.uadilifu usio na shaka. (lazima kutakuwepo maeneo ya kupima kwa hakika ktk cv ya muhusika)
2.uzoefu katika uongozi. (lazima tutahitaji walau tuone utumishi ktk uongozi wenye ufanisi kabla ya kugombea nafasi ya urais kwa mfano tunaweza kusema muhusika awe kwenye uongozi walau kwa awamu mbili za miaka mitano)
3.elimu, uelewa na ujuzi wa mambo.