Taarifa hizo ni kama ajali, mwendokasi wa chombo cha moto na kadhalika. Hii itasaidia sana watu katika kufuatilia usalama wao. Pia endapo programu hii itawezeshwa kwa gprs, zitawekwa sehemu muhimu katika barabara kubwa ili kuwaelekeza wateja sehemu rasmi za kuvuka barabara (zebra crossing).
Pia sehemu zenye hatari kama vile madaraja, maporomoko, misitu na kadhalika zitawekwa pia gprs ili kumsaidia mtu kufahamu mazingira hatarishi mapema hata kabla ya kufika katika eneo husika. Hii itawasaidia watu kupata taarifa mapema ili wawe na tahadhari kabla ya kufika eneo husika.
Pia katika application hii, kutakuwa na sehemu ya kuwafahamu madereva wa bodaboda ambao wanaleseni na ambao hawana makosa ya barabarani, hii application itaunganishwa na mfumo wa trafic police ambao watakuwa wanajaza taarifa muhimu za dereva wa bodaboda kama vile leseni, makosa ya barabarani na kadhalika.
Hii itamsaidia mteja kufahamu taarifa muhimu za dereva baada ya kuingiza namba ya pikipiki. Taarifa hizo ni kama picha ya dereva husika na taarifa za dereva kama ana leseni au hana. Jina la dereva wa bodaboda halitakuwepo ili kuzuia dereva wa bodaboda kujulikana jina na kutapeliwa kwa urahisi.
Mteja anapofika katika mgundi wa pikipiki anaweza kuingiza namba za pikipiki na kupata taarifa muhimu za hiyo pikipiki. Ili mteja awe na amani pale anaposafiri kwa usafiri wa bodaboda kwa sababu bodaboda nyingi nchini zinaongoza kwa kupata ajali au kufanya matukio ya uhalifu.
Pia kutakuwa na utaratibu wa kutoa taarifa kwa pikipiki iliyoibwa. Taarifa inaweza ikatolewa na mmiliki wa pikipiki pamoja na dereva wa pikipiki hiyo. Baada ya kuweka taarifa za wizi wa hiyo pikipiki watumiaji wengine wa programu hiyo (safe journey application) wanaweza kutoa taarifa ya kuonekana kwa pikipiki hiyo endapo atabahatika kuiona.
Na endapo atafanikisha kupatikana kwa pikipiki hiyo, atapewa zawadi ya Tshs 50,000/=. Kiwango cha zawadi ni kidogo kwa sababu kama kitawekwa kiwango kikubwa watu wanaweza wakafanya dili la kupata pesa. Pia kwa kuweka kiwango kidogo ni ngumu mtu aibe halafu badala ya kwenda kuiuza apate milioni na akakubali kupata elfu 50 kitu ambacho hakiwezekani hata kidogo.
Pia baada ya kupatikana taarifa sahihi ya pikipiki iliyoibwa na kufanikisha kupatikana kwa pikipiki hiyo, ndio zawadi itatolewa. Kama pikipiki itakuwa na gprs kila mtumiaji wa application hii atafanikiwa kuiona ile pikipiki na ufuatiliaji wake unaanzia hapo. Hii inaweza ikapelekea watoataarifa wakawa wengi wanaofuatilia pikipiki moja, na zawadi ni ya mtu mmoja tu. Zawadi itatoka kwa mtoataarifa mmoja au itategemea mwenye mali baada ya kuipata pikipiki yake ataamua vipi.
Si hayo tu, bali mambo mengi yatafanyika kwenye application hii ili kuhakikisha watoto na hata watu wazima wanaendelea kuwa salama. Si hilo tu, bwana Kingambe akabuni ramani za milango na mageti salama kwaajili ya usalama wa watoto wadogo pale ambapo mlango utajifunga ghafla, ikiwa mtoto ameshika upande wa mlango kule kwenye bawaba au upande ule ambao kinakaa kitasa asiumie.
Kwa mfumo huu, watoto wataendelea kubaki salama kutokana na ajali za kubanwa na milango. Hili litawezekana kwa kuweka uwazi wa kupita vidole vya wato pande zote mbili. Upande wa zinapowekwa bawaba na upande vinapowekwa vitasa. Hii itawaokoa wakubwa pia kutokana na ajali za kubanwa na milango au mageti.
Dhumuni ya milango hii ni kutumika katika taasisi zinazokusanya watu wengi kama vile mashule, vyuo, na hata katika nyumba za ibada. Pia milango hii inaweza pia kutumika majumbani. Katika masuala ya elimu aliandaa hesabu ambazo alikuwa na lengo zitumike katika kipindi ambacho angekianzisha katika runinga.
Kipindi hicho alikiita jina la "kuwa mbunifu katika hesabu" (be creative in mathematics) Lengo la kipindi hicho lilikuwa ni kuwafanya watu hasa wanafunzi waipende hesabu. Aliziongeza njia mbili za kufanya maswali ya quadratic equation.
Njia ya kwanza ni kujaribu kama jibu ni a. Njia ya pili ni kujaribu kama jibu ni b, na njia ya tatu ni kujaribu kama jibu ni c. Lilimjia wazo hili kutokana na kuwaza, unatafuta jibu wakati jibu lipo katika swali ambalo ni a, b au c.
Kama moja ya jibu ni "a", kuna kanuni ya kulithibitisha hili. Kanuni hiyo ni a3+ab+c=0. Kama hiyo kanuni itakubali basi moja ya jibu ni a. Hivyo x1=a, na x2=c/2a.
Pia kama jibu ni "b", kanuni ifuatayo itakubali b2(a+1)+c=0. Ikikubali kanuni hiyo x1=b na x2=c/b. Pia endapo jibu mojawapo ni c. Kanuni ifuatayo itakubali ac+b+1=0. X1=c na x2=1/a. Hizi zitawasaidia hata walimu katika kutunga maswali.
Pia kuna jambo napenda kuliweka sawa. Hili ni tatizo la walimu wengi wa hesabu Tanzania. Tatizo hilo ni katika mada za kidato cha pili exponents na logarithms. Badala ya kufanya ulinganifu wa pande mbili wao wanagawanya base kwa kukata kitu ambacho si sahihi. Mfano kama 2power4=2powerm, kisha wanakata 2 ya upande wa kulia na ile ya upande wa kushoto na kubakiwa na m=4, kitu ambacho si sahihi. Jibu ni sahihi ila njia si sahihi. Njia sahihi ni kulinganisha pande mbili, kulia na kushoto bila kukata chochote.
Tatizo hilohilo pia linajitokeza katika logarithm. Badala ya kufanya ulinganifu kati ya upande wa kulia na wa kushoto, wengi wao wanagawanya. Mfano log42=log4x. Kupata thamani ya x wanagawanya kwa log4 pande zote mbili na kubakiwa na x=2, kitu ambacho si sahihi. Kinachofanyika hapa ni ulinganifu 9upande wa kulia na upande wa kushoto.
Upande wa kulia una neno log na upande wa kushoto una neno log pia. Vilevile zote mbili zina base sawa. Hivyo ili kitu chote cha upande wa kushoto na kile cha upande wa kulia lazima x iwe sawa na 2. Na maswali haya badala ya kutumia njia ya kulinganisha, unaweza ukatumia njia ya quotient rule.
Chukua namba za upande mmoja peleka upande mwingine. Kisha tumia quotient rule kupata jibu.

Upvote
1