Wachaga: Geita na Chunya kuna Madini, nendeni huko!

Kangomba imenishinda aisee bei zipo juu mno nilikuwa na vituo mdimba na mambamba na namkomolela aisee nimefuata pesa zangu jana wanunuzi ni wengi mno na bei imenitisha 2400 hadi 2500
Bei hiyo sio rafiki, lengo la kangomba mnunuzi upate faida

Lakini kwa hizo bei, unaweza jikuta wewe ndiyo inakula kwako

Mimi niliwakopesha hela kwa korosho, kwaajili ya maandalizi ya kulima, kwahiyo hapa nakusanya mzigo wangu kadri nilivyokopesha

Tafuta ekari kadhaa uwe unalima lima pia
 
inaitwa kula maua....bila shaka ulikopesha sh 1000 kwa kilo
 
Hongera sana Mkuu, kama una mtaji fungua kiwanda kidogo uwe unabangua na kuuza roasted

Ukiwa mjini, hizo roasted zinauzwa ghali sana
Mji kama dar? Kwasababu mimi nipo huku kusini tu napiga mishe masasi na biashara hiyo sio kubwa sana...labda unipe mwanga zaidi kuhusu hilo mkuu
 
Mji kama dar? Kwasababu mimi nipo huku kusini tu napiga mishe masasi na biashara hiyo sio kubwa sana...labda unipe mwanga zaidi kuhusu hilo mkuu
Ndiyo Mkuu, mji wa DSM lakini nafikiri hadi majiji mengine kama Arusha wanaweza kuwa na wateja wazuri

Ukienda supermarket hapa mjini, nusu ya hizo roasted wanauza 20,000 na wengine 15,000

Kwahiyo ni suala la kuongeza thamani tu ya bidhaa yako
 
Nilivyosoma tu "wamesambaa dunia nzima kuliko wachina" nimeacha kusoma, kumbe mwehu mlevi amevamia jukwaa
 
Ndio kwa kilo..kuna vijana wanakuwa kwenye pikipiki na spika zao na mizani ndio wananunua hizo korosho zilizobanguliwa kwa bei ya 15000 ila bila shaka bei imeanza kupungua kwasababu siku 5 nyuma bei ilikuwa 17500 kwa kilo
Hata kwa hiyo 17,500/Kg bado ilikuwa inawalipa

Maana wao wanauza 30,000 kwa kilo, which means wanaingiza 12,500 kwa kilo kabla ya gharama za uendeshaji
 
mbona wapo wa kutosha sema hawanaga mbwembwe zile za kishamba tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…