Wabunge wataka Umri wa kugombea Urais uwe 35; Zitto asema umri mkubwa ni ushamba

Wabunge wataka Umri wa kugombea Urais uwe 35; Zitto asema umri mkubwa ni ushamba

Taratibu rangi halisi za ZZK zinajidhihirisha,umri ushushwe hadi 35,na kipindi kiwe miaka 7!
 
Kweliii nchii hiiii natamani niombeeee uraia naona tunaelekea kuzimu
 
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), ametaka umri wa kugombea urais ushushwe kutoka miaka 40 hadi kufikia 35.
Zitto ambaye amekuwa akihusishwa na harakati za kuusaka urais mwaka 2015, huku kigezo cha umri kikitajwa kuwa kikwazo, alitoa kauli hiyo jana wakati akitoa maoni yake kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyofika jana mjini hapa kukusanya maoni ya wabunge.
Akitoa maoni yake, Zitto alisema ni ushamba kwa nchi kama Tanzania kuweka umri mkubwa kama sifa ya kugombea urais.
“Umri wa kugombea urais, Rwanda wenzetu wanaruhusu miaka 35, Burundi miaka 35, Kenya miaka 35, Marekani miaka 35, Afrika Kusini miaka 35…Sisi ni ushamba tu, hakuna sababu ya kuweka umri mkubwa,” alisema Zitto ambaye wakati akianza kuchangia alitania akisema kuwa itakapofika mwaka 2015 atakuwa na umri wa miaka 39.
Mbali na Zitto, wengine waliounga mkono hoja hiyo ni pamoja na Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Keissy (CCM), Mbunge wa Tarime, Chacha Nyambari Nyangwine (CCM), Mbunge wa Nzega, Dk. Khamis Kigwangwala (CCM), Mbunge wa Viti Maalumu, Dk. Prudenciana Kikwembe (CCM) na Mbunge wa Kasulu Vijijini, Agripina Buyogera (NCCR-Mageuzi).
Kwa upande wake, Keissy alipendekeza umri wa kugombea urais iwe kati ya miaka 35-40 kwani umri huo ni watu wenye nguvu.
“Hii nchi ni kubwa sana… ina milima na mabonde, tunataka rais ambaye ataweza kutembea nchi nzima na mabonde yake, hatutaki kusikia rais ambaye baada ya siku mbili tukasikia ameenda India, Pakistan kutibiwa,” alisema.
Nyangwine alipendekeza miaka 35 na kuendelea na kuongeza kuwa, hali hiyo itatoa nafasi kwa vijana kushiriki, huku Dk. Kigwangala akisema haoni sababu ya umri kuwa zaidi ya miaka 35 kwa mtu kuwa rais.
Zitto amekuwa akitajwa kuusaka urais 2015, huku akipigania sifa ya umri kwa mtu kuwa nafasi hiyo ipunguzwe kutoka miaka 40 kwa mujibu wa katiba ya sasa hadi 35.
Tayari mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini amewahi kukaririwa mara kadhaa akisema kuwa hana mpango wa kugombea tena ubunge ifikapo mwaka 2015, badala yake anajipanga kuwania urais.
Mbali na hoja hiyo ya umri wa urais, nyingine ambayo ilionekana kuwagusa wabunge wengi ni ile ya Muungano.
Wabunge wengi hasa wa kutoka Zanzibar, walionekana kutotaka Muungano uvunjwe, badala yake walipendekeza kuwe na muundo mwingine tofauti na wa sasa.
Walipendekeza mifumo mitatu ya muundo wa Muungano. Muundo wa kwanza ni ule wa serikali tatu, muungano wa mkataba na tatu muungano wa kuwa na rais mmoja na mawaziri wakuu wawili; mmoja kutoka Tanzania bara na mwingine Zanzibar.
Wabunge waliopendekeza mfumo wa serikali tatu ni pamoja na Mbunge wa Mkanyageni, Mohamed Habib Mnyaa (CUF), ambaye alitaka pia uongozi uwe wa mkataba baada ya ule wa serikali mbili.
