Speaking from experience kabisa...mama yangu mdogo alizaa na kijana wa kichaga (Marangu) mama mkwe wwke akasema kitovu kitumwe hata kwa Bus kutoka Dar kwenda Kilimanjaro na kweli alifanya hivyo! Waliishi na yule baba kwa muda wa miaka3 then wakaja kushindwana,wakatengana...yule mzazi mwenzie akadai apewe mtoto mamdogo alikataa kwa kihezo kua yule mtoto bado ni mdogo hata miaka 4 hajafikisha...mvutano ulikua mkubwa na kibaya zaidi mamdogo kipato kilikua kikubwa kulinganisha na yule mzazi mwenzie...walimtolea kauli kali kua "unagombana na ndugu yetu na kumringia kisa una kazi nzuri hivyo una unamdharau na mtoto umemchukua,tutaona km huyo mtoto utamfaidi" baada km ya mwaka mtoto aliumwa umwa magonjwa yasiyoeleweka tu ila hakuja aliehidi ni imani za kishirikina mpk hali ilivyokua serious ndio mtu akamshtua,kwenda kwa hawa wataalamu wa jadi cha kwanza alimuuliza kitovu cha huyu mtoto ulimkabidhi nani? Au ulikitupa wapi? Kbl hajajibu akamwambia ntaweza kumtibu huyu mtoto kupona huu ugonjwa anaoumwa ila ufahamuwake siwezi kuurudisha sababu kitovu chake ndicho kimetumika kumfunga...basi mtoto yule kiafya sasa hv ni mzima ila mpk leo hii ana miaka 10 hajui kusoma wala kuandika kabadilisha shule mpk kachoka na ukikaa kwa makini na yule mtoto utagundua km alitaka kupata utaira flan hv hata kwa maongezi na jinsi anavyorespond while at the age of two years kalikua katoto sharp na kajanja sana!
Mtu yoyote asikurubuni umpe kitovu cha mtoto wako...kitupe unapopajua mwenyewe tu..nchi ina ujinga mwingi sana hii na washirikina si watu wazuri.