Hiyo ni mila fulani common sana kwa jamii nyingi za kichaga (japokuwa kwa sasa imepungua kwa sababu ya elimu, utandawazi, imani za kikristo/kiislamu, kuoa na kuolewa kwenye makabila tofauti na watu kukimbilia kuishi zaidi mijini).
Kwa kifupi sana, mila nyingi za kichaga haziruhusu mwili au kiungo cha mwili (kama kitovu, magovi) kutupwa au kuzikwa kiholela holela, wao wanataka vizikwe kwenye ardhi yao na wawe na urahisi wa kufanya matambiko yao sehemu hiyo ili mizimu iwape baraka au kuwalinda dhidi ya majanga.
Matambiko ya kichaga yamejikita kwenye kumwaga pombe ya mbege, kutupia nyama iliyochomwa/kupikwa na kutamkia maneno kwenye eneo ilipozikwa miili au hivyo viungo na kupandwa kwa majani ya sale.
Matambiko=Ushirikina=Uchawi