“Mfumo wa sasa umeleta matatizo sana, mimi napendekeza iwepo Serikali ya Bara ambayo sijui mtaamua kuiita Mzizima au lolote na ile ya Zanzibar, na Rais wa Muungano achaguliwe na wananchi wote kulingana na mzunguko wa kubadilishana,” alisema mbunge huyo.
Baadhi ya wabunge waliopendekeza muundo wa serikali tatu na ule wa mkataba ni pamoja na Mbunge wa Tumbe, Rashid Ali Abdallah (CUF), Mussa Kombo (Chake Chake), na Kombo Hamis Kombo (Magogoni) ambao wote ni wabunge wa CUF.
Wengine ni wabunge wa viti maalumu, Easter Bulaya na Diana Chilolo, wote kutoka CCM.
Kwa upande wa wabunge waliokuwa wakiunga mkono mfumo wa serikali mbili, wengi wao walionekana kuwa ni wa CCM.
Miongoni mwao ni pamoja na Mbunge wa Manyoni Mashariki John Chiligati (CCM), Mbunge wa Bunda, Steven Wassira (CCM), Mbunge wa Dole, Silvester Mabumba (CCM), Mbunge wa kuteuliwa na Rais, Zakhia Meghji, Mbunge wa Iramba, Mwigulu Nchemba (CCM) na wengine. Hata hivyo, wabunge hao waliokuwa wakitetea muundo wa serikali mbili walipendekeza uwepo utaratibu wa kushughulikia kero zinazowakabili Wazanzibari, huku wakitaka iundwe tume ya kushughulikia kero hizo.
Wengine walipendekeza Zanzibar iachwe huru katika masuala ya mafuta, bandari pamoja na kutaka isaidiwe kiuchumi.
Katika hilo, Chilligati alisema; “Kama muungano ungekuwa ni sumu inayojaribiwa, tungethubutu kuuvunja kwa muda kidogo, kule Zanzibar Watanzania elfu 15, na Wanzanzibari walioko bara laki 2.5 waonje adha ya kutafuta hati ya kusafiria au waambiwe wahame, tungejaribu kufanya hivyo.”
Alikosoa mfumo wa serikali tatu, Chiligati alisema unaongeza gharama kwa sababu utahitaji Baraza la Mawaziri na rais mwingine, na kwamba Tanganyika iliyokufa itabidi ifufuliwe.
Mbali na hilo, suala la mgombea binafsi nalo lilichukua nafasi kubwa katika maoni waliyokuwa wakichangia wabunge hao.
Wabunge wengi walipendekeza Katiba ijayo itamke wazi juu ya mgombea binafsi, ikiwa ni pamoja na uwepo wa Mahakama ya Katiba.
Aidha, wabunge wengi walitaka viti maalumu viondolewe na kupendekeza mfumo mwingine wa kuwanyanyua wanawake, ikiwa ni pamoja ule wa kutaka mbunge anayesimama katika jimbo asimame na mgombea mwenza mwanamke na atakapopita, mgombea mwenza naye atakuwa mbunge.
Suala la ukubwa wa madaraka ya rais nalo lilionekana kuwagusa wabunge wengi, ambao karibu wote waliochangia wakiwamo wachache wa CCM, walitaka yapunguzwe.
Pia walitaka utaratibu wa mawaziri kutokana na wabunge, ufutwe na kupendekeza mawaziri wateuliwe nje ya Bunge na wawe wataalamu wa wizara husika.
Kuhusu suala la mihimili mitatu, yaani Serikali, Bunge na Mahakama, wabunge wengi waliotoa maoni walitaka Katiba ijayo itamke wazi kuwa ni kosa kuingiliana na mihimili mingine.
Kwa upande wa wahujumu uchumi, baadhi ya wabunge waliotoa maoni walitaka watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo wanyongwe.
Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali (NCCR-Mageuzi), alisema hakuna sababu ya kulinda haki ya mhujumu uchumi ambaye amepewa mabilioni ya fedha kwa ajili ya kununulia dawa na badala yake anaweka fedha mfukoni halafu unalinda haki ya mtu mmoja.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, ambaye alipata wakati mgumu, alisema kabla ya kuanza kukusanya maoni kwa wabunge alipata woga.


