Wanabodi,
Leo asubuhi hii waheshimiwa wabunge wetu, wataujadili mkataba wa IGA ( Intergovernmental Agreement), na baada ya hapo ndipo HGA ( Host Government Agreement) zitaingiwa kati ya TPA na DPW baada ya IGA kupitishwa.
IGA kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya Dubai, kuruhusu kampuni ya DP World ya Dubai, kutuboreshea Bandari zetu.
Huku mitaani na kwenye mitandao ya kijamii kumeisha anza kuibuka makundi sogozi yanayoleta uhayawani wa sentiments za kibaguzi, Mwarabu wa Oman anataka kumpa Bandari yetu Mwarabu wa Dubai hivyo Watanzania Wazalendo tusikubali!. Hawa ni muflis!.
Kule nyuma nilipopandisha pandisha bandiko hili
Udhalimu wa Waarabu Zanzibar na Pemba: Ndugu zetu waliteswa, hasiwa, bakwa, na kuuawa kinyama nilitoa angalizo hili
Angalizo hili ni muhimu sana kwenye mjadala wa leo mule Bungeni kwetu. Tunawategemea kuwasikia waheshimiwa wabunge wetu wakitanguliza mbele maslahi ya taifa letu katika kulijadili hili la DP World. Hatutarajii kabisa kutokea mbunge mmoja yoyote muflis kuipinga DP World kwa Uarabu wao, kwa hoja za kibaguzi za Mwarabu ni Mwarabu tuu, awe ni Mwarabu wa Oman, Mwarabu wa Dubai, Mwarabu wa Arabuni, Mwarabu wa Zanzibar, Mwarabu ni Mwarabu tuu ni wale wale na mambo yao ni yale yale..., watu wa type hii ni ma hayawani!, hatutegemei kabisa uhayawani huu ukaibuka kwenye mjadala huu!.
Naendelea kusisitiza, ikitokea wewe huwezi jambo fulani, lazima utasaidiwa tuu!, utake kusaidiwa, utasaidiwa, usitake kusaidiwa, utasaidiwa!, mpaka pale utakapoweza kujisaidia!
Watanzania tujifunze kujikubali kuwa kuna vitu hauwezi, na tunaposhindwa tukubali kusaidiwa au tukomae? Baada ya Bandari ni ATCL na SGR au Tusubirie?
Nawatakia waheshimiwa wabunge wetu mjadala na majadiliano mema kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa.
Paskali