Wabunge Wetu, Macho ya Watanzania Wote Leo ni Kwenu!. Maslahi ya Taifa Mbele!. Tuwaogope Kama Ukoma Muflis Hawa!, Kama Huwezi, ni Lazima Usaidiwe Tuu!

Hii Bahar bora isingekuwepo tuu....tuwe na mbuga na hifadhii tuu na animals wawe nyumbu na fisi tuu eeh kila mtu afe kivyake
 
Nafkiri kila mtu Ana haki ya kusimamia na kusimamia pale anapoamini kuliko kuaminishwa.
Kwa hiyo ukiamini Tanzania ipo kwenye bara la Asia uachwe tu?Kuna imani na reality.Kuna mambo huaminishwi ni jinsi yalivyo hakuna mwanya wa kutafsiri.Ukweli ni ukweli na uzushi ni uzushi.Utachagua tu upande.
 
Hili jambo limepita ,Tanzania ina mambo ya kimchongo sana na ndo mana wachache ndo wanufaikao.
Wabunge waliomo ni ccm na tena walipitishwa kimchongo kwa manufaa ya ccm unazani ni kipi kipya cha maana hapo,siku zote watatazama faida inayoingia mifukoni mwao na si kwa watanzania

Nafasi pekee na mchango pekee wa mtanzania alio bakiziwa ni ulipaji kodi na tozo za moto,hayo mengine ni ya walamba asali na wagonga meza
 

Hongera Bunge letu kusupport kila kitu cha serikali, hata madudu!.
Hongera Wabunge wetu kujadili mlicholetewa kwenye karatasi bila kufanya homework yoyote!.
Hongera Spika Dr. Tulia, Mwanasheria mbobezi mbobevu kuruhusu Inter Governmental Agreement na kampuni inayojifanya ni serikali ya Dubai bila Bunge letu kufanya a due diligence report!.
P
 
Reactions: Tui
Kwa hiyo ukiamini Tanzania ipo kwenye bara la Asia uachwe tu?Kuna imani na reality.Kuna mambo huaminishwi ni jinsi yalivyo hakuna mwanya wa kutafsiri.Ukweli ni ukweli na uzushi ni uzushi.Utachagua tu upande.
Vivo hivyo usivyotaka watu kuachwa kwa wanachokiamini na wao hawatakuacha kwa unachokiamin.
 
Nimefuatilia mjadala huu mwanzo mwisho, Bunge limeridhia, maslahi ya taifa yamezingatiwa.
Hongera Bunge letu
Hongera Wabunge wetu
Hongera Spika Tulia.
P
"Something fishy" yes, Samia kahongwa kitu akatutoa sadaka, iko siku atalipa, hata mbele za Mungu.
 
Tanzania ni nchi sovereign, Dubai sio sovereign, Government inawezaje kuingia mkataba wa kiserikali na taasisi isiyo sovereign?. Nchi ni UAE na sio Dubai!.
Yawezekana, hisia zangu kuwa hawa DP wanaweza kuwa wametapeliwa huko na labda na huku! Zikawa za mashaka!!!
 
Ukweli ni kwamba, kinachoongelewa siyo mkataba wa kuendesha, kukodi au kuuaza bandari. Kinachoingelewa ni mkataba wa maridhiano ya ushirikiano wa kimaendeleo baina ya nchi mbili.

Umeelewa?
Article 23(4) umeisoma na kuielewa? Mbona kama imerukwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…