[TD="bgcolor: #ffffff"]
Zitto: Umri kuwania urais uwe 35
• Asema ni ushamba kuweka umri mkubwa kama sifa ya kugombea urais

na Ratifa Baranyikwa, Dodoma


[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF, align: center"]
amka2.gif
[/TD]
:crazy::crazy:
 
Hakuna jipya...kwanini hawajaongelea kuhusu mshindi wa Urais kuwa na absolute majority (50+1)? Mshindi wa pili anatakiwa kuwa Kiongozi wa Upinzani bungeni...mgombea binafsi..Kuondolewa kwa nafasi ya Makamu wa Rais (Kama tutakuwa na Waziri Mkuu) au kuondolewa kwa nafasi ya Waziri Mkuu kama tutakuwa na Makamu wa Rais... Wizara nyingi zisiwe na Manaibu waziri n.k
 
Huyu dogo ndiye mshamba anatumiwa na magamba kutaka kuisambaratisha CDM lakini hataweza,ashindwe na kulegea.



zitto atuambie ni kigezo gani alichutmia kuset umri wa chini kuwa miaka 35? au kwa kuwa yeye yuko above 35? kuna watu wana miaka 30 nao wanautaka Urais!


UBINAFSI BWANA!
 
Mimi huwa namdharau sana mtu ambaye reference yake ni 'mbona wenzetu' bila kueleza faida ya hicho wenzetu wanachopata juu ya jambo hilo.

Kuna jambo huyu bwana mdogo anaamini, si zuri sana kwake na kwa taifa. Sidhani kama ana wapenzi zaidi ya washabiki. Hiyo ndoto yake haitaishinda CCM bali itaishinda CDM na kuharibu mipango ya yoote iliyochukua muda kuifikisha hapa ilipofika.

Na huu ndio utoto wenyewe hasa. Ni rahisi tu kugombea Urais na miaka 35 lakini kushinda uchaguzi na umri huo ni ndoto kwani utoto wake bado unaonekana live. Ana ndoto za kufungia ndoa ikulu
 
Hiyo ya kupunguza umri wa ugombea uraisi itanifanya niikatae katiba hata kama mengine yatakuwa mazuri kiasi gani.Tunahitaji Raisi mwenye Uzoefu wa kutosha na kwa miaka 35 bado sana.Zitto huu ni uchu wa madaraka,subiri mda utafika.
 
Mr. Mkira mi naona kama ni hivyo umri wa kugombea urais ushushwe hadi miaka 18 ili tuheshimu katiba yetu inayompa haki kila mtu aliye na miaka 18 haki ya kuchagua na kuchaguliwa,nasubiri nami nitoe maoni yangu kupitia kwenye makundi maalum.
 
Mimi ningependa ushuke chini ya hapo, uwe kuanzia 22 tu.

Kwanini tunawadharau vijana? wakati inajulikana kuwa umri wa kuchapa kazi ni ujanani.
 
ni ushamba zaid kutaka kubadili mfumo wa sheria eti tuu kwa sababu kuna mtu mmoja asiye na busara wala uzalendo anayetamani kuwa rais.
 
Kwanini iwe umri wa miaka 35 na sie umri mwengine wowote?
 
Mods huu uzi uunganisheni na uzi uliokuwepo tangu juzi hapa!

Tumechoshwa na habari za huyu kijana kila kukicha lazima aje na vituko, hana tofauti na Wema Sepetu, Anti Ezekiel na wengine!
 
Mr. Mkira mi naona kama ni hivyo umri wa kugombea urais ushushwe hadi miaka 18 ili tuheshimu katiba yetu inayompa haki kila mtu aliye na miaka 18 haki ya kuchagua na kuchaguliwa,nasubiri nami nitoe maoni yangu kupitia kwenye makundi maalum.

Ntakuwa na amani nikiku support wewe,una base na hoja yako, sio kwasababu usa wanafanya.uliwahi ona usa wana Raisi mwenye umri chini ya 45? zitto huna hoja,yako ni kuwa umezidi miaka 35 tu.bora hii ya kutimiza haki ya kila mtanzania kikatiba.kuchagua na kuchaguliwa.unaweza kusikilizwa na watu wenye akili.
 
Ushamba? Agha! Anataka Rais Sharobaro kitu mlege hadi magogoni...lol Seriously Zitto hii kwangu ni a bit immature na inazidi kudhihirisha kinachopikwa kichwani mwako
 
Back
Top Bottom